tracy
JF-Expert Member
- Sep 22, 2010
- 784
- 268
Jamii nzima inatafunwa na ugonjwa wa upungufu wa maadili ambao binafsi nauona kama ni mbaya kuliko hata hata hili gonjwa la ukimwi. Mtu anapofikia kutoa thamani ya utu wake (penzi) ili tu kupata kazi, ama kupandishwa cheo,ama kufaulu katika mtihani flani huyu si mpiganaji ni mwoga wa maisha na hafai hata kwa mchuzi.
Mpiganaji wa kweli hawezi kukipimbia mapambano regardless yapi amekumbana nayo. Tabia ya kupenda kupita shortcut inatugharimu kama taifa. Watu hawataki kuhangaisha akili zao ili kuweza kujikwamua na maisha ila tunapenda kutimiza ndoto zetu pasina kuamka toka usingizini na kuanza kufanya kazi ili ndoto ziwe reality. Wengi wa binadamu ni waoga hata wa kujaribu ila tunataka tuamke asubuhi na kukuta kila kitu kimefanyika sasa ili iwe hivyo inagharimu maadili na utu wetu.
Tabia hii imekuwa na inaendelea kukua hasa kwa upande wa mabinti na wanawake kwa ujumla. Hatukatai ugumu wa maisha ila hawapaswi kujirahisisha kiivyo mie ninaamini kama bahati ni yako ipo itakuwepo tu. Wataalamu wananyimwa ajira kisa rushwa ya ngono imetolewa na baada ya muda taasisi ama kampuni inalalamika utendaji wake umeshuka huu ni wendawazimu ngoja niishie hapa naona hasira zimeanza kupanda nisije aandika vibaya nikala ban bure.
Acha tu!.kuna watu wamefukuzwa kazi kwa kulinda utu wao(kwangu mimi its worth it),.yani unahangaika na mavitabu afu mtu anakuja kutaka tena mengine!..wengi wamekua sexually abused and all naeza sema ni Mungu tu ndie mtetezi wa binadamu yeyote,.ni kuomba hekima tu.