Zanzibar insurance mjitafakari sana, nimetokea kuwachukia mno!

Sambusa kavu

JF-Expert Member
May 4, 2015
797
1,264
Moja kwa moja niende kwenye hoja kuu

Na bila kupepesa maneno nalitaja kabisa shirika husika...ZANZIBAR INSURANCE ni zaidi ya wasumbusu

Tena nadiriki kabisa kuwaita matapeli wakubwa msiojua thamani ya mteja wenu

Sasa ni nini maana au faida ya kuikatia gari bima ya Comprehensive?

Yaaan nipate ajali gari liumie (nashukuru mungu hakuna majeruhi) then niwapigie halaf mnipe taratibu zoote za kufuata (maripoti ya polisi, michoro, ukaguzi, mpaka na gereji ya kufanya tathmini ya marekebisho mnielekeze nyie, niandae invoince, na mpaka wakaguzi wenu manawaita assesors tena wawili wakalikagua gari na kujiridhisha na kila details.

Halafu mpaka leo eti bado hamjanilipa? jamani eeeh haya yooote nayoyaandika yamenikuta tangu MWAKA JANA MWEZI WA 11 MWANZONI KABISA! Mpaka sasa ni miezi mitatu imekatika!!!

Tena nikawaandikia barua ya kuwaomba niendelee na matengenezo mimi mwenyewe na hii ni baada ya nyie kumaliza ukaguzi wenu mkanikubalia.

Machungu ya thread hii yanakuja hapa mara baada ya gharama nilizotumia kutengeneza gari mwenyewe na kutumia kiasi cha tsh 3.6milioni cash, yaan nimezikopa kwa watu ili nitengeneze gari haraka nikiamini kabisa fedha izo zitarejeshwa na ZANZIBAR INSURANCE kwakua invoince niliyowapa baada ya wakaguzi wenu kufanya tathmini ilikua ni tsh 4.2milioni bila VAT.

Jana ZANZIBAR INSURANCE wananiambia voucher yangu ya malipo imetoka niende nikaisaini ili nilipwe.
Kituko nnachokutana nacho, ni kwamba iyo voucher ya malipo inaonyesha ni tsh 1.4milioni tu!!!!

Nauliza imekuaje malipo yameshuka tofauti na invoince ya mwanzo wananipa stori za kipumbavu pumbavu tu zisizokua na kichwa wala miguu!!!

Nawaambia kwamba tayari nimeshatumia 3.6m kutengeneza gari eti wananiambia makisio yao ya kutengeneza yanaishia kwenye 1.4m tu!!!! na kama siridhiki ya kiwango icho basi niandike barua tena kukataa kiasi icho, khaaaaa for sure ZANZIBAR INSURANCE THEY ARE SOOO F***K NONSENSE!!

Hasira nilizozipata ilibidi niondoke tu maana ningewatoa manundu wotee kwa kutembeza ngumi za ndoige.

Yaan, utumie zaidi ya miezi mitatu kunilipa ela yangu ya matengenezo

Halafu uniruhusu nitengeneze mwenyewe,mimi nitumie 3.6m, then wewe uje unipe 1.4m?!!!!

What if kwa mtu ambae angekua anasubiilia iyo ela yenu mumlipe kwanza kisha ndo atengeneze gari?

Maana yake ni kwamba gari lingekaa tu bovu miezi yote iyo ? na vipi kama lingekua ni gari la biashara na ndo analitegemea kumuingizia kipato cha maisha yake na familia??!!!

ZANZIBAR INSURANCE MJITAFAKARI SANA,NIMETOKEA KUWACHUKIA MNO!

MARA MIA NINGEKATA THIRD PARTY NIJUE MOJA,KULIKO KUKATA COMPREHENSIVE HALAFU MNITESE NAMNA HII!

ZANZIBAR INSURANCE KAMA NITAKATA BIMA YOYOTE TENA KWENU,MNIITE MBWA, SHENZI KABISA!
 
Halo wasumbufu Santa wapeleke mahakama ya BIMA TILLAmm tulifikishana huko within a week wakawa wameshalipa
 
Back
Top Bottom