Yuko wapi yule dereva "Giriki" wa basi la Tawaqal?

Sharuks : Abbas Gulamali Mhindi wa Ifakara .
Dar Oyee : Gulam Somji Mhindi wa Mahenge.
Halafu kulikuwa na Ulanga Express , mali ya Ushirika wa vijiji vya Tarafa ya Malinyi.
mtemiwaWandamba! Hawijeee!!! Hawijeee!! Kaimuka Bamboo!! Ha ha ha! Long time kitambo!

Nimeishi kwa miaka mingi sana huko Kilombero miaka ile ya 90's mpaka mwanzoni mwa 2000!! Nimeishi Nyandeo, Mang'ula, Ifakara, Mahenge, Namwawala, Chita,nk.
 
Giriki alikuwa akikaa kwny seat na kushika usukani wamama wanasali sana, wengine wakiulizana ni Giriki anatupeleka?

Mimi najua alikuwa anaendesha Dar - Mbeya
Baadae alihamia Singea - Dar akakutana na akina Okalla, Rwambi na Yoge wakivurumisha Kiswele, John Africa na Mapunda wakiwa na Special coach na yeye Giriki akiwa na Tawaqal.

Wakati huo Omary Msigwa tajiri wa Super Feo alikuwa anauza duka la mjomba wake pale Njombe!
 
Mabasi yaliyosafiri asubuhi ni Railway na KAMATA!
 
Hahahaaaa...... Long time bwashee!

Ila umenikumbusha ile Chai maharage ya Rpc Tryphon iliyokuwa inapiga route ya Masaki - Posta!
Ah mm dar nishakuwa konda kwenye coaster
Za Italy trans na kuna coaster ya baharia mmoja ilikuwa ina chata time will tell
Wamilik wote hao walikuwa wajanjajanja wa zamani,na ili kuwa kufanya kazi na watu kama hao na wakukubali lazima uwe mjanja

Ova
 
Alishaendesha pia kampuni ya mabasi ya safina syo ...dar - mby
Ila enzi zile Nissan diesel zilikuwa znatembea sana,alafu ile stop engen zake ahh ni balaa

Ova
Nissan Diesel UD nazo zilitikisa sana bwashee.

Makete Bus walitoa mbili Dsm - Njombe zilikuwa moto chini na mzee Kiwanga wa Makambako alitoa mbili zikiitwa Ilanga Moto!
 
Haikua kitonga,zilikua zile kona za kwenda songea,alikua anatoa fuse ya taa za break,kama amekutangulia kwenye kona anakanyaga break kwa kua fuse katoa huoni,unakuja moto mara kona hii hapa unaanza kuhangaika nayo
 
Ah mm dar nishakuwa konda kwenye coaster
Za Italy trans na kuna coaster ya baharia mmoja ilikuwa ina chata time will tell
Wamilik wote hao walikuwa wajanjajanja wa zamani,na ili kuwa kufanya kazi na watu kama hao na wakukubali lazima uwe mjanja

Ova
Si unajua awali mabaharia walikuwa wakishuka lazima wawavue wazee nyumba za national housing laki laki baadae wakaanza kununua coaster.

Pale Kinondoni zilikuja coaster zikapewa chata ya Mo Money duh zilitesa sana ilibidi akina Simba Luwala wabadilishe route!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…