Ze Utamu blogger under arrest?

Ze Utamu blogger under arrest?

Status
Not open for further replies.
Hii case ni ngumu sana, unatakiwa uwe na mwanasheria wa uhakika. Kwa wale wote wanaojijua ni victim wa hili sakata tuwasiliane as soon as possible kuweka mambo sawa mapema, haraka na upesi.

Haya bwana ngoja nijipange nitakutafuta tu nikitajwa kama ndo hivyo basi tutegemee serikali kuvunjika hivi punde.
 
hahahaha sasa na wale waliokuwa wamepigwa za utupu tutawafanyaje nao? Maana najua ni kosa la kisheria kupiga picha za utupu sasa itabidi nao tuwasimamishe kizimbani.

Unayo hiyo sheria utupe mkuu, au ni maneno yako unatunga?
 



Polisi wa Tanzania kwa kushirikiana na Polisi wa Kimataifa (Interpol),wamefanikiwa kumshika Raia mmoja wa Uingereza ambaye ana asili ya Tanzania Ndg Malecela Peter Lusinde (pichani) mwenye umri wa miaka 39 na kutuhumiwa kwa kuundesha mtandao wa Ze Utamu. Ndugu Malecela ambaye anajulikana pia kwa jina la "Male" ni Mtaalamu wa kompyuta na ana uwezo wa kuzungumza na kuandika Kiingereza,kiswahili na kichina ana makazi katika mji wa Essex nchini Uingereza.

Wataalamu wa Idara ya upelelezi kutoka Tanzania wakishirikiana na wenzao wa Uingereza wamefanikiwa kuonana na Ndg Male na kupata ushahidi wa kutosha kwamba ndiye alikuwa mmiliki wa Mtandao huo.Idara ya Upelelezi na polisi wa Uingereza wameutaarifu Ubalozi wa Tanzania mjini London kuhusu suala hilo.Maofisa Ubalozi Mr.Clement Kiondo na Amos Msanjila wamefahamishwa jambo hilo.Malecela ni Mtoto wa Mzee Job Lusinde ambaye amewahi kufanya kazi kwenye nyadhifa mbalimbali za utumishi wa serikali Nchini Tanzania.

Habari zilizothibitishwa zinadai kuwa Ndg Malecela amerudishwa Tanzania kwenda kujibu tuhuma mbalimbali za kuendesha mtandao uliokuwa unadhalilisha watu,kuna malalamiko 6850 yaliyoandikishwa kulaumu udhalilishwaji wa watu uliofanywa na mtandao huo,Mtandao huo ulisimamishwa mwanzoni mwa mwezi wa pili kwa maombi ya serikali ya Tanzania baada ya kutoa picha ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete,ufuatiliaji uliofanywa baada ya picha hiyo ndio umepelekea kukamatwa kwa Ndg Malecela.

Haijaeleweka wazi Ndg Malecela atashitakiwa kwa sheria gani? Lakini ni wazi kwamba atashitakiwa Nchini Tanzania. Licha ya Ndg. Malecela Polisi wa Upelelezi wamezungumza na Watanzania wengine wawili katika miji ya Wichita na San Diego Nchini Marekani, ambao pia wanahusishwa na Mtandao huo wa Ze Utamu.
 

Attachments

Unayo hiyo sheria utupe mkuu, au ni maneno yako unatunga?

Mkuu kuna binti mmoja Morogoro hapo alipiga picha za utupu alifungwa jela mwaka mmoja tafuta DATA za kimahakama Moro utaona..
 
Hahaha watanzania kweli waoga! Eti mtu aliyekomment au kuvisit site atashtakiwa!! lol!

Kwanza kabisa sijaona ushahidi wowote kuwa huyu jamaa kamatwa kweli, watu mnapost habari ile ile ambayo haina kichwa wala miguu!! Halafu habari yenyewe imeandikwa kitoto toto eti wameinterogate host!, pia Israeli imeingiaje? Yaani waingereza wakubali waisraeli waingilie mambo yao?? Mnachekesha kweli.
 
kwi kwi kwi kwi,Fidel kumbe na wewe ulikuwa mdau waku-comment sio? nakushauri ubadilishe uraia mara maja kabla hawajakufikia.https://www.jamiiforums.com/images/icons/icon10.gif

hahahaha hapa ile kitu inagonga nilipo kaa na kurudi tena we acha bana na wewe unavyo tisha lakini all in all mbona Bush wamemfanyia sana photoshop saana tu lakini USA wapo kimyaaaaa TZ ndo tuanze kutishiana amani wapi na wapi mkuu.
 
Hahaha,

Ni kweli, mimi wewe na wengine sote tuna ukaribu na mmiliki wa Ze Utamu. Ni mwanachama wa JF na unaweza kufuatilia kuangalia wakati anai-promote tovuti yake hapa:

https://www.jamiiforums.com/313709-post226.html

na hapa:

https://www.jamiiforums.com/314650-post230.html

katika hii topic: https://www.jamiiforums.com/habari-...ze-utamu-blog-ni-aibu-kubwa-mno-kwa-taifahtml

Kwakuwa umeniuliza nikakujibu huenda nami ukanijibu nikikuuliza:

Hivi nani kakuambia hayo mkuu josm?
Mkuu nadhani jibu lipo kwenye post yangu ya mwanzo.nimesema kuna habari nyingi kwenye mitandao zinadai kuwa wewe upo karibu sana na Zeutamu.ni hivyo tu mkuu na kama ujaridhika na majibu yangu nitakupa link ujionee mwenye usije sema na kuchafua buree mkuu wangu Heshima mbele.
 
Nimesoma ktk Mwananchi leo kwamba Manumba hana taarifa za kukamatwa kwa Ze utamu boss. na hata balozi wa tz uingereza hana taarifa.

Walio karibu na Membe watupe nyeti basi tujue kama amekamatwa au bado tupo weekend.
 
Kuna mtandao mkubwa sana utakaoshtakiwa, watoa comments, wapiga picha, pamoja na waliokuwa wakii-visit ile blog najua kuna wana JF wengi tu watakao simamishwa kizimbani.

Mmoja wao ukiwa ni wewe mwenyewe mkuu.
 
Yaani huweziamini kama huyo kijana (sijui mbaba maana 39 amekwenda age) mzuri hivyo ameoza kichwani mwake!! Sitaki hata kukumbuka uchafu alikuwa akiuanika kule kwake!! Duh si mzima huyu hivi hana familia? Hajaoa?

Huko UK anafanya nini hasa kimaisha au ndo wale waliokwenda kutalii?

Mwanajamii One, inaelekea umemzimia sana huyu kijana.

Ila ndhani huyu ni mtu ambaye chama chawala kinamtumia katika mbinu zake za kutafuta kula. Always goals are set and missions are done. Check out his profile.

Just click below
ze utamu
 
Safi sana, nilisema bwana as long as u re using PC u re wide open 2 de world na uko traceable. Sasa ngoja akae ndani kwanza kwa siku kadhaa wakati upelelezi ukiendelea, atutajie na wenzake waliokua wakimpelekea picha then ndio court itafanya kazi yake. Alipitiliza kituo bwana, huwezi ukamkashifu kivile Our Head of State n get away with it. Iwe fundisho kwa wale wote tunaodhani when we are behind our pc nobody is watching............................Bado Global Publishers..... na Sani...
 
Hajakamatwa mtu jamani!! Acheni kushabikia upumbavu!!!!!
 
Mkuu nadhani jibu lipo kwenye post yangu ya mwanzo.nimesema kuna habari nyingi kwenye mitandao zinadai kuwa wewe upo karibu sana na Zeutamu.ni hivyo tu mkuu na kama ujaridhika na majibu yangu nitakupa link ujionee mwenye usije sema na kuchafua buree mkuu wangu Heshima mbele.

Mkuu JOSM ... sorry but i smell something fishy about you
 
kweli anastahili adhabu tena kubwa sana ikiwa ni pamoja na kumuomba mheshimiwa JK samahani na watanzania kwa ujumla ikiwezakana ikiwa ni pamoja na kifungo atobolewe na macho kabisa.hata kama ni mtoto wa kigogo tena hao ndio wanaharibu baadhi ya viongozi waadilifu ktk nchi kwa chuki za wazazi wao na kiongozi husika.nikweli hata mimi nimezisoma ktk chazo cha habari fulani ingawa wahusika wakutupa uhakika wa hapa nchini (manumba) na wa mahusiano ya nchi za nje nchini uk. baadhi ya watuhumiwa wakiwa marekani

zeutamu kaharibu viongozi waadilifu?????
kwa hiyo hao viongozi sio waadilifu tena.....
mfano tafadhali
 
Jeshi la polisi wanakataa kupokea taarifa.
Balozi wa TZ UK anakataa kupata taarifa kutiwa nguvuni.
Huyo aliye leta habari hizi za upotoshaji itabidi ashughulikiwe nae kwa kuchafua watu wasio kuwa na hatia.
 
haya kuhusu.Kaa kimya
hahhahahhaha sasa wakuuu naona badala ya ze utamu awe roho juuu na agonized imehamia kwenu maaana mnavyoshushuana? mhhhhhh now i too smell smthing fishyy ..... oh no smthing chickenyyyyy
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom