Ziara ya Kabudi ya kuomba msamaha ni nzuri kwa taifa

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,601
8,741
Waziri Kabudi amekuja US kukutana na wawakilishi wa serikali ya Trump na World Bank.

Kwenye World bank alikuja kwa unyeyekevu na kuwahakikishia bank kwamba Tanzania itaweka shule maalumu za kulinda watoto waliopata mimba na hii wamehakikisha kapiga sahihi kabisa.

Pili amepeleka ujembe kutoka kwa Magufuli kwenda kwa Trump kuhusu uchaguzi huru, haki za binadamu na mambo mengine ambayo yamefanya Tanzania kwa mara ya kwanza kuingizwa kwenye list mbaya wa wananchi wake kusafiri kwenda US.

Kiukweli kabisa hii ziara ni ziara ya kuomba msamaha na kujaribu kurudisha uhusiano ambao Kikwete na Mkapa waliutengeneza.

Zile sera za kibabe na kuita watu mabeberu tunashukuru Kabudi ameona mwenyewe hazitupeleki mbele. Lakini amejua ukweli kwamba Dunia ni ndogo tuangalie Corana virus wote tupo kama binadamu ikipatikana kinga ambayo kampuni ya US inatengeneza ni ya Dunia nzima sio ya mabeberu pekee.

Hongereni kwa kujali taifa na kuanza kukutana na upinzani naona Magu kaona ukweli.
 
Yes, tunataka uchaguzi huru na haki sio yale mauzauza ya uchaguzi wa S/M na mahakama zisiingiliwe na pia polisi wawe professional, waache tabia za ki-interahamwe.
 
Tuliwaambia China jamani bado kuna mengi hawezi na kujikweza kwao kote . Chanjo ya Corona sio pesa pekee ni technologia inahitajika na itatoka wapi hukohuko kwa mabeberu. Hao China huku nyuma wanapiga magoti na kuomba msaada Bunge la US limepitisha $8.5B lakini $3B ya chanjo na itapatikana hawabahatishi.
 
Ni furaha kuu jamani kuona kuwa tumejitambua kuwa sisi si kisiwa. B/up sana Kabudi kwa kuuweka kando ukaidi ukaona vyema kushuka tu ili mambo yende vizuri. Tulitaka kutengeneza Zimbabwe ya pili lakini heri wenzetu walikuwa na kaubavu kidogo kwenye uchumi. Sisi sijui tungeendesha nchi siku ngapi.

Tufuate amri zao bila shuruti. Huu si wakati wa kusema; Misaada ya masharti hatuitaki. Sii leo tena.
 
Naunga mkono hoja.
P
Kweli ni huu...
IMG-20200307-WA0096.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pumba, hakuna lolote hapo ni ngonjera tu. Wewe unafahamu uhusiano aliotengeneza Mkapa na Kikwete? Kweli mwenye macho haambiwi tazama.
 
eti tunajitutumua kushindana na nchi wahisani, wafadhili wa bajeti zetu...

hawa wanataka kutupeleka chaka kabisa
 
Back
Top Bottom