Ziara ya Rais Samia Russia: Tanzania itapata nini katikati ya mashinikizo ya EU, Marekani?

Elias Msuya

Platinum Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
217
Reaction score
860
884728b6-1183-469f-87df-9cf36008a85e.jpg

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya ziara nchini Russia inayotajwa kuwa na umuhimu wa kihistoria kwa Tanzania na inafungua hatua mpya za ushirikiano wenye manufaa kwa wananchi wa pande zote mbili.

Samia anakuwa rais wa pili wa Tanzania kutembelea nchi hiyo, tangu Hayati Mwalimu Julius Nyerere kufanya ziara rasmi nchini humo.

Ziara ya Urusi imekuja katika kipindi ambacho Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa katika uhusiano wake na baadhi ya mataifa ya Magharibi.

Baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025 uliogubikwa na tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu, pamoja na shinikizo kutoka Marekani na Umoja wa Ulaya, safari hiyo ya Moscow imeibua mjadala mpana kuhusu mwelekeo wa diplomasia ya Tanzania na manufaa ambayo taifa linaweza kuyapata kutokana na kuimarisha ushirikiano wake na Russia.
50949e83-3981-4500-8a86-004e3de5014c.jpg

Kwa mtazamo wa haraka, ziara hiyo inaweza kuonekana kama sehemu ya ratiba ya kawaida ya kidiplomasia kati ya mataifa mawili yenye historia ndefu ya ushirikiano.

Hata hivyo, ukiangalia mazingira ya sasa ya kisiasa na kimataifa, ni wazi kwamba ziara hiyo ina uzito mkubwa zaidi kuliko mikutano ya kawaida ya viongozi wa nchi mbili.

Katika mazungumzo yake na Rais Vladimir Putin, Rais Samia ameeleza maeneo mengi ya ushirikiano yanayoweza kuwanufaisha Watanzania.

Miongoni mwa maeneo hayo ni kilimo, nishati, afya, elimu, teknolojia za kidijitali, akili bandia, sayansi ya anga, madini, usafiri wa anga na maendeleo ya bandari. Haya ni maeneo muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa Tanzania na yanahitaji uwekezaji mkubwa wa teknolojia, mtaji na utaalamu.

Katika sekta ya kilimo, Tanzania imekuwa ikitafuta kwa muda mrefu njia za kuongeza uzalishaji, kuimarisha upatikanaji wa pembejeo na kuongeza thamani ya mazao.

Russia ni moja ya wazalishaji wakubwa wa mbolea duniani. Ushirikiano katika eneo hili unaweza kusaidia kupunguza gharama za uzalishaji kwa wakulima na kuongeza ushindani wa mazao ya Tanzania katika soko la kimataifa.

Kadhalika, katika sekta ya nishati, Tanzania inahitaji uwekezaji mkubwa ili kukidhi mahitaji ya viwanda na uchumi unaokua kwa kasi. Ikiwa mazungumzo ya Moscow yatazaa miradi ya nishati au uhamishaji wa teknolojia, basi taifa linaweza kunufaika kwa muda mrefu zaidi ya matamko ya kidiplomasia.

Lakini pamoja na masuala ya kiuchumi, kuna upande mwingine wa ziara hii ambao hauwezi kupuuzwa.

Huu ni upande wa diplomasia na taswira ya Tanzania katika jukwaa la kimataifa.

Tanzania inajisafisha kimataifa

Mhadhiri wa Chuo cha Diplomasia cha Dk. Salim Ahmed Salim, Godwin Gonde, anaona ziara hiyo kama sehemu ya juhudi za Tanzania kujijenga upya kimataifa baada ya uchaguzi wa mwaka 2025.

Kwa mtazamo wake, Russia ni mshirika ambaye hana masharti makubwa ya kisiasa kuhusu masuala ya demokrasia na haki za binadamu kama ilivyo kwa nchi nyingi za Magharibi.

“Kwangu mimi naona ziara hii ni mkakati wa Tanzania kujisafisha kimataifa maana baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025 Tanzania iliyokuwa ikisifika kwa Amani nayo ilitikisika.

“Russia ni nchi ambayo haichagui rafiki kwa hiyo hii fursa ya kuimarisha uhusiano na kujijengea jina upya kwa Tanzania (rebranding)."

07f5b6d4-55c3-40ba-b631-ef3baed5e799.jpg

Kwa mujibu wa Gonde, mataifa ya Magharibi yana masharti magumu katika masuala ya demokrasia, lakini Russia katika sera zake inaona hayo ni masuala ya ndani ambayo haiwezi kuingilia.

Hoja hii ina mantiki fulani. Katika miaka ya hivi karibuni, Russia imeimarisha ushawishi wake katika Afrika kwa kujenga ushirikiano unaojikita zaidi kwenye masuala ya kiuchumi, usalama na biashara kuliko ajenda za kisiasa za ndani za nchi washirika wake.

Hali hiyo imeifanya Moscow kuwa kivutio kwa baadhi ya mataifa yanayokabiliwa na ukosoaji kutoka kwa nchi za Magharibi yakiwamo ya Burkina faso, Mali na Niger yaliyokumbwa na mapinduzi ya kijeshi.

Hata hivyo, Tanzania inapaswa kuwa makini isije ikatoa taswira kwamba inaachana na washirika wake wa jadi wa Ulaya na Marekani.

Uchumi wa Tanzania bado unategemea kwa kiasi kikubwa biashara, uwekezaji, misaada ya maendeleo na ushirikiano wa kiufundi kutoka nchi za Magharibi.

Umoja wa Ulaya na Marekani bado ni miongoni mwa washirika wakubwa wa maendeleo wa Tanzania.

Kwa sababu hiyo, ziara ya Moscow haipaswi kutafsiriwa kama mabadiliko ya ghafla ya sera ya mambo ya nje ya Tanzania.

Badala yake, inaweza kuonekana kama mwendelezo wa sera ya muda mrefu ya kutofungamana na upande wowote ambayo iliasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Mchambuzi wa diplomasia Amos Msanjila anasisitiza hoja hiyo kwa kueleza kwamba Tanzania imekuwa ikifuata sera ya usawa katika mahusiano yake ya kimataifa tangu kupata uhuru.
60b4943e-f83f-4bb0-b483-64ff3b2e12c5.jpg

Katika kipindi cha Vita Baridi, Tanzania iliweza kushirikiana na mataifa ya Mashariki kama Urusi na China huku wakati huo huo ikidumisha uhusiano na baadhi ya mataifa ya Magharibi.

Sera hiyo ndiyo iliiwezesha Tanzania kupata msaada kutoka pande mbalimbali bila kujifungamanisha na kambi moja pekee. Katika dunia ya sasa yenye ushindani mkubwa wa kiuchumi na kisiasa, sera hiyo inaendelea kuwa na umuhimu mkubwa.

Kwa upande mwingine, Tanzania inaweza kutumia ziara hii kama fursa ya kuonyesha kwamba bado ina uwezo wa kushirikiana na mataifa mbalimbali duniani licha ya changamoto za kisiasa zinazojitokeza. Hiyo ni sehemu muhimu ya uhuru wa kidiplomasia ambao taifa limeujenga kwa miongo mingi.

“Ni kweli kwamba ziara hii inakuja wakati Tanzania inakabiliwa na tishio la uhusiano wake na Marekani na wakati huo huo, tumeona Kati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Umoja wa Ulaya likipiga kura ya kutaka nchi hiyo ifutiwe misaada, lakini haimaanishi kwamba Tanzania ndiyo itaacha juhudi za kurejesha uhusiano huo.

“Ni suala la Tanzania kuendelea na majadiliano na pande zenye misuguano, kama tumekwenda hatua 10 na wao hatua 10, basi tunarejea hatua 8 au 5, basi tunasonga mbele, kwa hiyo sio kwamba uhusiano umekwisha kabisa,” amesema.

Kwa ujumla, ziara ya Rais Samia nchini Urusi inaweza kuleta manufaa makubwa ikiwa itazalisha ushirikiano wa kiuchumi, kiteknolojia na kielimu unaotekelezeka. Lakini thamani yake ya kweli itapimwa si kwa ukubwa wa mapokezi ya Kremlin au idadi ya makubaliano yatakayosainiwa, bali kwa matokeo yatakayogusa maisha ya Watanzania.

Katika kipindi ambacho Tanzania inakabiliwa na changamoto za ndani na shinikizo kutoka baadhi ya washirika wa kimataifa, diplomasia ya usawa na ushirikiano wa pande nyingi inaweza kuwa njia sahihi ya kulinda maslahi ya taifa.

Hapo ndipo kipimo halisi cha mafanikio ya ziara hii kitakapopatikana.
 
"Tusiseme hatuna matatizo kwa kuyaficha matatizo yetu wenyewe. Ujasiri wa taifa hauko katika kuficha kasoro zake, bali katika kuzikubali na kuzitatua."

Mwalimu J K Nyerere.
 
Tena kaenda na mtoto wake Abdul.
Rejea (I am the state) mtanifanya nn?
Siku yaja
 
View attachment 3601047
Rais Samia Suluhu Hassan amefanya ziara nchini Russia inayotajwa kuwa na umuhimu wa kihistoria kwa Tanzania na inafungua hatua mpya za ushirikiano wenye manufaa kwa wananchi wa pande zote mbili.

Samia anakuwa rais wa pili wa Tanzania kutembelea nchi hiyo, tangu Hayati Mwalimu Julius Nyerere kufanya ziara rasmi nchini humo.

Ziara ya Urusi imekuja katika kipindi ambacho Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa katika uhusiano wake na baadhi ya mataifa ya Magharibi.

Baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025 uliogubikwa na tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu, pamoja na shinikizo kutoka Marekani na Umoja wa Ulaya, safari hiyo ya Moscow imeibua mjadala mpana kuhusu mwelekeo wa diplomasia ya Tanzania na manufaa ambayo taifa linaweza kuyapata kutokana na kuimarisha ushirikiano wake na Russia.
View attachment 3601048

Kwa mtazamo wa haraka, ziara hiyo inaweza kuonekana kama sehemu ya ratiba ya kawaida ya kidiplomasia kati ya mataifa mawili yenye historia ndefu ya ushirikiano.

Hata hivyo, ukiangalia mazingira ya sasa ya kisiasa na kimataifa, ni wazi kwamba ziara hiyo ina uzito mkubwa zaidi kuliko mikutano ya kawaida ya viongozi wa nchi mbili.

Katika mazungumzo yake na Rais Vladimir Putin, Rais Samia ameeleza maeneo mengi ya ushirikiano yanayoweza kuwanufaisha Watanzania.

Miongoni mwa maeneo hayo ni kilimo, nishati, afya, elimu, teknolojia za kidijitali, akili bandia, sayansi ya anga, madini, usafiri wa anga na maendeleo ya bandari. Haya ni maeneo muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa Tanzania na yanahitaji uwekezaji mkubwa wa teknolojia, mtaji na utaalamu.

Katika sekta ya kilimo, Tanzania imekuwa ikitafuta kwa muda mrefu njia za kuongeza uzalishaji, kuimarisha upatikanaji wa pembejeo na kuongeza thamani ya mazao.

Russia ni moja ya wazalishaji wakubwa wa mbolea duniani. Ushirikiano katika eneo hili unaweza kusaidia kupunguza gharama za uzalishaji kwa wakulima na kuongeza ushindani wa mazao ya Tanzania katika soko la kimataifa.

Kadhalika, katika sekta ya nishati, Tanzania inahitaji uwekezaji mkubwa ili kukidhi mahitaji ya viwanda na uchumi unaokua kwa kasi. Ikiwa mazungumzo ya Moscow yatazaa miradi ya nishati au uhamishaji wa teknolojia, basi taifa linaweza kunufaika kwa muda mrefu zaidi ya matamko ya kidiplomasia.

Lakini pamoja na masuala ya kiuchumi, kuna upande mwingine wa ziara hii ambao hauwezi kupuuzwa.

Huu ni upande wa diplomasia na taswira ya Tanzania katika jukwaa la kimataifa.

Tanzania inajisafisha kimataifa

Mhadhiri wa Chuo cha Diplomasia cha Dk. Salim Ahmed Salim, Godwin Gonde, anaona ziara hiyo kama sehemu ya juhudi za Tanzania kujijenga upya kimataifa baada ya uchaguzi wa mwaka 2025.

Kwa mtazamo wake, Russia ni mshirika ambaye hana masharti makubwa ya kisiasa kuhusu masuala ya demokrasia na haki za binadamu kama ilivyo kwa nchi nyingi za Magharibi.

“Kwangu mimi naona ziara hii ni mkakati wa Tanzania kujisafisha kimataifa maana baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025 Tanzania iliyokuwa ikisifika kwa Amani nayo ilitikisika.

“Russia ni nchi ambayo haichagui rafiki kwa hiyo hii fursa ya kuimarisha uhusiano na kujijengea jina upya kwa Tanzania (rebranding)."

View attachment 3601049

Kwa mujibu wa Gonde, mataifa ya Magharibi yana masharti magumu katika masuala ya demokrasia, lakini Russia katika sera zake inaona hayo ni masuala ya ndani ambayo haiwezi kuingilia.

Hoja hii ina mantiki fulani. Katika miaka ya hivi karibuni, Russia imeimarisha ushawishi wake katika Afrika kwa kujenga ushirikiano unaojikita zaidi kwenye masuala ya kiuchumi, usalama na biashara kuliko ajenda za kisiasa za ndani za nchi washirika wake.

Hali hiyo imeifanya Moscow kuwa kivutio kwa baadhi ya mataifa yanayokabiliwa na ukosoaji kutoka kwa nchi za Magharibi yakiwamo ya Burkina faso, Mali na Niger yaliyokumbwa na mapinduzi ya kijeshi.

Hata hivyo, Tanzania inapaswa kuwa makini isije ikatoa taswira kwamba inaachana na washirika wake wa jadi wa Ulaya na Marekani.

Uchumi wa Tanzania bado unategemea kwa kiasi kikubwa biashara, uwekezaji, misaada ya maendeleo na ushirikiano wa kiufundi kutoka nchi za Magharibi.

Umoja wa Ulaya na Marekani bado ni miongoni mwa washirika wakubwa wa maendeleo wa Tanzania.

Kwa sababu hiyo, ziara ya Moscow haipaswi kutafsiriwa kama mabadiliko ya ghafla ya sera ya mambo ya nje ya Tanzania.

Badala yake, inaweza kuonekana kama mwendelezo wa sera ya muda mrefu ya kutofungamana na upande wowote ambayo iliasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Mchambuzi wa diplomasia Amos Msanjila anasisitiza hoja hiyo kwa kueleza kwamba Tanzania imekuwa ikifuata sera ya usawa katika mahusiano yake ya kimataifa tangu kupata uhuru.
View attachment 3601050
Katika kipindi cha Vita Baridi, Tanzania iliweza kushirikiana na mataifa ya Mashariki kama Urusi na China huku wakati huo huo ikidumisha uhusiano na baadhi ya mataifa ya Magharibi.

Sera hiyo ndiyo iliiwezesha Tanzania kupata msaada kutoka pande mbalimbali bila kujifungamanisha na kambi moja pekee. Katika dunia ya sasa yenye ushindani mkubwa wa kiuchumi na kisiasa, sera hiyo inaendelea kuwa na umuhimu mkubwa.

Kwa upande mwingine, Tanzania inaweza kutumia ziara hii kama fursa ya kuonyesha kwamba bado ina uwezo wa kushirikiana na mataifa mbalimbali duniani licha ya changamoto za kisiasa zinazojitokeza. Hiyo ni sehemu muhimu ya uhuru wa kidiplomasia ambao taifa limeujenga kwa miongo mingi.

“Ni kweli kwamba ziara hii inakuja wakati Tanzania inakabiliwa na tishio la uhusiano wake na Marekani na wakati huo huo, tumeona Kati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Umoja wa Ulaya likipiga kura ya kutaka nchi hiyo ifutiwe misaada, lakini haimaanishi kwamba Tanzania ndiyo itaacha juhudi za kurejesha uhusiano huo.

“Ni suala la Tanzania kuendelea na majadiliano na pande zenye misuguano, kama tumekwenda hatua 10 na wao hatua 10, basi tunarejea hatua 8 au 5, basi tunasonga mbele, kwa hiyo sio kwamba uhusiano umekwisha kabisa,” amesema.

Kwa ujumla, ziara ya Rais Samia nchini Urusi inaweza kuleta manufaa makubwa ikiwa itazalisha ushirikiano wa kiuchumi, kiteknolojia na kielimu unaotekelezeka. Lakini thamani yake ya kweli itapimwa si kwa ukubwa wa mapokezi ya Kremlin au idadi ya makubaliano yatakayosainiwa, bali kwa matokeo yatakayogusa maisha ya Watanzania.

Katika kipindi ambacho Tanzania inakabiliwa na changamoto za ndani na shinikizo kutoka baadhi ya washirika wa kimataifa, diplomasia ya usawa na ushirikiano wa pande nyingi inaweza kuwa njia sahihi ya kulinda maslahi ya taifa.

Hapo ndipo kipimo halisi cha mafanikio ya ziara hii kitakapopatikana.
Screenshot_20260604-133242~2.png
 
Muhimu hapa kujua ni kuwa; ule ni mwaliko rasmi kutoka kwa Rais wa Urus Vladimir Putin
Hivi unaweza kualikwa na Nchi yenye nguvu kama, Urusi, China, Ujerumani nk ukatae kwenda?

Lakini pia kwa miaka ya nyuma kidogo Urusi ilikuwa inafanya vizuri sana kwa kutusomeshea (Scholarship) wataalam wengi wa sayansi (Engineers and Doctors); natamani huo moyo urudi tena ili iwasaidie vijana wetu wawe wabobevu na kuweza kukuza uchumi wetu....
 
Back
Top Bottom