Zamu ya Zanzibar Urais 2015?

Zamu ya Zanzibar Urais 2015?

Watanzania hivi karibuni tumeshuhudia makundi mawili makubwa yanayo utaka Urais ie Kundi la Mafisadi kwa upande mmoja na kundi la Wapinga ufisadi.

Kundi la mafisadi lilanonekana lilijipanga muda mrefu na lina fedha nyingi ambazo limekua likizitumia ili mgombea wao aweze kuibukaa mshindi wa kuiwakilisha CCM kama mgombea. Kundi la Wapinga ufisadi nalo limejikita katika kutetea uzalendo zaidi.

Sasa kwakua kuna kila dalili kwamba Chadema haitaweza kutwaa nchi, na kwakuwa kuna mkinzano mkubwa kati ya makundi haya mawili mimi nashauri kwamba Rais ajaye wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atoke Zanzibar.

Hii itakuwa imeyakata kilimilimi makundi haya ambayo yameacha kufanya kazi za kujenga nchi kwa kuwaza Urais tu. Pia hii itafanya Zanzibar nayo itoe walau Rais wa pili wa Muungano maana zaidi ya Mwinyi hakuna mwingine aliyetoka Zanzibar.

Hii itakuwa safi kama vile Mtaange wa kugombea Uspika kati ya Chenge (akiwakilisha kundi la mafisadi) na Sitta aliyewakilisha kundi la kupinga ufisadi.

CCM ilitumia busara na kuyapiga chini makundi yote na kumchagua mwanamama. Naona CCM pia inaweza kumpata compromise candidate kwa kumtoa mgombea Zanzibar.

Hii imekaaje wadau?

Tunataka Raisi bora hu upuuzi wenu wa atoke wapi mwisho 2014 period!.............chake chake ,kamachumu ........rombo na temeke it doest matter my men,a good presz is a good prez .we need leadership not stupid CCM culture ya atoke huku na ukule
 
Nyie wabara kila wakati mnataka mtu toka bara tu sasa huo ni muungano gani? Hata mwinyi ni mtu wa bara maana katokea bagamoyo so zanzibar actually haijawahi kutoa rais. 2015 zamu ya znz
 
Nyie wabara kila wakati mnataka mtu toka bara tu sasa huo ni muungano gani? Hata mwinyi ni mtu wa bara maana katokea bagamoyo so zanzibar actually haijawahi kutoa rais. 2015 zamu ya znz

Nafasi yenu tulishawapa ni VP. Tangu uzaliwe ulishawahi kusikia PM wa China anatoka Hong Kong au Taiwan? Get real dude.
 
CCM ilitumia busara na kuyapiga chini makundi yote na kumchagua mwanamama. Naona CCM pia inaweza kumpata compromise candidate kwa kumtoa mgombea Zanzibar.

Hii imekaaje wadau?....[/QUOTE]

we nahisi dish lako sio zuri..
 
Ndugu wana bodi na wenye akili na iq ya kupambanua mambo ya kisiasa tujadili jambo hili bila jazba wala matusi. Mimi nikiwa mmoja wa vijana wanaotaka kuiona tanzania yetu ikisonga mbele kimaemdeleo na kiuchumi pamoja na afya ningefurahi kuona rais ajae either atoke chadema cuf tlp nccr mageuzi na hata hata sisiemu atoke upande wa pili wa muungano wetu nikimanisha atoke zanzibar due to tje fact that marais watatu wametoka tanzania bara hiyo haina uwiano wa kimadaraka. Kwa nini rais ajae asitokee zanzibar ama ndio nduguzetu hawana uwezo na iq ya kuongoza. Tutafakari ili kuulinda muungano wetu. Nawasilisha
 
Fahamu ya kwamba rais wa Tanzania 2015 ni LAZIMA AWE MKRISTO. Sasa jiulize je Wazanzibar mna mtu ambaye ni MKRISTO na anafaa kuwa rais 2015? Kama jibu ni hakuna basi kaeni kimya.
 
Sitakutusi ila nitakuuliza ile katiba ya Zanzibar ya sasa umeisoma? Ndugu hatuko pamoja tena! Hata hao UAMSHO wanalijua hili. Ndugu muungano haupo! tusidanganyane!
 
Fahamu ya kwamba rais wa Tanzania 2015 ni LAZIMA AWE MKRISTO. Sasa jiulize je Wazanzibar mna mtu ambaye ni MKRISTO na anafaa kuwa rais 2015? Kama jibu ni hakuna basi kaeni kimya.

Ingawa wewe ni headless hapa nakupalikeumetumia akili sasa iko sehem gani sujuibcause ur headless
 
Wee ratashobanyuma wazanzibar wanajitoa kwenye muungano we bado unawapa urais wa muungano tena? Acha mambo yako bhana.
 
Thubutu! Greed is centre stage. Zanzibar simply out of focus.
 
siku hizi hawaiti tena tanganyika,eti wanaita tanzania bara.
Right, na wao siku hizi wamekataa jina la Tanzania Visiwani, wanaitwa Tanzania Zanzibar. Sisi tukanyimwa jina la Tanzania Tanganyika.

Tuvunje mahusiano tegemezi haya ya Tanzania Zanzibar kutunzwa na Tanzania Tanganyika. Tuwe na Zanzibar na Tanganyika halafu hakuna kupigiana kelele once and for all.

Kuna athari fulani si rahisi kuziona kwa macho, mfano mmoja ni kitu kinaitwa "distraction." Kwenye nchi za watu hata timu ya mpira ikiwa na mtu mmoja anaeleta drama za maisha yake kwenye kambi, mara kakamatwa na polisi mara kakamatwa na machangu, wanamkata kwenye timu hata awe muhimu sana kwa sababu sasa amegeuka gumzo la timu na kuitoa timu kwenye focus.

Sasa Zanzibar ni eneo moja dogo sana, dogo kushinda Newala, Newala ni wilaya iliyo kwenye mkoa kiduchu wa Mtwara, na ni kisiwa chenye umuhimu finyu sana wa kiuchumi kwa Tanzania, ni sawa na mchezaji wa benchi halafu kila siku analeta vioja kwenye timu na kugeuka gumzo, unam cut loose kwenye timu! Sasa kila siku Zanzibar- Bi Kidude kapewa nishani ya Taif Uhuru wa Bara! Zanzibar - Waziri wa Afya sio Mtanganyika, Zanzibar-Uamsho wamechoma makanisa! Zanzibar... Zanzibar... Zanzibar... Zanzibar!

Let's cut Zanzibar loose, they are creating inordinate levels of distraction from Tanganyika's national agenda!
 
Back
Top Bottom