Consigliere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 12,037
- 24,595
Kuna Clip ina trend ikimuonyesha Mkurugunzi wa Mawasiliano Ikulu , Zanzibar, ndugu Charles Hillary akitoa kauli ya onyo kwa wale aliowaita wavamizi wa eneo la hekari 6,000 mali ya SMZ huko Bagamoyo mkoani Pwani.
Kauli hii haina kingine nyuma yake isipokua ni jitihada za kujaribu kuuzima au kuuhamisha mjadala uliowashwa na balozi Karume huko visiwani. Kwa wafuatiliaji wa siasa za Zanzibar watakubaliana na ugumu anaokutana nao rais Hussein Mwinyi katika kuiongoza Zanzibar.
Ili mambo yaende, amelazimika kutoa nafasi kadhaa muhimu za ajira huko serikalini kwa watu kutoka bara. Maana wenyeji wamekua wakifanya mambo yasiende either kwa sababu ya mazoea yao ya kizembe, au sabotage, pia utoaji wa siri.
Hili swala la wabara wengi kupewa nafasi nyingi na nyeti kule ndani ya SMZ, nalo limezidi kuibua manung'uniko huko visiwani.
Wakati hayo yakiendelea, balozi Karume ameibuka na madai yake. Karume anauelewa vizuri sana upepo wa visiwani. Anajua yeye si miongoni mwa sauti zenye ushawishi visiwani, bali anajua vyema kwa hali iliyopo ni kipi cha kuongea ili kuyavutia masikio ya hadhira walio wengi) na kumkosesha utulivu yule aliyepo madarakani.
Kauli ya Charles Hillary imetolewa kwa lengo la kujaribu kuirudisha hadhira upande wa Hussein mwinyi. SMZ inajua kwa kauli ile ya kujifanya wanatengeneza mgogoro na serikali ya JMT atafanikiwa kuubadili upepo wa Karume na kufanikiwa kuwavuta wazanzibar upande wake na kuanza kuuimba wimbo wa kuulalamikia Muungano, kama mjuavyo, huu ni wimbo pendwa sana huko visiwani Zanzibar. Hiyo ndiyo hali iliyopo, juu ya utoto unaofanywa na SMZ.
Lakini, haya yote yanaashiria nini? Hiki ni kiashiria cha vita za ukoo, ni kiashiria cha vita za makundi, ni kiashiria cha minyukano ya kimaslahi. Serikali badala ya kuja ni mambo ambayo yatakua ni long term solution ya changamoto za nchi, wao wanakuja na malundo ya mizigo ya sheria kandamizi, sheria ambazo zina wakinga kutowajibika kwa uonevu wa aina yoyote utakaofanywa kwa wananchi.
Muwe na siku njema