Jaji Mkuu; Kesi hii kati ya mmiliki wa gari lililopata ajali na wakala wa bima wa Jubilee Insurance 'inaichafua' Mahakama

Ambakucha

JF-Expert Member
Aug 16, 2019
277
445
Kwanza nikupe kongole Jaji Mkuu kwa kusimamia kwa weledi taasisi yenye kuamua haki kwa Watanzania (na hata wasiyo Watanzania). Umekuwa ukitajwa kufanya vyema katika kuhakikisha mahakama zinakwenda kwa weledi, bila uonevu wala upendeleo.

Kwako wewe, sheria ni sawa na msumeno, ukienda mbele unakata, ukirudi nyuma unakata, ilimradi upite kwenye njia yake. Hata hivyo, sikia hii Jaji Mkuu.

Novemba 3, 2010, gari aina ya Toyota Town Hiace, lenye namba za Usajili T 530 AAA likimilikiwa na bwana, Annuel Stanley Mduma lilipata ajali maeneo ya Mbezi kwa Msuguri kwa kugongwa na gari aina ya Nissan Datsun (pick-up) lenye usajili T 674 ACR, mmiliki Chesco Edward Nongolo.

Town Hiace hilo lilikuwa likiendeshwa na dereva aliyekuwa akitimiza majukumu ya kuwapeleka watoto shuleni kwa tenda.

Baada ya trafiki kupima, ilionekana dereva wa gari la Nissan Datsun ndiye aliyekuwa na makosa ya usalama barabarani, hivyo kwa sababu gari hilo (Nissan) lilikuwa na Bima toka Jubilee Insurance, bwana Mduma alifuata taratibu ili alipwe na wakala huyo lakini kukawa na kusuasua.

Hivyo, Mduma alifungua shauri kwenye Mahakama ya Kinondoni, Dar es Salaam kwa faili namba 138/2011 likisomeka Annuel Stanley Mduma (mdai) Vs Jubilee Insurance (mdaiwa) mbele ya hakimu Mheshimiwa Kasailo.

Kesi ilisikilizwa mpaka mwaka 2014, uamuzi ukatoka kwamba, bwana Mduma ana haki, hivyo alipwe fedha ili kufidia uharibifu wa gari lake. Kwa hiyo kesi hiyo ilikwisha.

Ucheleweshaji wa malipo, ulimfanya Mduma akazie hukumu (kisheria Mahakama inamkumbusha mdaiwa). Jubilee Insurance wakakata rufaa kupinga malipo (inaruhisiwa), Mduma akashinda tena, kwamba alipwe.

(Sheria inaruhusu mdaiwa asipokubaliana na maamuzi), Jubilee Insurance walikata tena rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama ya Kinondoni. Mduma akashinda tena. Jubilee wakakataa kulipa. Mduma akataka kukazia hukumu, faili likapotea. Jubilee wakakata rufaa, faili likaonekana! Hii imetokea mara mbili!

Katika rufaa yao, Jubilee Insurance walitaka kesi ipelekwe Mahakama Kuu.
Mwaka 2015 huko Mahakama Kuu lilifunguliwa faili namba 100/2019 likisomeka Jubilee Insurance (mdai) Vs Annuel Stanley Mduma (mdaiwa), Jubilee wakipinga malipo.

Kesi hiyo ikafika mbele ya Mheshimiwa Jaji Mgonywa ambaye aliitisha faili la kesi iliyokuwa ikisikilizwa Mahakama ya Kinondoni ili kupitia mwenendo wa kesi, akaambiwa lilipotea, linatafutwa.

Toka mwaka huo, 2015, Jaji Mgonywa amekuwa akiitisha faili la kesi hiyo kutoka Mahakama ya Kinondoni. Lakini majibu yameendelea kuwa 'faili halijaonekana' na mwanasheria wa Jubilee Insurance anaomba kesi ianze upyaa! Jambo ambalo Jaji Mgonywa amekuwa akiuliza kwa nini kesi ianze upyaa?

Ilifika mahali, Jaji Mgonywa aliandika Barua kwa Msajili wa Mahakama akitaka faili hilo lipelekwe kwake kwa mwendelezo wa kesi, lakini mpaka sasa halijafika.
Hali hiyo imesababisha kesi kuahirishwa mara zote inapotajwa Mahakama Kuu.

Toka Mwaka huo, 2015 mpaka sasa 2021, ni miaka 6, faili halijapelekwa Mahakama Kuu (halionekani Kinondoni) na kila kesi ikitajwa, jaji akiulizia faili anajibiwa halijaonekana!!

Alhamisi iliyopita, tarehe 29/7/2021, kesi hiyo ilitajwa tena na kuahirishwa tena hadi Septemba, 2021.

Cha kujiuliza Mheshimiwa Jaji Mkuu, kuna nini katika mahakama zetu kesi kusuasua kwa miaka 10 bila kufikia mwisho?! Miaka 10 ni muda mrefu sana tofauti na ambavyo wewe Jaji Mkuu umekuwa ukisisitiza kesi zisichukue miaka mingi kufika mwisho na hukumu ya haki kutendeka.

Naamini Jaji wa Mahakama Kuu, Mheshimiwa Mgonywa anao uwezo wa kisheria kuliangalia hili na kumaliza kesi kwa haki kutendeka kwa pande husika ili maisha mengine yaendelee kama ambavyo ameonesha nia hiyo, hivyo ni matumaini makubwa kuwa, Mheshimiwa Jaji Mkuu utasukuma hili shauri lifike mwisho kwa mara nyingine tena.
 
Hahahaa kudadeki na huyo Mduma kaamua kukomaa nao ananata na biti tu mpaka wamlipe.

Kwakuwa nia yao ilikua akate tamaa na jamaa hakati tamaa kwa kupotezewa muda.

Sasa hilo gari lenyewe bado lipo kweli? Au alishalitengeneza anataka arudishiwe hela yake. Na hiyo hela si atalipwa ishashuka thamani maskini

Unanikumbusha kuna kesi ya kiwanja iko mahakamani toka 1992 kiwanja kilinunuliwa lakI 2 ila saivi kina thamani balaa halafu watu walihukumiwa mwaka jana kimagumashi warudishiwe lakI 2 yao😂😂
 
Kwanza nikupe kongole Jaji Mkuu kwa kusimamia kwa weledi taasisi yenye kuamua haki kwa Watanzania (na hata wasiyo Watanzania). Umekuwa ukitajwa kufanya vyema katika kuhakikisha mahakama zinakwenda kwa weledi, bila uonevu wala upendeleo.

Kwako wewe, sheria ni sawa na msumeno, ukienda mbele unakata, ukirudi nyuma unakata, ilimradi upite kwenye njia yake. Hata hivyo, sikia hii Jaji Mkuu.

Novemba 3, 2010, gari aina ya Toyota Town Hiace, lenye namba za Usajili T 530 AAA likimilikiwa na bwana, Annuel Stanley Mduma lilipata ajali maeneo ya Mbezi kwa Msuguri kwa kugongwa na gari aina ya Nissan Datsun (pick-up) lenye usajili T 674 ACR, mmiliki Chesco Edward Nongolo.

Town Hiace hilo lilikuwa likiendeshwa na dereva aliyekuwa akitimiza majukumu ya kuwapeleka watoto shuleni kwa tenda.

Baada ya trafiki kupima, ilionekana dereva wa gari la Nissan Datsun ndiye aliyekuwa na makosa ya usalama barabarani, hivyo kwa sababu gari hilo (Nissan) lilikuwa na Bima toka Jubilee Insurance, bwana Mduma alifuata taratibu ili alipwe na wakala huyo lakini kukawa na kusuasua.

Hivyo, Mduma alifungua shauri kwenye Mahakama ya Kinondoni, Dar es Salaam kwa faili namba 138/2011 likisomeka Annuel Stanley Mduma (mdai) Vs Jubilee Insurance (mdaiwa) mbele ya hakimu Mheshimiwa Kasailo.

Kesi ilisikilizwa mpaka mwaka 2014, uamuzi ukatoka kwamba, bwana Mduma ana haki, hivyo alipwe fedha ili kufidia uharibifu wa gari lake. Kwa hiyo kesi hiyo ilikwisha.

Ucheleweshaji wa malipo, ulimfanya Mduma akazie hukumu (kisheria Mahakama inamkumbusha mdaiwa). Jubilee Insurance wakakata rufaa kupinga malipo (inaruhisiwa), Mduma akashinda tena, kwamba alipwe.

(Sheria inaruhusu mdaiwa asipokubaliana na maamuzi), Jubilee Insurance walikata tena rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama ya Kinondoni. Mduma akashinda tena. Jubilee wakakataa kulipa. Mduma akataka kukazia hukumu, faili likapotea. Jubilee wakakata rufaa, faili likaonekana! Hii imetokea mara mbili!

Katika rufaa yao, Jubilee Insurance walitaka kesi ipelekwe Mahakama Kuu.
Mwaka 2015 huko Mahakama Kuu lilifunguliwa faili namba 100/2019 likisomeka Jubilee Insurance (mdai) Vs Annuel Stanley Mduma (mdaiwa), Jubilee wakipinga malipo.

Kesi hiyo ikafika mbele ya Mheshimiwa Jaji Mgonywa ambaye aliitisha faili la kesi iliyokuwa ikisikilizwa Mahakama ya Kinondoni ili kupitia mwenendo wa kesi, akaambiwa lilipotea, linatafutwa.

Toka mwaka huo, 2015, Jaji Mgonywa amekuwa akiitisha faili la kesi hiyo kutoka Mahakama ya Kinondoni. Lakini majibu yameendelea kuwa 'faili halijaonekana' na mwanasheria wa Jubilee Insurance anaomba kesi ianze upyaa! Jambo ambalo Jaji Mgonywa amekuwa akiuliza kwa nini kesi ianze upyaa?

Ilifika mahali, Jaji Mgonywa aliandika Barua kwa Msajili wa Mahakama akitaka faili hilo lipelekwe kwake kwa mwendelezo wa kesi, lakini mpaka sasa halijafika.
Hali hiyo imesababisha kesi kuahirishwa mara zote inapotajwa Mahakama Kuu.

Toka Mwaka huo, 2015 mpaka sasa 2021, ni miaka 6, faili halijapelekwa Mahakama Kuu (halionekani Kinondoni) na kila kesi ikitajwa, jaji akiulizia faili anajibiwa halijaonekana!!

Alhamisi iliyopita, tarehe 29/7/2021, kesi hiyo ilitajwa tena na kuahirishwa tena hadi Septemba, 2021.

Cha kujiuliza Mheshimiwa Jaji Mkuu, kuna nini katika mahakama zetu kesi kusuasua kwa miaka 10 bila kufikia mwisho?! Miaka 10 ni muda mrefu sana tofauti na ambavyo wewe Jaji Mkuu umekuwa ukisisitiza kesi zisichukue miaka mingi kufika mwisho na hukumu ya haki kutendeka.

Naamini Jaji wa Mahakama Kuu, Mheshimiwa Mgonywa anao uwezo wa kisheria kuliangalia hili na kumaliza kesi kwa haki kutendeka kwa pande husika ili maisha mengine yaendelee kama ambavyo ameonesha nia hiyo, hivyo ni matumaini makubwa kuwa, Mheshimiwa Jaji Mkuu utasukuma hili shauri lifike mwisho kwa mara nyingine tena.
Kuna haja apa utunzwaji wa mafaili ya kesi uwe kidijitali kwenye data base ya mahakama ili authorized judge awe na uwezo wa ku access ata kama makabrasha yakipotea
 
Mkuu racso kaunda jina sahihi la Jaji unayemtaja kwenye jambo lako ni Jaji Mgonya na si Mgonywa. Pole na kila la heri katika kufuatilia suala lako. Waweza kuandika malalamiko rasmi kwa Jaji Mkuu na kumpatia kiofisi kwa ajili ya utatuzi wa haraka.
 
Katika utetezi wao labda hao Jubilee walikuwa wanasemaje? Kwamba Town Haice haikupata ajali au vipi? Maana nashindwa kuelewa sababu za Jubilee kugomea kulipa fidia wakati wanafanya biashara ya kulipa fidia, ikizingatiwa hadi trafiki alifika kupima ajali!
 
Hapo shida ipo kwa wapelelezi/police rushwa imeshawashinda nguvu!
 
Back
Top Bottom