Yusuf Makamba: Mokiwa muombee January aote nywele

Yusuf Makamba: Mokiwa muombee January aote nywele

Hivi Mnyoa kipara ni Janiary peke yake?
Mbona hata mimi nimenyoa Kipara lakin Mzazi wangu kachuna tu na wala hajastushwa na kauli ya Askofu.
Wanasema ukisikia Paaa,basi jua limempata
Usikute bado huyo mwanae anakaa kwao hajaanza kujitegemea ndio Maana baba yupo front hivi January kamtuma baba yake amjibu Askofu au baba kajisemea tu ?
 
Makamba atakuwa bize na tunguli ili mwanawe apate Urais...ni hivi nchi hii haitaongozwa na muislamu tena na hasa kama anayoa upara ndo kabisaaaa

huu ni ujanja wa mbwa kujilamba mk.undu......
 
Ujinga mtupu, anayenyoa unga 24/7/365 naye fara fulani tu, aliyesema kunyoa ni kigezo cha mtu kutokuwa kiongozi naye fara fulani tu; January pamoja na unga wake aseme kwanini nchi ni masikini kwa zaidi ya miaka 50 ya uhuru na atafanya nini ambacho sasa hawezi fanya ili kubadilisha hali hii dhaifu ya wananchi
 
Ujinga mtupu, anayenyoa unga 24/7/365 naye fara fulani tu, aliyesema kunyoa ni kigezo cha mtu kutokuwa kiongozi naye fara fulani tu; January pamoja na unga wake aseme kwanini nchi ni masikini kwa zaidi ya miaka 50 ya uhuru na atafanya nini ambacho sasa hawezi fanya ili kubadilisha hali hii dhaifu ya wananchi
Kibongo bongo si unajua ahadi huwa ni zile zile za nitajenga Hosptal ,barabara ,shule,Madaraja na kuboresha huduma za jamii ikiwemo maji,kilimo nk ,Binafsi Sidhani Kama January Makamba anaweza Kuwa Rais wa Tz , na ikitokea CCM wakampitisha kugombea Urais basi wajue Kuwa wamesafisha njia kwa Chadema kuingia ikulu.
 
Ni rahisi kuyaona mawe yakiongea kuliko January kuwa Rais.

Ni rahisi kwa Ngamia kupenya kwenye Tundu la sindano kuliko January Makamba Kuwa Rais wa Tanzania.
 
Baadhi ya wanyoa upara ambao ni marais combred jacob zuma, josefu kabila na mtarajiwa wetu January makamba wote ni viongozi makini barani africa

Kwa kuwa ametangaza nia anatakiwa kutulia na kusikiliza watu wanavyomsema bila kupambana nao kwa maneno, mwisho wa siku sanduka la kura kuanzia ngazi ya Chama chake hadi kwa Umma litaamua.
 
Ni rahisi Ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko rais kutoka kwenye chama cha upinzani Tanzania.

Ni rahisi kwa Ngamia
kupenya kwenye Tundu la sindano kuliko January Makamba Kuwa Rais wa
Tanzania.
 
Huyo makamba nae anaongea pumba.

CCM wote watupu kichwani
 
Naomba kurudia kutoa shukrani zangu za dhati
kwa wale wote miongoni mwenu, wake kwa
waume, wazee kwa vijana, walionitumia ujumbe
na salamu kutoka pande zote za nchi - kwa
kupiga simu, kwa kutuma ujumbe mfupi wa
simu na kupitia mitandao ya kijamii - kueleza
kufurahishwa kwao na uamuzi wangu wa
asilimia 90 kutaka kujitokeza kugombea Urais
wa Taifa letu pale muda utakapowadia, na kwa
mujibu wa taratibu za Chama chetu cha CCM.
Nimepokea salamu nyingi sana za kunitia moyo
katika kipindi hiki ninapoendelea kujitathmini na
kupata nasaha, baraka na ushauri kutoka kwa
wazee wetu, viongozi wetu wa zamani na wa
sasa, na viongozi wetu wa dini. Nafarijika sana
kwamba wengi wenu mmeupokea uamuzi
wangu kwa furaha sana. Tueendelee kuwa
pamoja na naahidi sitawaangusha. Tukifanikiwa,
na wakati utakapofika, tutaendesha kampeni ya
kihistoria itakayotoa matumaini mapya kwa
Tanzania mpya.
Pia nimesoma na kuyapokea kwa moyo
mkunjufu maoni ya baadhi yenu, ambao kwa
namna moja au nyingine hamkupendezwa na
uamuzi wangu. Hata nyie, kama ilivyo kwa
Watanzania wote, mnayo haki na uhuru wa
kutoa maoni yenu. Naahidi kuyazingatia na
kuyafanyia kazi maoni na mawazo yenu, hasa
yale yenye kujenga na kuimarisha mjadala juu
ya Tanzania tuipendayo.
Najua wengi mna shauku kubwa ya kufahamu
kwa mapana na marefu mawazo yangu juu ya
namna gani tunaweza kuibadili nchi yetu kuwa
bora zaidi. Kwa sasa naomba subira kidogo
kutoka kwenu. Wakati muafaka ukiwadia,
nitaeleza kwa mapana na marefu fikra zangu
kuhusu Tanzania mpya tuitakayo. Mjadala wa
kuhusu aina ya uongozi tunaoutaka na sifa za
Rais atakayefuata, pamoja na mahitaji ya nchi
yetu ni mjadala bora zaidi kuliko mjadala
unaendelea sasa wa majina ya wagombea Urais
au ule mjadala wa "vijana dhidi ya wazee". Nchi
yetu hii ni nchi yetu wote bila kujali umri.
Tunapoongelea kuhusu nia na haja ya kuwa na
uongozi wa kizazi kipya hatumaanishi kwamba
hiyo ndiyo sifa pekee ya Urais kama baadhi
wanavyotaka ieleweke.
Nchi yetu ina changamoto nyingi lakini bado ni
nchi nzuri na mfano wa kuigwa hapa Afrika.
Wapo viongozi waliotangulia ambao wamefanya
tuwe na sifa hii. Wazee wetu ni hazina katika
Taifa letu na wataendelea kushirikishwa katika
ujenzi wa nchi yetu. Ili kuleta fikra mpya,
maarifa mapya na majawabu mapya kwa
changamoto mahsusi za zama hizi, wengi wetu
tunaamini wakati umewadia sasa wa
kupokezana kijiti kutoka kizazi kimoja hadi
kingine cha uongozi, na siyo kizazi hicho hicho
kimoja kupokezana kijiti. Na wala hili sio jambo
la ajabu kwasababu huu ndio umekuwa
utamaduni wetu katika awamu zote. Kila kizazi
kina changamoto zake na kina wajibu wake.
Wakati umewadia kwa kizazi cha sasa kushika
usukani ili nacho kitengeneze mustakabali wake
mpya badala ya kuendelea kutumiwa na
wanasiasa kama daraja tu wakati wa kuomba
kura na baadaye kuwekwa kando katika
maamuzi makubwa yanayohusu mustakabali wa
nchi yetu.
Pia, wakati tukitumia haki yetu ya kujadili
kuhusu Rais ajaye, ni muhimu kutambua
kwamba nchi yetu inaye Rais sasa hivi mwenye
mamlaka kamili na ridhaa kubwa ya wananchi
– na lazima aheshimiwe na apewe nafasi ya
kufanya kazi yake. Ningependa kurudia shukrani
zangu za dhati kwa Mheshimiwa Rais Dr.
Jakaya Kikwete kwa ziara yake aliyoifanya wiki
iliyopita jimboni kwetu Bumbuli kukagua
shughuli za maendeleo na kuhimiza utekelezaji
wa Ilani ya uchaguzi ya CCM. Namshukuru
sana kwa maneno yake ya busara, yaliyojaa
hekima na yenye kutia moyo aliyoyasema juu
yangu.
Mwisho, nawasihi sana wapenzi na mashabiki
wangu kujiepusha na malumbano yasiyo na
msingi, hasa hasa wale wanaotumia jina langu
kufanya hiyo. Tuwe wavumilivu wa mawazo
yaliyo tofauti na yetu. Hiyo ndiyo njia pekee ya
kupanua demokrasia yetu. Tujenge hoja zaidi
badala ya kulipiza dhihaka juu yangu kwa kutoa
dhihaka juu ya wagombea wengine au kutoa
dhihaka kwa wazee wetu kwa ujumla. Hata
hivyo msiache kunisemea pale mnapoona kuna
njama za makusudi za kupindisha ukweli juu
yangu na juu ya makusudio yangu. Kuomba
uongozi ni kuomba utumishi. Sio mapambano.
Sio suala la kufa na kupona. Unaomba kibali
kwa Mungu kuwaongoza watu wake kupitia
ridhaa yao. Tusisahau kumuomba Mungu
atupatie kiongozi mzuri mwenye hekima na
atakayetenda haki kwa watu wote.
Asanteni sana.
Pamoja tunaweza.
January Makamba (MB),
17-7-2014
 
Hivi huyu mnyoa kipara ana rekodi ipi ya utendaji hapa Tz zaidi ya kubebwabebwa tu? Hapo wizarani alipo kafanya nini cha maana? Huyu ni kibaraka wa mafisadi na hatumuhitaji kwani hafai hata kwa udiwani tu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom