Wanasema Vijana: Haya Ndio yanayotokea Mradi wa BBT. Waziri wa Kilimo Njoo Ujibu Tuhuma

Fursakibao

JF-Expert Member
Dec 12, 2017
6,681
11,123
Nimeitoa sehemu na mwandishi namba yake kaweka. Mimi nafikisha tu unumbe na mjumbe hauwawi.

HISTORIA YA MRADI WA BBT NA UHUNI UNAONDELE

Mradi wa bbt uliandikwa vijana wa kitanzania waombe mwenye umri kwanzia miaka 18-40 wawe wanajihusisha na shughuli za kilimo waliomba vijana wengi zaidi ya ishirini Elfu ila waliochaguliwa watu 812 baadae wakaenda mafunzo ya miezi 4 kuanzia Machi 2023 mpaka Julai 2023, wakiwa katika vituo Atamizi vya kilimo Wizara yenye dhamana ikaongeza muda wa mwezi mmoja mpaka Agosti 2023.

Vijana walikuwa kwenye MATI tofauti tofauti bila kujali hali na changamoto za kipesa mana makubaliano ya awali kulikuwa hakuna posho yoyote (japo upo meongozo ulikuwa unaonyesha kila kijana wabbt atapewa fedha ya kujikimu awapo mafunzoni kupitia ofisi ya waziri mku wizara ya Vijana, ajira.... lakini fedha hizo hakuwafikia vijana wa bbt).

Hivyo kila kijana akiwa kituoni alivumilia changamoto zote mfano kujinunulia sabuni, mafuta ya kupaka, dawa za meno n.k na wengine walikuwa wanatembea 10km kwenda na kurudi shamba na changamoto nyingi sana ila walivumilia wakiamini katika ndoto zao na kutimizia lengo la Mh Rais wetu Mpendwa na serikali.

Vijana waliomaliza wakawa 763 kwa MATI zote kwa ujumla wake. Baada ya hapo wakaitwa Dodoma wakiamini wanaenda kupewa mashamba kwa ajili ya uzalishaji kama walivyoahidiwa na Wizara badala yake wakaambiwa wakapumzike mwezi mmoja wakapewa nauli 75,000 lakini vijana wakaomba kuonana na Waziri ili pesa iongezwe mana wameacha familia na wengine shughuli zao kwa muda wa miezi 5 sasa watarudi vipi mtaani wakiwa hawana chochote na mambo mengi yameharibika.

Vijana hao waliomba kwa kilio kikubwa na kushinikiza kwa machozi mengi basi Mh Waziri wa Kilimo kwa shinikizo la ombi na kutishiwa na Waziri kuwa atafuta mradi na akaahidi anatoa hyo laki 2 ila sharti asiende kutangazwa huko mtaani...hivyo akaongeza kiasi cha 125,000 jumla ikawa 200,000 na wakaambiwa wataripoti Dodoma baada ya mapumziko maana wanatakiwa kwenda JKT kujifunza uzalendo.

Bila kuwa na makubaliano hayo mwanzoni pamoja kauli ya Mh Rais wetu ni sheria ila sheria hiyo hiyo in apply retrospection (Hakuna kurudi nyuma).vijana walipokea kwa moyo mkunjuvu nakuwa tayari kulipigania taifa lao la leo na kesho.

Tokana na changamoto za kibinadamu wachache hawa kwenda JKT kutokana na sababu mbalimbali za kifamilia, kiafya na nyingine nyingi basi hivyo walioenda JKT wakahitimu vijana 688.

Wakiwa JKT wakaambiwa wajaze fomu za kuchagua mashamba anaetaka kwenda chinangali au Ndogowe wilayani Chamwino, mkoani Dodoma na baadae vijana wakaomba likizo ya mwezi mmoja kupumzika, baada ya wizara kutotoa dira kamili ya kinachoendelea hivyo wizara ikakubali na kutoa nauli ya kiasi cha Tsh 200,000, kwa kila mmoja na kutoa taarifa kwamba waliochagua Chinangali watalima mazao ya bustani (horticulture crops) na watapewa Ekari 5 badala ya 10 na waliochagua Ndogowe watapewa ekari 10 kwa kuwa wao watatakiwa kulima mazao ya nafaka na watapewa 150,000 kila mmoja kwa mwezi kwa muda wa miezi 6 na pesa hiyo italipwa kutoka Taesa ikiwa ni elfu 5 kwa siku ikiwa kwa milo mitatu hiyo na mahitaji mengine hivyo kiuhalisia na maisha ya sasa pesa hiyo haitoshi.

Baada ya mafunzo walihaidiwa kwamba izo ekari watakazopewa zitakuwa na miundo mbinu ya umwagiliaji, hati ya miaka 66 na mtaji kama ilivyoahidiwa na Mh Rais na Serikali na viwanja vya square mita 600 mpaka 800 kila mmoja vyenye hati ili watakapoanza kupata fedha baada ya kuzalisha waweze kujenga makazi yao ya kudumu waishi na familia zao maana nyumba zitakazojengwa shambani zitakuwa za kuishi vijana wa 4 kila chumba hivyo sio rafiki kuishi na familia zao, kama ambavyo walivyotangaza fursa hii nzuri hapo awali kwa ajili ya taifa na vijana.

Vijana wakaenda likizo ilipofika tarehe 10 Januari 2024 uongozi au secretariat ikatuma barua ya vijana 268 waripoti shamba la Chinangali kwa nauli zao kuanzia tarehe 15 Januari mpaka tarehe 20 Januari kwa ajili ya zoezi la kukabidhiwa mashamba na hati zao ili waanze uzalishaji na kutoa taarifa kwamba vijana wa Ndogowe wasubiri watapewa taarifa lini wataripoti na tunavyoongea vijana hao bado wapo majumbani hawajui wataripoti lini, huenda wakaripoti au wakapotezewa.

UHUNI ULIPOANZIA

Lakini cha kushangaza yote hayo yaliyotangazwa na kuahidiwa hapo awali hayakuwa kama yalivyosemwa pamoja ya kuwa vijana walitimiza yote matakwa ya Wizara na Badala yake vijana wamepewa shamba moja la ekari 600 walime alizeti vijana 260 walioripoti shamba la Chinangali wote kwa pamoja na wote wakiwa chini ya off-taker na kupewa makazi ambayo kiuhalisia hayakizi vigezo. Japo wamepokea kwa moyo wa dhati kabisa

Lakini baada ya yote hayo vijana wale walioripoti Chinangali hawajapewa mashamba isipokuwa kupiga picha na ma trekta na Mh Waziri. Na kuyapost kwenye mitandao ya kijamii kuonyesha wamepewa mashamba na vitendea kazi jambo ambalo sio kweli.

Mashamba ya chinangali hayajawekwa miundo mbinu yoyote ya umwagiliaji na watalima kutegemea kilimo cha mvua kinyume na makubaliano. Ndoto ya ufaulu wa kilimo cha kisasa na kilimo biasha imehujumiwa moja kwa moja.

Vijana hawajapewa mitaji tena waliohaidiwa badala yake watabaki na hiyo 150,000 kwa mwezi ya kujikimu na kupewa mbegu kisha watalima kwa pamoja bila kujua shamba ni lao au la mwekezaji yani bila mtu kujua eneo lake ni lipi licha ya karatasi za kupangishwa mashamba hayo na masharti magumu zikionyesha shamba na coordinates bila kujua hata hayo mashamba yao yapo sehemu gani na yana hali gani?.

Bado huzuni kubwa katika muda wote huu vijana bbt walipata huzuni kubwa baada ya kuwapoteza ndugu zao wawili kwa kufariki ambao pia hao familia zao hawajapewa stahiki yoyote wala haki yoyote ya mashamba na Wizara imewasahau kama walikuwa hawapo jambalo ni la kusikitisha sana.

Hizo ekari ni tofauti na tangazo lilivyosema na ahadi ya Mh Rais , Mh Waziri wa Kilimo na Bungeni kitu ambacho kinazua taharuki kubwa. Nakuonyesha wazi upo upigaji mkubwa katika utekelezaji wa mradi huu muhimu kwa Taifa.

Kumekuwa na sintofahamu kwenye utekelezaji wa huu mradi na vijana kutishwa wanapouliza au kuhoji kinachoendelea hadi wengine kufikia kuondolewa kwa kuuliza kwao.

Na si hivyo tu hivi tarehe 25 january 2024 Mh Waziri huyo huyo alikutana na vijana chinangali kujibu maoni yao na akaendelea kutoa vitisho na maneno ya kuwadharau vijana hadi wazazi wao, vijana waliojitoa kwa ajili ya kutimiza ndoto zao na ndoto ya Mh Rais kuwa hawawezi kufanikiwa bila BBT wala wazazi wao na Familia zao haziwezi kufanyia hayo wanayoyaomba ambayo ni haki yao baada ya kukidhi vigezo na kusema pia kuwa vijana wa BBT hawakisaidii chama kitu chochote.

Ukihoji unatishiwa na waziri anasema wazi ni ana file lako. Mfano kijana mwezetu Fredrick Ngowi ali mtaja wazi ana file lake. So kumekuwa na vitisho vingi hata mimi Pascal Samwel na wengine tunapotengeneza mazingira ya kutao maoni na kutafuta njia njema ya kushirikisha na kuhakikisha ndoto ya Mh. Rais na taifa itimie nimeanza kunyooshewa vidole kwa ukali wa hali ya juu.

Sis vijana wa bbt kwa umoja wetu tuomba wizara isimamie na kutekeleza kwa ufanisi yale serikali na Mh. Rais wamewania kuyatekeleza. Yani:-

1. Vijana kupewa ardhi kwa ajili ya kilimo biashara kuweza kuilisha nchi na kutoa ajira kwa vijana milioni 3 ifikapo 2030.
2. ⁠vijana kupewa mitaji
3. ⁠vijana kutafutiwa soko lenye uhakika na kuuza mazao kwa bei iliyosokoni (competitive price)
4. ⁠kufikia Ajenda 10/30 yani kilimo kuchangia aslimia kumi kwenye bajeti.

@⁨+255 687 047 111
 
Vijana wa umri kati ya 18 mpaka 40, mkiwa 260; mnaweza kufanya mengi mkiwa na umoja na taarifa zikiufikia umma wote wa Tanganyika.
  • Mnaweza kushtua taifa
  • Mnaweza kulifurahisha taifa
  • Mnaweza kulisanua taifa
  • Mnaweza kulihuzunisha taifa
  • Mnaweza kuliteketeza taifa la waporaji
  • Mnaweza kukikomboa kizazi cha walalamikaji wasio na vitendo

Naamini wakiume ni wengi hapo, ebu fanyeni vikao vya siri, tupate mrejesho wa vitendo.
  • Wakina Julius nao si walifanya vikao vyao kulikomboa taifa?
  • Kina Kinje nao walijaribu
  • Kuna yule mwamba wakuitwa Tuntemeke, hawezi kuwa roli modo?
 
Kuna aliwatuma mkalime?
 
Mwamba unamsagia kunguni Bashe sio kutaja jina tu ukaishia na kutoa namba Yako ya simu kabisa. Utakuwa mkurya au mmasai ww bila shaka.

Naagiza jeshi la polisi likuimarishie Usalama wako mara moja.
 
Back
Top Bottom