Ze Comedy wabwagwa kortini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ze Comedy wabwagwa kortini

Discussion in 'Entertainment' started by Iteitei Lya Kitee, Aug 20, 2008.

 1. Iteitei Lya Kitee

  Iteitei Lya Kitee JF-Expert Member

  #1
  Aug 20, 2008
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 589
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ze Comedy wabwagwa kortini
  na Vumilia Kondo  MAHAKAMA Kuu Kitengo cha biashara, jana ilitupilia mbali ombi la kundi la sanaa za vichekesho la Ze Comedy kutaka mahakama hiyo itoe idhini ya wao kuendelea na kazi zao kwa kutumia jina hilo wakati kesi ya msingi ikiendelea.

  Katika ombi hilo la awali, wasanii hao wakiongozwa na Isaya Mwakilasa ‘Wakuvanga’, waliiomba mahakama hiyo kutoa zuio kwa kituo cha televisheni cha East Africa, EATV na Chama cha Haki Miliki Tanzania (COSOTA), kutowazuia wao kufanya kazi kwa jina la Ze Comedy.

  Akitoa uamuzi huo jana, Jaji wa mahakama hiyo, Catherine Urio, alisema ili mahakama iweze kutoa zuio, lazima kitu kinachogombewa kiwe katika hali fulani.

  Jaji huyo alisema, katika hoja zote zilizoletwa mahakamani hapo na walalamikaji (wasanii) na EATV (walalamikiwa), hakuna yeyote aliyeonyesha kutumia alama ya Ze Comedy kwa sasa, ingawa wadaiwa wa kwanza, EATV, wameomba kuwa wamiliki wa jina hilo kwa mdaiwa wa pili (COSOTA), lakini bado ombi hilo halijatekelezwa.

  Aliongeza kuwa, walalamikaji (Ze Comedy), walikuwa na kibali cha kulitumia jina hilo la Ze Comedy Production kwa mwaka mmoja, kuanzia Julai mosi mwaka 2007 hadi Juni 30 mwaka huu.

  Alisema, licha ya kibali cha wasanii hao cha kutumia jina la Ze Comedy kwisha, hakuna maombi ya kibali kingine, huku EATV wakiwasilisha maombi COSOTA kutaka kupewa umikili wa jina la Ze Comedy.

  Jaji alisema, kwa mazingira, mahakama inatakiwa kutoa uamuzi kwa uangalifu mkubwa pasipo kuingilia hoja za kesi ya msingi ambayo bado haijaanza kusikilizwa.

  Alisema kutokana na hilo, mahakama imeona si sahihi kisheria kwa sasa kuruhusu kazi na jina la Ze Comedy kuendelea kutumika kabla ya kesi ya msingi haijaamuliwa.

  Kuhusu madai ya wasanii wa Ze Comedy kutaka EATV iwalipe fidia ya usumbufu katika uamuzi wa ombi la awali, mahakama pia imetupa ombi hilo.

  Baada ya kutupwa kwa ombi hilo la awali, kesi ya msingi sasa itaanza kusikilizwa Oktoba 21.

  Wasanii waliokuwa wakiunda kundi la Ze Comedy, baada ya kujiondoa katika umiliki wa EATV na kuhamia TBC1, EATV wakawazuia wasanii hao kutumia jina hilo na majina yao na vionjo walivyokuwa wakitumia awali.
   
 2. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #2
  Aug 20, 2008
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Ze commedy wanajisumbua tu. Sheria iko palepale. Warudi EATV waache kutangatanga. Heri tonge moja mdomoni kuliko mia yajayo. Ebo
   
 3. ChocolateColor

  ChocolateColor Member

  #3
  Aug 20, 2008
  Joined: Jul 18, 2008
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  simbadilishe tu jina kama tatizo ni jina tu kulikoni kuendelea kupoteza muda.
   
 4. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #4
  Aug 20, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  The problem is how to think outside the box.
  Watz tuliwahi kuambiwa tu wavivu wa kufikiri!
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  Sep 3, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Hawa ze comedy wanadanganywa na yule fisadi Manji. Huyu anawatia kiburi kwa pesa yetu aliyotuibia. Na wao bila kujua wanacheza tune yake.
  Maskini Seki! Mmejiharibia kabisa? na hapo ndio kwisha tena, maana watakuja comedians wakali kuliko nyinyi na kupanda kwenye majukwaa ya EATV na hapo ndipo kiama chenu kitaonekana.
   
Loading...