Zaidi ya Vijana 100 waondoka kwenye mradi wa BBT, sababu yadaiwa hakuna uelekeo

Wakulima halisi wenye kazi zao wamewatosa,mna watafuta vijana waliyozoea kushinda kidimbwi ndy muwapeleke shamba,wataweza wapi ???

Ova
Kilimo sio amapiano. Ila huo mradi watu wengi tumelalamika una dalili za upigaji wa hela. Hao vijana wanakuwa mbuzi wa kafara. Hizo hela za bbt wanaenda kukopa nje huko benki ya dunia (WB), Benki ya maendeleo ya Afrika ( Afdb), wanazipiga, kisha vijana wanateseka tu.
 
Karne hii bado Kuna vijana wanaamini katika ujamaa! Hiyo move ilikuwa ya kijamaa sana, kijana inabidi aamini katika ubepari na kupambana mwenyewe hadi ufanikiwe. Yani upewe shamba la bure eka 10 lenye miundombinu sijui na blah blah nyingine ukaamini, ukaacha na shughuli zako kabisaaa what an imbecile!
 
Umenikumbusha miaka ya 90+ huko kuna rasta mmoja tena alikuwa anyone wNgu aliwakusanya marasta kibao tz akawambia waende wakaanzishe maisha morogoro shambani,wawe wanalima tu yaani maisha yao yote yawe huko
Wakaenda bana,unafikiri walikaaa
😄

Ova
 
Zaidi ya vijana 100 wa Programu ya Kuwezesha Ushiriki wa Vijana Katika Kilimo Biashara (BBT- YIA) wanadaiwa kuondoka katika kambi ya Chinangali, Dodoma, ambako vijana hao wamekusanywa, wakidai hakuna mwelekeo kambini hapo, huku wakiishutumu Serikali kwa kushindwa kwake kutimiza ahadi ilizotangaza awali.

Kwa mujibu wa taarifa ilizozifikia The Chanzo, mpaka kufikia jioni ya Machi 19, 2024, vijana waliokuwepo kambini hapo ni kati ya 120 na 128 kutoka vijana 268 ambao Serikali imekuwa ikidai kuwepo Chinangali kushiriki kwenye programu hiyo inayokusudiwa kuongeza ajira za vijana milioni tatu na kuongeza ukuaji wa kilimo nchini hadi kufikia asilimia kumi ifikapo mwaka 2030.

“Watu tulioko pale [kambini] mpaka sasa hivi tunafika 134, kati ya watu 268 tuliotakiwa kuripoti, lakini walioripoti ni 261,” alisema mmoja wa viongozi wa vijana hao ambaye The Chanzo imeamua kutotaja jina lake kulinda usalama wake. “Watu wengine waliobaki hawako kwenye kituo, hawako kwenye kituo kwa sababu pale hakuna kinachoeleweka.”

“Wengine wanakuja, wanakaa siku mbili, wanachungulia, wanaondoka, wale wenye uwezo wa kifedha,” aliongeza kijana huyo. “Kwa siku mbili hizi, [Machi 18 na 19], watu wengi wameondoka, tumebaki watu kama 120 hivi. Lakini muda mwingi tunacheza hapo 120 hadi 130. Wengi wamekimbia hali iliyoko pale [kambini].”

Mmoja kati ya vijana walioondoka kambini hapo ameiambia The Chanzo: “Mimi binafsi nimeondoka, kuna mambo yangu nimekuja kufuatilia. Unajua kipindi kile watu wengi tuliondoka kwa sababu hapakuwa panaeleweka hapo ila nitarudi muda si mrefu. Pale kambini kusema ukweli panaboa. Sasa ukae pale ufanye shughuli gani, sasa ukalime shamba la ushirika ambalo hujui hata utavuna nini?”

The Chanzo ilimuuliza Vumilia Zinkankuba, Mratibu wa Programu ya BBT, endapo kama taarifa za vijana kuondoka kambini hapo zina ukweli wowote, ambapo aliomba apewe kwanza chanzo cha taarifa hiyo ndiyo ajibu kama ni za kweli au la.

The Chanzo, hata hivyo, iligoma kufichua watoa taarifa wake kwani kufanya hivyo siyo tu kungewaweka hatarini bali pia ni kwenda kinyume na maadili ya uandishi wa habari yanayosisitiza umuhimu wa kuwaficha watoa taarifa.

The Chanzo
Kuna mmoja namfahamu kabla ya hapo alikuwa muuza genge na maisha yako powa ila nadhani nae katoroka maana namwona karudia biashara yake ya genge ila kachoka utadhani alikuwa jkt Kwa mujbu wa Sheria.

Kawa mpole , wenzake wanamcheka Kwa ujinga aliofanya
 
Naunga mkono,ni ujinga Kwa Serikali eti kutafutiza graduate na kuwafundisha kulima wakati Kuna Vijana wenye passion wako tayari shambani badala ya kuwawezesha hao wao wanalazimisha jobless awe mkulima.

Serikali acheni huo ujinga wa kupoteza pesa Kwa upuuzi unless ni mradi wenu wa kipigaji.Mbaya zaidi waliochaguliwa ni wale wenye kadi za chama
Shida ilianzia hapa!! tena ngoja yawapate.....Jamaa walichaguliwa kwa kujuana uccm mwingi
 
Zaidi ya vijana 100 wa Programu ya Kuwezesha Ushiriki wa Vijana Katika Kilimo Biashara (BBT- YIA) wanadaiwa kuondoka katika kambi ya Chinangali, Dodoma, ambako vijana hao wamekusanywa, wakidai hakuna mwelekeo kambini hapo, huku wakiishutumu Serikali kwa kushindwa kwake kutimiza ahadi ilizotangaza awali.
Kama tunajenga majengo mazuri makubwa wanashindwa kufanya matengenezo ya vitasa tu ndiyo waweze mradi mkubwa huo, hakuna tunachoweza zaidi ya kujipambanua majukwaani
 
Zaidi ya vijana 100 wa Programu ya Kuwezesha Ushiriki wa Vijana Katika Kilimo Biashara (BBT- YIA) wanadaiwa kuondoka katika kambi ya Chinangali, Dodoma, ambako vijana hao wamekusanywa, wakidai hakuna mwelekeo kambini hapo, huku wakiishutumu Serikali kwa kushindwa kwake kutimiza ahadi ilizotangaza awali.

Kwa mujibu wa taarifa ilizozifikia The Chanzo, mpaka kufikia jioni ya Machi 19, 2024, vijana waliokuwepo kambini hapo ni kati ya 120 na 128 kutoka vijana 268 ambao Serikali imekuwa ikidai kuwepo Chinangali kushiriki kwenye programu hiyo inayokusudiwa kuongeza ajira za vijana milioni tatu na kuongeza ukuaji wa kilimo nchini hadi kufikia asilimia kumi ifikapo mwaka 2030.

“Watu tulioko pale [kambini] mpaka sasa hivi tunafika 134, kati ya watu 268 tuliotakiwa kuripoti, lakini walioripoti ni 261,” alisema mmoja wa viongozi wa vijana hao ambaye The Chanzo imeamua kutotaja jina lake kulinda usalama wake. “Watu wengine waliobaki hawako kwenye kituo, hawako kwenye kituo kwa sababu pale hakuna kinachoeleweka.”

“Wengine wanakuja, wanakaa siku mbili, wanachungulia, wanaondoka, wale wenye uwezo wa kifedha,” aliongeza kijana huyo. “Kwa siku mbili hizi, [Machi 18 na 19], watu wengi wameondoka, tumebaki watu kama 120 hivi. Lakini muda mwingi tunacheza hapo 120 hadi 130. Wengi wamekimbia hali iliyoko pale [kambini].”

Mmoja kati ya vijana walioondoka kambini hapo ameiambia The Chanzo: “Mimi binafsi nimeondoka, kuna mambo yangu nimekuja kufuatilia. Unajua kipindi kile watu wengi tuliondoka kwa sababu hapakuwa panaeleweka hapo ila nitarudi muda si mrefu. Pale kambini kusema ukweli panaboa. Sasa ukae pale ufanye shughuli gani, sasa ukalime shamba la ushirika ambalo hujui hata utavuna nini?”

The Chanzo ilimuuliza Vumilia Zinkankuba, Mratibu wa Programu ya BBT, endapo kama taarifa za vijana kuondoka kambini hapo zina ukweli wowote, ambapo aliomba apewe kwanza chanzo cha taarifa hiyo ndiyo ajibu kama ni za kweli au la.

The Chanzo, hata hivyo, iligoma kufichua watoa taarifa wake kwani kufanya hivyo siyo tu kungewaweka hatarini bali pia ni kwenda kinyume na maadili ya uandishi wa habari yanayosisitiza umuhimu wa kuwaficha watoa taarifa.

The Chanzo
Ipo hivi: Kuna Kampuni ndo waanzilishi wa hizi programs Duniani Kote! Kwa karibu na Tanzania Wapo Zambia:Kilichotokea baada ya hii kampuni kuleta Wazo Biashara(proposal) Bashe na Mwenzake wa Wizara ya Samaki - wakaja na mawazo yao wenyewe ?? WATAPIGA MAHELA NA SOME HOW MIRADI ITAENDA😁😁wakaomba na Rushwa kwa hawa majamaa pia...Wakamwakikishia Mama Samia kuwa kila kitu kitaenda sawa na pia wakawaakikishia wawkezaji hivyo hivyo.Ikimbukwe kama Nchi atuna mbegu zetu wenyewe,ata Mbolea na madawa pia!! Bashe akajiona Mkombozi atafanya , atapiga na mahela pia😂😂Yeye na mwenzake wa Samaki wote chali..... bado kidogo tutaanza sikilizia ile BBT ya Sato kule Mwanza.-Nao Wakileft Group kutokana na Ukapa. Bashe hili daima litamfata kama kivuli katika maisha yake yote yaliobaki hapa Duniani yeye na yule wa samaki
 
Attachments

  • IMG_4744.jpeg
    IMG_4744.jpeg
    31.3 KB · Views: 3
  • IMG_4743.jpeg
    IMG_4743.jpeg
    32.1 KB · Views: 4
  • IMG_4742.png
    IMG_4742.png
    83.2 KB · Views: 3
  • IMG_4741.jpeg
    IMG_4741.jpeg
    50.6 KB · Views: 6
  • IMG_4740.jpeg
    IMG_4740.jpeg
    42.4 KB · Views: 3
Back
Top Bottom