Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 14,047
- 20,411
Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro,imeliamuru baraza la Ardhi wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro,kurejea upya mgogoro wa Ardhi wa familia maarufu ya chifu Marealle kwa kutembelea eneo linalobishaniwa na wanandugu hao na kurekodi upya mipaka na kisha kutoa maamuzi chini ya mwenyekiti mwingine wa baraza hilo
Jaji kuu,Lilian Mongella katika kesi namba 51/2023 ya mrufani Frank Mareale dhidi ya Ackley Mareale ambao wote ni wanandugu, Jaji Mongella alisema mahakama imepitia ushahidi na maamuzi ya Baraza la Nyumba na Makazi la Mji wa Moshi chini ya Uenyekiti wa Reginald Mtei yaliyotolewa mei 5 mwaka huu na kusema kuwa maamuzi hayo yalikuwa na kasoro za kisheria.
"Nimeamua kesi hii ya wanafamilia wa Mareale isikilizwe upya kwa sababu Baraza la Ardhi lilikosea kisheria kwa kushindwa kuonyesha mipaka ya ekari mbili inayogombaniwa"
Katika kesi ya awali iliyofunguliwa na Frank Mareale katika Baraza la Ardhi Nyumba na Makazi katika Mji wa Moshi, alikuwa na madai matatu moja wapo ni ombi la Baraza hilo litamke kuwa eneo la ekari mbili yeye ni mmiliki halali, Pili Baraza litoe amri ya kufukuliwa kwa mwili wa mama yake mdogo marehemu Veronica Mareale aliyeishi katika eneo hilo miaka 80 na kufariki mwaka 2020 na pia alitaka alipwe gharama za kesi.
Akizungumza nje ya Mahakama,Wakili wa Ackley Mareale,Julius Semali alisema kuwa hana pingamizi na uamuzi wa Mahakama kwani ana uhakika kuwa mteja wake ni mmiliki halali wa eneo hilo kwa kuwa mama yake alipata kihalali na alizikwa katika eneo lake.
Naye Wakili wa frank Mareale,Modest Njau aliishukuru Mahakama Kuu kwa uamuzi wake wa kuiagiza Baraza la Ardhi Nyumba na MakaziMoshi kusikiliza upya kesi hiyo na aliamuru Mwenyekiti wa Baraza na wajumbe wake wabadilishwe.
Njau alidai Mahakama Kuu iliona jinsi haki ilivyokuwa ikitaka kuchezewa katika usikilizwaji wa awali nayeye na mteja wake wameridhika na maamuzi hayo
Mei 5 mwaka huu chini ya mwenyekiti wa Baraza hilo la Ardhi Nyumba na Makazi ,Reginald Mtei lilitupilia mbali madai hayo ya Frank Mareale na kusema kuwa Ackley Mareale ni mmiliki halali wa eneo hilo na sio vinginevyo.