Zanzibar inachangia nini kwenye Serikali ya Muungano? Isije ikawa wanatumia Kodi za Bara

DASM

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
2,184
2,000
Na siku tukisema wabara tujitoe hao jamaa sijui kama watakubali kirahisi au wanaweza kudai fidia UN utadhani ni ndoa ya binadamu
Siku ya kuiacha Zanzibar naitabiria kuwa itakuwa ni Somalia, Sudan, Syria , Afghanistan mpya . Uwezekano mkubwa wa Unguja na Pemba kujengeana uhasama ni mkubwa Sana. Kale Ka-Zanzibar kanategemea utalii tuu kwaajili ya income. Wataanzisha visheria vitakavyo fukuza utalii ndiopo umasikini utaitafuna Znz. Mafuta ni story za Alinacha ambazo zimekuepo zikiimbwa tokea 1960 hayajawahi kuchimbwa .
 

tinkanyarwele

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
2,000
2,000
Mnalalamika Zanzibar haina mchango wowote kwenye Muungano,ila AJABU NI KWAMBA WAZANZIBARI WAKITAKA KUJIONDOA KWENYR HUO MUUNGANO MNATUMIA HADI MITUTU KUHAKIKISHA HAWAONDOKI.

CCM na viongozi wa serikali wanaotoka Bara akili zao si timamu!
Na mimi hapa huwa sijui kwa nini
 

mgen

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
20,659
2,000
Jee ni kweli au bla bla?!
 

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
12,492
2,000
Zanzibar wananufaila nini na muungano??
Wanamiliki ardhi Tanganyika.

Wanapata teuzi na kazi nyingine za serikalini Tanganyika.

Wanafunzi elimu ya juu wanapata mikopo Tanganyika.

Jaribu wewe mtanganyika
-uende Zanzibar kutaka ardhi uone kama utapata
-katafute mtanganyika aliyeteuliwa ktk SMZ.
-hakuna mtanganyika elimu ya juu anayeweza kupata elimu ya juu.
 

Megalodon

JF-Expert Member
Apr 9, 2021
495
1,000
Watu tunataka Elimu mchango ambao Zanzibar inatoa kwenye Serikali ya Muungano. Naona kama Tunaumia sana sisi wa Bara. Kuubeba Muungano.

Mfano nataka kuoa. Nimeandaa Harusi baadaye nikaamua kutofanya sherehe. Je zile pesa nagawa pia kwa bibi harusi? Ndicho ambacho alichofanya Samia. Yaani pesa hizi ambazo zimeandaliwa na Watanzania Bara kwa Sherehe isiyo na tija kaamua zigawanywe sawa kwa sawa.

Hili suala tuanze likemea mapema. Kodi za Wabara zitumike kwa Wabara. Na Wazanzibar zitumike kwao kwa maendeleo ya nchi yao.

Tabia ya kupendelea eneo moja analotoka Rais ikomeshwe isiendelee.tuliona miradi mingine ilivyokuwa ikipelekwa sehemu ambazo hiyo miradi haikuwa na tija.

Lakini suala langu kubwa ni kupeana Elimu kuwa kuna pesa gani ambazo Bara inapata toka Zanzibar? Au zinaingia kwenye Muungano toka Zanzibar?

But pia hizi pesa anazotaka zipelekwe Zanzibar pia. Zilitokea au patikana wapi? Kodi za Wabara zisitumike vibaya. Watu kwa sasa kwa woga au Unafiki wanashindwa kuhoji hili jambo.

Ila wajue mwanzo wa ngoma ni lelele.... Tusikubali mambo ya hovyo kuendelea. Na mchakato wa Katiba urudishwe ili haya mahusiano yawe yame balance. Zanzibar wasionewe hali kadhalika Bara pia wasionewe. Hawa wabara ndo hata Serikali yao hawana.

Usalama wa Taifa tangu mwanzo, walishataka kabisa uchaguzi mdogo ufanyike. Makamu wa Rais alikuwa ni incompetent kuwa Rais. Kila linalofanywa kwa sasa linafanywa kwa mihemko. Mama hana Dira, na kuna watu nyuma yake ndio wanatoa Instruction. Hii ni hatari sana kwa Ustawi wa Taifa letu. Tunaona Uongozi wa awamu ya nne umeshaanza kupigia debe suala la uenyekiti. Lakini Watanzania tutambue nchi inarudi vyuma tena. Tunaona Chanjo za COVID zitaingizwa soon. Ndjo tujue hapa kunapandikizi na ni suala la muda tu.Chunguza maamuzi ya huyu mama, mengi ni kwa kusikiliza watu na mengine ni kuonesha utawala wa nyuma ulikuwa mbovu. Miaka 4 itaisha na hakuna la maana zaidi ya kutusikilizisha vijembe na kuonesha mtangulizi wake alikuwa hafai. Tutachelewa sana
 

jabulani

JF-Expert Member
Aug 1, 2015
5,005
2,000
Tishio la warusi kuweka sana za kivita Zanzibar halipo tena muungano hauna faida tena kwa Watanganyika.
Nyerere aliogopa cuban missile crisis kujirudia Zanzibar.
 

makwega7

JF-Expert Member
Mar 18, 2018
758
1,000
Wanamiliki ardhi Tanganyika.

Wanapata teuzi na kazi nyingine za serikalini Tanganyika.

Wanafunzi elimu ya juu wanapata mikopo Tanganyika.

Jaribu wewe mtanganyika
-uende Zanzibar kutaka ardhi uone kama utapata
-katafute mtanganyika aliyeteuliwa ktk SMZ.
-hakuna mtanganyika elimu ya juu anayeweza kupata elimu ya juu.
katafute mtanganyika aliyeteuliwa ktk SMZ.
SUZAN PETER KUNAMBI. Mkuu wa wilaya ya Magharibi A.
Mluguru wa Mji kasoro bahari
 

Falconer

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
842
500
Mimi nafurahi sana pale munapo hoji muungano. Sisi wazanzibari hatuutaki huu muungano na kama nyinyi wenzetu hamuutaki basi pelekeni mswad wa kuvunja muungano kupitia viongozi wenu na sisi tuta wasapoti. Nyinyi ni wengi na ndio munao tawala. Kuvunja muungano ni kuondosha udhalalishwaji wa wazanzibari. Koloni pekee lililobakia linalotawaliwa na mwaafrika.
 

dos.2020

JF-Expert Member
Feb 17, 2009
6,042
2,000
Ni usamaria wema tu unatusumbua. Tunaona kabisa tukiwaacha

1. Hamuwezi ujiongoza. Mtasambaratika na kufanya hivyo visiwa viwe vichaka vya magaidi.

2. Hamuwezi kujilisha. Mnaweza mkafa kwa njaa.

Hivi nyinyi ndio mnaweza kujiongoza? 60 years from freedom bado ni among poorest countries duniani?

Na mnachowalisha Zanzibar ni kipi ?
 

dos.2020

JF-Expert Member
Feb 17, 2009
6,042
2,000
Usalama wa Taifa tangu mwanzo, walishataka kabisa uchaguzi mdogo ufanyike. Makamu wa Rais alikuwa ni incompetent kuwa Rais. Kila linalofanywa kwa sasa linafanywa kwa mihemko. Mama hana Dira, na kuna watu nyuma yake ndio wanatoa Instruction. Hii ni hatari sana kwa Ustawi wa Taifa letu. Tunaona Uongozi wa awamu ya nne umeshaanza kupigia debe suala la uenyekiti. Lakini Watanzania tutambue nchi inarudi vyuma tena. Tunaona Chanjo za COVID zitaingizwa soon. Ndjo tujue hapa kunapandikizi na ni suala la muda tu.Chunguza maamuzi ya huyu mama, mengi ni kwa kusikiliza watu na mengine ni kuonesha utawala wa nyuma ulikuwa mbovu. Miaka 4 itaisha na hakuna la maana zaidi ya kutusikilizisha vijembe na kuonesha mtangulizi wake alikuwa hafai. Tutachelewa sana

Hivi ikiwa JIwe ameweza kuwa Raisi wa nchi hii nani atashindwa?
 

gachacha

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
2,192
2,000
Sisi ndo tunawag'ag'ania wanzanzibari maana wao wao wanajihesabu kama nchi mfano kitambulisho cha mzanzibari, Bunge lao, TRA wanayo, ila kiukweli wazee wetu walikosea kwenye muungano walitakiwa zenji iwe mikoa.
 

gachacha

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
2,192
2,000
BOT msingi wake zanzibar ndio walitoa fedha nyingi za kigeni kuanzishwa kwake leo Tanganyika wanajifaragua na BOT wamesahau msingi wake, TRA inakusanya kodi kule zanzibar lakini zile kodi zinaenda kutumika kwa maendeleo ya Tanzania Bara, hizo fly over zote ni hela za karafuu
IMG_20201123_162150.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom