Yusuf Makamba: Mokiwa muombee January aote nywele

Yusuf Makamba: Mokiwa muombee January aote nywele

Nilishasema! January Makamba atakua Raisi wa Bumbuli tu!

asante mkuu,mimi ni kada ndani ya ccm na pia ni kiongozi sitaki kusikia habari ya huyu aneyenyoa vipara kama mabaunsa wa disko za usiku,akipitishwa na chama ndio nitapokuwa muasi wa kuikapenia upinzani
 
Nadhani wote mbapoteza muda kujadili wageni km January au makanjanja km lowasa. Rais yupo katulia tuli ni professor Mark mwandosya
 
-------- ni wewe ambae umeshindwa kung'amua alichomaanisha mokiwa. shame on you!

naona mko wengi mliokwishaharibiwa mnatetea ujinga! viongozi wa dini wa namna hii hawafai kabisa kwa usalama wa vijana wetu, wana mawazo hasi kabisa yasiyo na maana yoyote katika ustaawi wa jamii, ni wachafu kuanzia maneno mpaka matendo!
 
hamna kauli kauli ya kufuta hapo ila bi kusisitza tu, HATUWEZI KUONGOZWA NA WANYOA UNGA

ananyoa dongo au unga halafu anataka nchi,anadhani watanzania wote tuna akili sawa kama watu wake wa bumbuli waliomchagua,nyambafu sana huyu january
 
Not unified nation/peoples,michango yenu inaonyesha kuwa wote waislam wanamshambulia askofu na wote wakristo wana muunga mkono askofu nahii ndio trend ya mwaka 2015.

Hiyo ni mojawapo ya sehemu za legacy ya Mr Dhaifu. Historia ya Tanganyika itamkumbuka kwa kutuachia huyu mdudu.
 
Huyu mzee anaweza fikiri anamsaidia kumbe anamdidimiza mwanae,
Kwani Makamb:a yeye hana majini yamrudishie nywele?
 
ananyoa dongo au unga halafu anataka nchi,anadhani watanzania wote tuna akili sawa kama watu wake wa bumbuli waliomchagua,nyambafu sana huyu january

Makamba amjibu Mokiwa

NAIBU Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, amesema hawezi kubishana na Askofu Mkuu mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Valentino Mokiwa, kwa sababu ni kama baba yake.

January aliyasema hayo jana wakati akizungumza na kituo kimoja cha redio jijini Dar es Salaam. January ambaye pia ni mbunge wa Bumbuli mkoani Tanga (CCM), alisema iwapo
Askofu Mokiwa kwa mtazamo wake anaona staili ya unyoaji nywele ni sifa ya urais basi anawaachia waumini wake na Watanzania kupima wenyewe kauli hiyo. Mbali na Mokiwa pia January alitumia nafasi hiyo kujibu kauli ya Rais Kikwete ambaye alimpa ushauri wa kusikiliza ushauri wa wazee kabla ya kufanya uamuzi wake. "Wako wazee wengi ndani ya CCM wa kuwaona na wengine nimekwishawaona na Rais Kikwete kwa nafasi yake ni refarii wa mchezo," alisema January. Alisema kutangaza kwake kugombea si kwamba anataka cheo cha urais kwani kwake urais ni utumishi.

January alitoa kauli hiyo siku moja baada ya Askofu Mokiwa kuzungumzia sifa za mgombea urais akisema nchi haiko tayari kuongozwa na wanyoa ‘unga' (kipara) na kwamba wakati wa Tanzania kuongozwa na vijana haujafika.
Ingawa Mokiwa hakutaja moja kwa moja jina la January, lakini ndiye kijana pekee ambaye ametangaza nia ya kuwania urais na kudai ni wakati wa vijana kushika hatamu za uongozi.

Wasomi nao wamshauri

Baadhi ya wasomi nchini wamemtaka January kufuata ushauri aliopewa na Rais Jakaya Kikwete, asilazimishe kuwania nafasi ya urais kwa sababu wakati ukifika atapata. Akiichambua kauli hiyo, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Benson Bana, alisema haiwezekani kwa mtu kupewa nafasi ya uongozi kama hana uzoefu wa kazi. Dk. Bana alisema kutokana na hali hiyo ndio maana hata, Rais Kikwete alitengenezewa njia kabla ya kupewa jukumu la kuiongoza nchi. Mhadhiri mwingine wa UDSM, Profesa Hajji Semboja alisema kauli ya Kikwete ni ya kiongozi mwenye hekima na busara. Alisema kila chama kina utaratibu wake wa kuchagua wagombea, hivyo alipaswa kufuata utaratibu huo kabla ya kutangaza hadharani.

Kauli ya Kikwete imekuja siku chache baada ya January kutangaza kuwania nafasi hiyo wakati akihojiwa na Shirika la Habari la Uingereza (BBC), wiki iliyopita.

Habari hii imeandikwa na Patricia Kimelemeta, Grace Shitundu na Veronica Romwald (Dar)

Moderators ipachikeni hii kwenye uzi mkuu
 
Wakuu,

Aliyekuwa katibu mkuu wa CCM na akashindwa, amekuja na kiroja na kituko.

Eti amemtaka askofu Mokiwa amuombee mwanae January aote nywele kwa maana Mokiwa alitoa tamko kuwa hawatakuwa tayari kuongozwa na wanyoa unga.

Hii kauli inadhihirisha uelewa mdogo wa wanaCCM

Usilete habari nusu nusu. Leta makala nzima watu waisome. Sio unapotosha tu humu ndani
 
Mkuu huyu amefanya biashara ikulu,alikuwa anatoza watu dola 500-1000 kuonana na JK ikulu.Akiwa mgombea ubunge alifadhili na shemeji zake wazungu wa GGM

Haujui Hata protocal za ikulu we we Nazi yako ni kukalili uliyosikia kwa Fundi viatu
 
chamsingi aachane nae tu huyo askofu,kwanza amaonekana ana matatizo ata ukijaribu kufuatilia status yake ya uongozi akiwa askofu mkuu wa anglinaka unaona kabisa alikuwa ni tatizo ndio maana wakamtimua uongozi wa kanisa.
 
Du ! Hii Kali umejuaje Kama Mzee makamba ni muumini wa Tunguli ? Thibitisha tuone kisha hapo kwenye Udini pamekaaje? Awamu ya kwanza Rais alitoka Tanganyika,ya pili akatoka Zenji,tatu akatoka Tanganyika na awamu ya Nne Tanganyika ,Sasa ni Zamu ya Zanzibar ...
Sasa kama awamu ya tatu na ya nne walifululiza kutoka Tanganyika, hizo zamu ziko wapi? Rais atatoka mahali popote, yeyote mwenye uwezo achukue fomu ajaze, akikubalika atachaguliwa na wananchi!
 
asante mkuu,mimi ni kada ndani ya ccm na pia ni kiongozi sitaki kusikia habari ya huyu aneyenyoa vipara kama mabaunsa wa disko za usiku,akipitishwa na chama ndio nitapokuwa muasi wa kuikapenia upinzani

Kama wewe nikiongozi Wa Ccm bhasi ndio wale voongozi mizigo.Zuma ananyoa mini Na nchi yake ipo wap?hatutauza nchi yet Kwa walanguzi Na mafisadi
 
Makamba amjibu Mokiwa

NAIBU Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, amesema hawezi kubishana na Askofu Mkuu mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Valentino Mokiwa, kwa sababu ni kama baba yake.

January aliyasema hayo jana wakati akizungumza na kituo kimoja cha redio jijini Dar es Salaam. January ambaye pia ni mbunge wa Bumbuli mkoani Tanga (CCM), alisema iwapo
Askofu Mokiwa kwa mtazamo wake anaona staili ya unyoaji nywele ni sifa ya urais basi anawaachia waumini wake na Watanzania kupima wenyewe kauli hiyo. Mbali na Mokiwa pia January alitumia nafasi hiyo kujibu kauli ya Rais Kikwete ambaye alimpa ushauri wa kusikiliza ushauri wa wazee kabla ya kufanya uamuzi wake. “Wako wazee wengi ndani ya CCM wa kuwaona na wengine nimekwishawaona na Rais Kikwete kwa nafasi yake ni refarii wa mchezo,” alisema January. Alisema kutangaza kwake kugombea si kwamba anataka cheo cha urais kwani kwake urais ni utumishi.

January alitoa kauli hiyo siku moja baada ya Askofu Mokiwa kuzungumzia sifa za mgombea urais akisema nchi haiko tayari kuongozwa na wanyoa ‘unga’ (kipara) na kwamba wakati wa Tanzania kuongozwa na vijana haujafika.
Ingawa Mokiwa hakutaja moja kwa moja jina la January, lakini ndiye kijana pekee ambaye ametangaza nia ya kuwania urais na kudai ni wakati wa vijana kushika hatamu za uongozi.

Wasomi nao wamshauri

Baadhi ya wasomi nchini wamemtaka January kufuata ushauri aliopewa na Rais Jakaya Kikwete, asilazimishe kuwania nafasi ya urais kwa sababu wakati ukifika atapata. Akiichambua kauli hiyo, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Benson Bana, alisema haiwezekani kwa mtu kupewa nafasi ya uongozi kama hana uzoefu wa kazi. Dk. Bana alisema kutokana na hali hiyo ndio maana hata, Rais Kikwete alitengenezewa njia kabla ya kupewa jukumu la kuiongoza nchi. Mhadhiri mwingine wa UDSM, Profesa Hajji Semboja alisema kauli ya Kikwete ni ya kiongozi mwenye hekima na busara. Alisema kila chama kina utaratibu wake wa kuchagua wagombea, hivyo alipaswa kufuata utaratibu huo kabla ya kutangaza hadharani.

Kauli ya Kikwete imekuja siku chache baada ya January kutangaza kuwania nafasi hiyo wakati akihojiwa na Shirika la Habari la Uingereza (BBC), wiki iliyopita.

Habari hii imeandikwa na Patricia Kimelemeta, Grace Shitundu na Veronica Romwald (Dar)

Moderators ipachikeni hii kwenye uzi mkuu

mkuu huu ushauri anatakiwa kufuata hatuwezi kumkubali mtu eti kwasababu ni kijana na kumkataa mtu kwasababu ni mzee
 
Wakuu,

Aliyekuwa katibu mkuu wa CCM na akashindwa, amekuja na kiroja na kituko.

Eti amemtaka askofu Mokiwa amuombee mwanae January aote nywele kwa maana Mokiwa alitoa tamko kuwa hawatakuwa tayari kuongozwa na wanyoa unga.

Hii kauli inadhihirisha uelewa mdogo wa wanaCCM

Lazima amtetee mwanaye ,mokiwa anaongozwa kwa chuki.she.nzi hili zee
 
Katika hali ya kukasirishwa na kitendo cha kauli ya askofu mokiwa ; kusema nchi aitaongozwa na wanyoa unga (watu wenye vipara); mzazi wa januari makamba kwa kutumia tafsida , ya kuwa kipara si ugonjwa au kilema na kama askofu akaona ni ugonjwa au kilema . Amfanyie maombi januari ili nywele ziotea .

Ushauri . Askofu najua kajua kauli yake imemchukiza mzazi . Ni wakati wa kuomba au kufuta kauli yake.
Mambo yaende

Huyu si ndio askofu wa kanisa la mabwa.bwa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom