SoC03 Ulinzi wa Bima kwa mtu wa tatu

Stories of Change - 2023 Competition

Loran

Member
Jun 7, 2023
52
337
Utangulizi
Maana ya Bima
Bima ni mfumo wa ulinzi au fidia ambao unamuwezesha mtu au shirika kulinda mali zao au kujilinda dhidi ya hatari au hasara ambazo zinaweza kutokea. Kuna aina mbalimbali za bima mfano bima ya Afya, bima ya vyombo vya moto, bima ya maisha, bima ya moto n.k.
Aina ya bima za vyombo vya moto
  • Bima kubwa ( comprehensive cover).
  • Bima ndogo ( Third party only).
  • Bima ndogo + moto na wizi ( third party, fire and theft)
katika andiko hii tutazungumzia sana kuhusu Bima ndogo (Third party only). Bima hii ni muhumu sana katika vyombo vya moto na pia ni lazima kisheria.
Aina hii ya bima humlinda mmiliki wa chombo Cha moto endapo atagonga Mali za watu wengine mfano gari, duka, pikipiki n.k. lakini pia itamlipia fidia kwa uharibifu wowote au vifo kwa binadamu au wanyama. Endapo atamsababishia kifo au kilema mtu wa tatu, Dereva Atatakiwa kulipa fidia, hivyo bima hiyo itamsaidia kulipa madai hayo

Hivyo basi ikiwa umepata ajali kwa kugonga mtu au mali ya mtu, arafu chombo chako pia kimeharibika basi bima hiyo itamlipa yule uliyemgonga ila wewe na chombo chako hamtapata malipo yoyote isipokuwa abiria uliowapakiza

Kulingana na Sheria ya Bima ya Tanzania ya mwaka 2002, sura ya 169, kifungu Cha 04, inamlazimu kila mmiliki wa chombo Cha moto haruhusiwi kuingia barabarani kama hana bima angalau akate bima ndogo ambayo ipo kwaajili ya kumlinda mtu wa tatu. Mtu wa tatu katika bima ni kama vile abiria, watembea kwa miguu, dereva mwingine au mtu yeyote ambae atasababishiwa madhara na mmiliki wa chombo Cha moto.

Haki za abiria na watembea kwa miguu

Faida ya bima ndogo ni kumlinda mtu wa tatu kutokana na madhara kama kuharibiwa Mali, ama kusababishiwa ukilema, vifo n.k

Mahakama ina mpa haki mtembea kwa miguu au abiria kulipwa endapo atasababishiwa hasara au madhara yoyote na chombo Cha moto, haki hizo ni kulipwa fidia kama ifuatavyo
  • Gharama za matibabu
  • Gharama za kuendesha kesi endapo mtu wa tatu akishinda kesi hiyo
  • Fidia ya vifo au ukilema Cha aina yeyote
  • Uhalibifu wa Mali ( gari, nyumba, duka n.k )
    images (1).jpeg
    picha kutoka mtandaoni
utaratibu wa kufuata wakatati wa kudai fidia.
Wajibu wa mtu wa tatu (third party person) katika kuhakikisha analipwa fidia baada ya ajali . Kwa ujumla, mtu wa tatu anaweza kuchukua hatua zifuatazo:

Ripoti ajali: Kwanza kabisa, anapaswa kuhakikisha kwamba anaandika taarifa kamili ya ajali na kutoa ripoti kwa polisi au mamlaka husika mara moja. Ripoti hii itakuwa na maelezo muhimu kuhusu ajali, ikiwa ni pamoja na sehemu na tarehe ya ajali, maelezo ya watu waliohusika, na maelezo ya uharibifu uliotokea.

Kutoa ushahidi: Mtu wa tatu anaweza kuwa shahidi muhimu katika kuthibitisha jinsi ajali ilivyotokea na ni nani aliyesababisha ajali. anaweza kutoa taarifa na ushahidi wao kwa polisi, mamlaka husika, au kampuni ya bima ili kusaidia katika uchunguzi na madai.

Kutoa taarifa na ushahidi: Mtu wa tatu anaweza pia kuwasilisha taarifa na ushahidi unaohusiana na ajali na madai ya fidia. Wanaweza kuandika taarifa ya ushahidi wao, kutoa maelezo ya tukio, na kutoa ushahidi wa picha au video ikiwa inapatikana. Ushahidi huu unaweza kuwa muhimu katika kujenga hoja za fidia.

Kutoa ushahidi wa gharama: Ikiwa mtu wa tatu ameshuhudia hasara ya mali au uharibifu uliosababishwa na ajali, anaweza kusaidia kwa kutoa ushahidi wa thamani ya mali iliyoharibiwa au gharama zinazohusiana na ukarabati. Hii inaweza kusaidia katika kuthibitisha madai ya fidia yanayohusiana na uharibifu.

Kushirikiana na mamlaka husika: Mtu wa tatu anaweza kushirikiana na polisi, mamlaka za barabarani, au mamlaka zingine zinazohusika katika uchunguzi wa ajali. Hii inaweza kusaidia kuhakikisha kuwa haki inatendeka na kwamba pande zote zinazohusika zinatoa ushirikiano wao katika mchakato wa madai.

Mapendekezo kwa mamlaka ya bima (TIRA) na serikali
hivi karibuni kumekuwa na malalamiko mengi sana kutoka kwa wadau/ washiriki wa bima kutotendewa haki, pia watu mbalimbali kutopata haki zao baada ya ajari.
Serikali na mamlaka ya bima Tanzania (TIRA) wanapasa kutoa elimu muhimu kwa wateja wa bima kuhusu faida za bima, utendaji kazi wa bima, mipaka, na vitu vinavyopelekea usilipwe. Pia elimu kwa wamiliki wa vyombo vya moto kuhusiana na bima itawafanya wanunue vifurushi sahihi na vyenye tija kwao.

Elimu hiyo ijikite kuelimisha kuhusiana na haki za raia na mali zao , iweke wazi kuwa abiria au watembea kwa miguu wanapopata ajari kwa kugongwa na vyombo vya moto yawapasa kufungua kesi za madai na sio kumalizana kienyeji.
Bila kusahau elimu kwa madereva watakapo sababisha ajari/madhara kwa raia au mali wasikimbilie kutoa pesa za kupooza au kukimbia maana jukumu la malipo sio lake hivyo yampasa kuangalia usalama wake wakati akisubili hatua za kisheria zitazo mfanya asimkoseshe fidia muhanga wa ajari hio.

Ushauri
Kumekuwa na mijadala mingi kususiana na Bima , watu wengi wana mitazamo dhanifu kuhusu bima , wengi wakisema kuwa bima ni utapeli lakini ukweli ni kwamba ukosefu wa elimu ya bima umeenea sana kwa jamii ya Tanzania na kuitizama bima kama ni wizi au utapeli kitu ambacho sicho.
wahanga wote wanaopata madhara kutokana na vyombo vya moto wanapaswa kufungua kesi za madai, endapo amepoteza maisha muhanga wa ajari hio basi ndugu zake wana haki ya kudai fidia na ikumbukwe kua endapo muhanga anacheleweshewa fidia zake anapaswa kwenda (TIRA) kutoa taarifa upesi

Watu hununua bima kwa mazoea bila kujua ni aina gani ya bima inatoa fidia zipi na nani hulipwa fidia hizo . Kiukweli bima hufuata misingi ya sheria kumtaka mteja wa bima kujua ni aina gani ya bima anahitaji. Mfano mteja anakata bima ndogo tena kwa shinikizo la sheria za usalama barabarani akipata ajari anataka alipwe kitu ambacho hakiwezekani.

Watu wengi wamekua wakimalizana na madereva baada ya kusababishiwa ajari au majanga, kitu ambacho kinapelekea kupoteza kwa haki zake za msingi. Pia watembea kwa miguu wanapaswa kutembea au kupita katika eneo husika wakiwa barabarani.

Pia abiria wapaswa kufunga mkanda wakati wote wakiwa safarini.

Kumbuka: Bima hii sio kwaajil ya mmiliki wa chombo Cha moto Bali ni kwaajil ya watu wengine na Mali zao ambao unaweza kuziharibu au kuwaumiza kutokana na udereva wako.
 
Elimu nzuri sana ila tatizo ni kuwa asilimia kubwa ya Watanzania hawana Elimu hii na ndo maana watu wakisababisha ajali hukimbia.

Asilimia 99 ya Pikipiki zote nchini hazina BIMA
Hivyo Serikali iangalie uwezekano wa mnunuzi wa pikipiki kulipia bima ya miaka 3 kwenye pikipiki husika pale tu anapoinunua
 
Bima ni Nini

Bima ni mfumo wa ulinzi au fidia ambao unawezesha mtu au shirika kulinda mali zao au kujilinda dhidi ya hatari au hasara ambazo zinaweza kutokea. Kuna aina mbalimbali za bima mfano bima ya Afya, bima ya vyombo vya moto, bima ya maisha, bima ya moto n.k.

Aina ya bima za vyombo vya moto

  • Bima kubwa ( comprehensive cover).
  • Bima ndogo ( Third party cover).
  • Bima ndogo + moto na wizi ( third party, fire and theft)
Leo hii tutazungumzia sana Bima ndogo (Third party cover). Bima hii ni muhumu sana katika vyombo vya moto kwakua ni lazima ( kisheria).

Aina hii ya bima humlinda mmiliki wa chombo Cha moto endapo atagonga Mali za watu wengine mfano gari, duka, pikipiki n.k. lakini pia itamlipia fidia kwa uharibifu wowote au vifo kwa binadamu au wanyama. Endapo atamsababishia kifo au kilema mtu wa tatu. Dereva Atatakiwa kulipa fidia, hivyo bima hiyo itamsaidia kulipa.

Hivyo basi ikiwa umepata ajali kwa kumgonga mtu, arafu chombo chako kimeharibika basi bima hiyo itamlipa yule uliyemgonga lakini na chombo chako hakitalipwa.

Kulingana na Sheria ya Bima ya Tanzania ya mwaka 2002, sura ya 169, kifungu Cha 04, inamlazimu kila mmiliki wa chombo Cha moto akate bima ndogo ambayo ipo kwaajili ya kumlinda mtu wa tatu. Mtu wa tatu katika bima ni kama vile abiria, watembea kwa miguu, dereva mwingine au mtu yeyote ambae atasababishiwa madhara na mmiliki wa chombo Cha moto.

Haki za abiria na watembea kwa miguu

Faida ya bima ndogo ni kumlinda mtu wa tatu katakana na madhara kama kuharibiwa Mali, ama kusababishiwa ukilema, vifo n.k

Mahakama ina mpa mtembea kwa miguu au abiria haki ya kulipwa endapo atasababishiwa hasara au madhara yoyote na chombo Cha moto, haki hizo ni kulipwa fidia kama ifuatavyo

  • Gharama za matibabu
  • Gharama za kuendesha kesi endapo mtu wa tatu akishinda kesi hiyo
  • Fidia ya vifo au ukilema Cha aina yeyote
  • Uhalibifu wa Mali ( gari, nyumba, duka n.k )
WAJIBU WA ABIRIA /WATEMBEA KWA MGUU

Wajibu wa mtu wa tatu (third party person) katika kuhakikisha analipwa fidia baada ya ajali nafasi yake . Kwa ujumla, mtu wa tatu anaweza kuchukua hatua zifuatazo:

Ripoti ajali: Kwanza kabisa, wanapaswa kuhakikisha kwamba wanaandika taarifa kamili ya ajali na kutoa ripoti kwa polisi au mamlaka husika mara moja. Ripoti hii itakuwa na maelezo muhimu kuhusu ajali, ikiwa ni pamoja na sehemu na tarehe ya ajali, maelezo ya watu waliohusika, na maelezo ya uharibifu uliotokea.

Kutoa ushahidi: Mtu wa tatu anaweza kuwa shahidi muhimu katika kuthibitisha jinsi ajali ilivyotokea na ni nani aliyesababisha ajali. Wanaweza kutoa taarifa na ushahidi wao kwa polisi, mamlaka husika, au kampuni ya bima ili kusaidia katika uchunguzi na madai.

Kutoa taarifa na ushahidi: Mtu wa tatu anaweza pia kuwasilisha taarifa na ushahidi unaohusiana na ajali na madai ya fidia. Wanaweza kuandika taarifa ya ushahidi wao, kutoa maelezo ya tukio, na kutoa ushahidi wa picha au video ikiwa inapatikana. Ushahidi huu unaweza kuwa muhimu katika kujenga hoja za fidia.

Kutoa ushahidi wa gharama: Ikiwa mtu wa tatu ameshuhudia hasara ya mali au uharibifu uliosababishwa na ajali, wanaweza kusaidia kwa kutoa ushahidi wa thamani ya mali iliyoharibiwa au gharama zinazohusiana na ukarabati. Hii inaweza kusaidia katika kuthibitisha madai ya fidia yanayohusiana na uharibifu.

Kushirikiana na mamlaka husika: Mtu wa tatu anaweza kushirikiana na polisi, mamlaka za barabarani, au mamlaka nyingine zinazohusika katika uchunguzi wa ajali. Hii inaweza kusaidia kuhakikisha kuwa haki inatendeka na kwamba pande zote zinazohusika zinatoa ushirikiano wao katika mchakato wa madai.

Mapendekezo kwa mamlaka ya bima (TIRA) na serikali

Serikali na TIRA inawapasa kutoa elimu muhimu kwa wateja wa bima kuhusu faida za bima, utendaji kazi wa bima, mipaka, na vitu vinavyopelekea usilipwe. Elimu kwa wamiliki wa vyombo vya moto kuhusiana na bima itawafanya wanunue vifurushi sahihi na vyenye tija kwao.

Pia elimu hio ijikite kuelimisha kuhusiana na haki za raia na mali zao , kuelimisha kuwa abiria au watembea kwa miguu wanapopata ajari kwa kugongwa na vyombo vya moto yawapasa kufungua kesi za madai na sio kumalizana kienyeji. Bila kusahau elimu kwa madereva watakao gonga raia au mali ya mtu , asikimbilie kutoa pesa za kupooza au kukimbia maana jukumu la malipo sio lake hivyo yampasa kuangalia usalama wake tu na kusubili hatua za kisheria zitazo mfanya asimkoseshe fidia muhanga wa ajari hio

Ushauri

Kumekuwa na mijadala mingi kususiana na Bima , watu wengi wana mitazamo dhanifu kuhusu bima , wengi wakisema kuwa bima ni utapeli lakini ukweli ni kwamba ukosefu wa elimu ya bima umeenea sana kwa jamii ya Tanzania na kuitizama bima kama ni wizi au utapeli kitu ambacho sicho.

Watu hununua bima kwa mazoea bila kujua ni aina gani ya bima inatoa fidia zipi na nani hulipwa fidia hizo . Kiukweli bima hufuata misingi ya sheria kumtaka mteja wa bima kujua ni Aina gani ya bima anahitaji. Mfano mteja anakata bima ndogo tena kwa shinikizo la sheria za usalama barabarani akipata ajari anataka alipwe kitu ambacho hakiwezekani.

Watu wengi wamekua wakimalizana na madereva baada ya kusababishiwa ajari au majanga, kitu ambacho kinapelekea kupoteza kwa haki zake za msingi. Pia watembea kwa miguu wanapaswa kutembea au kupita katika eneo husika wakiwa barabarani.

Pia abiria wapaswa kufunga mkanda wakati wote wakiwa safarini.

Kumbuka: Bima hii sio kwaajil ya mmiliki wa chombo Cha moto Bali ni kwaajil ya watu wengine na Mali zao ambao unaweza kuziharibu au kuwaumiza kutokana na udereva wako.
Uelimishaji huu ni mzuri na unafaa hivyo ingeandaliwa njia nyingine ya jumbe kama hizi ziwafikie watu mbalimbali na ambao hawana nafasi ya kutembelea page kama hizi na kusoma
 
Back
Top Bottom