Mwanamaji
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 2,896
- 4,495
Utangulizi:
Kijiografia bahari zinachukua takriban 71% ya eneo lote la uso wa Dunia yetu na kwa nadharia za kisayansi inaaminika kwamba maisha ya viumbe yalianzia baharini. Hivyo basi, kwa vyoyote vile iwavyo, bahari imekua sehemu muhimu kabisa ya maisha ya kila siku ya binadamu. Binadamu anafanya shughuli zake mbalimbali katika mazingira ya maji au bahari, nyingine ni za kiuchumi na nyingine si za kiuchumi.
Uchumi wa bluu:
Huu ni mkusanyiko wa shughuli zote za kiuchumi ambazo zinafanyika katika mazingira ya maji hasa bahari. Shughuli hizo ni pamoja na uvuvi (fishing), ukuzaji viumbe maji (aquaculture), utalii (tourism), usafiri na usafirishaji (transportation and shipping), uvunaji wa mafuta na gesi (oil and gas exploration), uzalishaji nishati (energy generation), uchimbaji madini (minerals extraction) na mengineyo mengi. Ukienda mbele zaidi, uchumi wa bluu unajumuisha pia shughuli za utunzaji na uhifadhi wa mazingira ya bahari (conservation and management activities).
Ili kuleta uwiano mzuri kati ya matumizi ya rasilimali za baharini na kuzitunza au kuzihifadhi ndipo inakuja dhana nzima ya matumizi endelevu ya rasilimali bahari (Sustainable utilization of marine resources).
Kwa sababu bahari imeenea kwenye eneo kubwa sana katika uso wa dunia, jitihada za kuhakikisha kunakua na uhifadhi na matumizi endelevu ya bahari zinapaswa kuwa ni za pamoja baina ya mataifa mbalimbali (collaborative approach of marine resources management).
Jitihada hizo hufanyika kwa namna mbalimbali kama vile mikutano na makongamano (summits, conferences and conventions) ili kujadiliana, kuweka mikakati ya pamoja na wakati mwingine kusaini mikataba na kupitisha sheria mbalimbali. Lakini pia hatua nyingine za kiutekelezaji zinajumuisha kufanya miradi ya uhifadhi pamoja, kupeana misaada ya rasilimali kadha wa kadha, kubadilishana taarifa za tafiti na mambo mengine “chungu nzima”.
Mkutano wa Kimataifa wa Rasilimali za Bahari: The One Planet Summit for The Oceans
Ni mkutano wa kimataifa unaojumuisha mataifa ya Ulaya na mataifa mengine kwa lengo la kuchukua hatua dhidi athari hasi zinazoyakabili mazingira ya bahari. Mwaka huu 2022, mkutano huu unafanyika mjini Brest nchini Ufaransa chini ya uenyeji wa Rais wa nchi hiyo bwana Emmanuel Macron. Pamoja na wahudhuriaji wengine mkutano huu unajumuisha wakuu wa nchi, wakuu wa taasisi mbalimbali za kimataifa pamoja na wadau wengine wanaoguswa moja kwa moja na masuala ya mazingira ya bahari.
Lengo kuu la mkutano huu ni kutafuta suluhu ya pamoja ya kukabiliana na changamoto “za kesho” ya bahari ambazo kwa uchache ni kama vile uchafuzi (pollution), uharibifu wa maeneo muhimu ya bahari (degradation of keystone habitats), madhara ya mabadiliko ya tabia ya nchi (marine induced climate changes) na mengineyo mengi. Masuala mengine yanayoangaziwa macho ni pamoja na kuweka mikakati ya pamoja ya kuendeleza uvuvi endelevu bila kusahau hatua nyingine za uhifadhi na utunzaji wa bayoanuai (biodiversity).
Katika mkutano huo, Tanzania imewakilishwa na Rais Mh. Samia Suluhu Hassan.