Kabla hatujaanza kuushangaa huu waraka mpya wa Papa Francis tujikumbushe waraka wa mwezi uliopita, kanisa katoliki linaelekea wapi ?

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
Waraka huu mpya umewasilishwa bado tukiwa kwenye sintofahamu ya waraka wa mwezi uliopita ulioruhusu maaskofu kubatiza waliobadili jinsia na kuwaruhusu wawe wazazi wa kibatizo bila kutoa msisitizo mkali kwamba suala la kubadili jinsia ni chukizo kwa Mungu.

Chanzo cha uhakika cha kupata matamko, waraka, speech, barua, n.k. huwa ni tovuti ya makao makuu ya kanisa katoliki Vatican, lugha za uwasilishaji huwa ni kiitaliano, kiingereza, kifaransa, kijerumani, kihispania, n.k.

Tamko hili liliwekwa 3 November 2023 na unaweza kulisoma hapa >> Answers to Several Questions from His Excellency, the Most Reverend José Negri, Bishop of Santo Amaro, Brazil, Regarding Participation in the Sacraments of Baptism and Matrimony by Transgender Persons and Homosexual Persons (3 November 2023)

1. Je, mtu aliebadili jinsia anaweza kubatizwa ?

Mtu aliebadili jinsia ambaye amepitia matibabu ya homoni na upasuaji wa kubadilisha jinsia anaweza kupokea ubatizo kama ilivyo kwa waumini wengine wa kanisa katoliki ikiwa hakuna hali ambayo italeta taharuki kwa kwenda kinyume na utaratibu wa zoezi la ubatizo. Kwa watoto au vijana wadogo wenye mashaka katika ubadilishaji wa jinsia, wakiwa tayari na wanapotaka wanaweza kupokea ubatizo.

Kwa wakati huo huo, Vifuatavyo ni muhimu kuvizingatia, hasa wakati panapokuwa na shaka kuhusu hali ya maadili, lengo au kuhusu nia yake kuelekea neema.

Katika Ubatizo, Kanisa linafundisha kwamba, wakati sakramenti inapopokelewa bila toba kwa dhambi kubwa, anaebatizwa hawezi kupokea utakatifu wa kiroho, ingawa atatambulika kapata ubatizo. Katekisimu inasema: misingi ya Kristo na Kanisa iliyofikiwa na Roho, haifutwi bali inabaki milele ndani ya Mkristo kama hali chanya kuelekea neema kama ahadi na uhakikisho wa ulinzi takatifu na kama wito wa ibada ya kimungu na utumishi wa Kanisa.

Mtakatifu Thomas wa Aquinas alifundisha kwamba wakati kitu kilichokuwa kikizuia neema ya Mungu kabla ya ubatizo kinaondolewa kwa mtu ambaye aliebatizwa bila kuwa na nia sahihi, alama maalum ya kiroho wanayoipata wakati wa ubatizo inawasaidia kuwa wazi zaidi kupokea neema ya Mungu. Mtakatifu Augustine wa Hippo alikumbusha hali hii akisema kwamba, hata kama mwanadamu anajikuta katika dhambi, Kristo haangamizi alama aliyopokea kwake katika Ubatizo, alama hii imemweka wazi kama mali yake.

Hivyo, Inatupasa tuelewe kwamba Papa Francis alitaka kusisitiza kwamba ubatizo ni mlango unaomruhusu Kristo kujiweka ndani yetu na sisi tuweze kuzama katika imani yake. Hii inamaanisha kwa vitendo kwamba hata milango ya Sakramenti haipaswi kufungwa kwa sababu yoyote ile hata kama mtu kabadili jinsia ama anafanya mapenzi ya jinsia moja. Hii ni kweli hasa linapokuja suala la sakramenti ya mlango wa ubatizo...., Kanisa katoliki si ofisi ya forodha, ni nyumba ya baba ambapo kuna nafasi kwa kila mtu na maisha yao yenye taabu.

Hivyo, hata wakati shaka zinabaki kuhusu hali ya maadili ya mtu au nia yake kama ni nzuri ama mbaya kuelekea neema ya Bwana, hatupaswi kamwe kusahau upendo wa dhati usio na masharti wa Bwana, Hata pale mtu anapokosea mara kwa mara, Mapenzi ya Mungu yapo wazi na anaweza kumrudia kutengeneza uhusiano imara. Mapenzi haya yapo wazi ila hubadilika kwa maana hatuwezi kutabiri matendo yetu ynavyoweza kuathiri uhusiano. Hata ale ambapo mtu anaefanya juhudi kumrudia Bwana ana uwezekano wa kuendelea kufanya makosa, hatuwezi kubeza jitihada zake za kutaka kubadilika. Hivyo yatupasa tuthamini jitihada zao kila moja wetu anaetaka kubatizwa na kuungana nao kwenye safari ya kikristo

2. Je, mtu aliebadili jinsia anaweza kuwa mzazi wa ubatizo katika Kanisa Katoliki ?

Mtu mzima aliebadili jinsia anaweza kuruhusiwa kuchukua jukumu la kuwa mzazi wa ubatizo. Hata hivyo, busara ya kichungaji inahitaji isiwezeshe zoezi hili ikiwa kuna ukiukaji wa utaratibu wa ubatizo unaoweza kuleta taharuki ama kuidhinisha kwa njia isiyofaa.

3. Je, mtu aliebadili jinsia anaweza kuwa shahidi wa ndoa?

mtu aliebadili jinsia anaweza kuwa shahidi wa ndoa za kikatoliki chini ya misingi sawa na ile inayotoa ubatizo kwa waumini wengine.

4. Je, watu wawili wa jinsia moja wanaweza kuwa wazazi wa ubatizo kwa mtoto ambaye anapaswa kubatizwa, ikiwa mtoto huyo wamemuasili ?

Ndio inawezekan, Ili mtoto apate ubatizo, lazima kuwe na matumaini yenye msingi kwamba ataelimishwa katika dini ya Katoliki (angalia kanuni ya 868 1, 2 au CIC; kanuni ya 681, 1, 1st CCEO).

5. Je, watu wenye jinsia sawa wanaoishi pamoja wanaweza kuwa kuwa wazazi wa ubatizo kwa mtu ambae tayari kabatizwa ?

Kulingana na kanuni ya 874 1, 1o na 3o CIC, yeyote mwenye uwezo na "anaishi maisha yanayolingana na imani na jukumu analochukua" anaweza kuwa mzazi wa ubatizo. Hali ni tofauti ambapo kuishi pamoja kwa watu wawili wa jinsia moja siyo tu kuhusiana na kuishi pamoja, bali ni wawe na uhusiano thabiti unaofahamika na jamii.

Kwa hali yoyote, busara ya kichungaji inahitaji kuzingatia kwa busara kila hali, ili kuhifadhi sakramenti ya ubatizo na hasa upokeaji wake, ambao ni mali yenye thamani inayopaswa kulindwa, kwani ni muhimu kwa wokovu.

Kwa wakati huo huo, ni muhimu kuzingatia thamani halisi inayotolewa na jumuiya ya Kikristo kwa majukumu ya wazazi wa kibatizo, jukumu walilonalo katika jumuiya, na heshima wanayoiweka kuendana na mafundisho ya Kanisa. Mwishowe, inapaswa pia kuzingatiwa kwamba kuna uwezekano wa kuwepo kwa mtu mwingine kutoka familia ambaye anaweza kuhakikisha uhamisho sahihi wa imani ya Katoliki kwa mtu anayebatizwa, huku wakijua kwamba wanaweza bado kumsaidia mtu anayebatizwa, wakati wa ibada, si tu kama wazazi wa kibatizo bali pia kama mashahidi wa tendo la ubatizo.

6. Je, wapenzi wawili wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja wanaweza kuwa mashahidi wa ndoa ?

watu wenye jinsia zinazofanana wanaopendana na kuishi Pamoja wanaweza kuwa mashahidi wa ndoa za kikatoliki chini ya misingi sawa na ile inayoruhusu waumini wengine kuwa mashahidi wa ndoa.
 
Ukisoma hapo,

Aliyebadili JINSIA haguswi, Wala kuambiwa kitendo Cha kubadili JINSIA ni makufuru/ Abomination.

Nimewambia Wakatoliki,

Solution ni kuhama, hakuna kitu inaitwa Formal na Informal blessing - Rabbon.
 
Kweli tupu,lakini watabishaa
 
Mada iko pumped kinyama
X-mass kaa nyumbn kwakutulia
 
Ukisoma hapo,

Aliyebadili JINSIA haguswi, Wala kuambiwa kitendo Cha kubadili JINSIA ni makufuru/ Abomination.

Nimewambia Wakatoliki,

Solution ni kuhama, hakuna kitu inaitwa Formal na Informal blessing - Rabbon.
Wahame wahamie wapi?

Mimi Mkatoliki napenda ibada za Kanisa langu kwa sababu zina utulivu,zina mpangilio maalumu wenye mantiki nahubiriwa neno la Mungu kwa ajili ya mustakabali wa maisha yangu ya baadae (siyo ahadi za maisha mazuri au kumiliki vitu vizuri pasipo kufanya kazi au kusengenya wengine).

Sihubiriwi chuki kwamba wale wana dhambi ile au hawamuabudu Mungu kwa njia inayopaswa na kwamba sisi ndiyo tupo sahihi sana,mambo ni mengi ambayo kwa wengine siwezi kuyapata ilikuwa at least Anglican lakini nao wameshaenda tofauti na aliyoyaagiza Mungu KKKT huwa naingia lakini ibada za kelele siziwezi huwa naona kama sala zangu hazifiki.

Ukweli ni kwamba hili ni shambulio baya sana kwa kizazi chetu kiimani (yalishakuwepo mengine mengi tu na yalipita) ila naamini hata hili litapita.
 
Tunakoelekea sasa hawa Roman Catholic Church wanataka kuhalalisha yale ambayo watu wengi duniani watalikimbia kanisa hilo
 
Wanaolengwa ni kizazi kibichi cha vijana na watoto, wataohama ni wale wachache ambao umri upo jioni ama usiku.

Mikakati kibao ishawekwa, hawajakurupuka !!
 
Nikweli na ni hatari sana kwa kizazi kijacho yaani saizi mtoto wa kulindws kama mboni ya jicho ni wa kiume
Kuna misamiati mipya ishatungwa na inapewa promo kubwa sana kubrainwash kizazi kipya kwamba mtu anechukua ushoga ama usagaji inabidi aitwe neno flani na ni sawa na gaidi.

Mtoto hata umfungie bado kuna shule, tv, simu, n.k. kimawazo hana fensi ila kimwili waweza kumdhibiti, Maya zaidi waweza mkataza kwamba ushoga sio mzuri ila anavyoona hao watu wanabarikiwa anaweza kukuona wewe ndie shetani.
 
Ni sahihi kabisa mkuu,saizi mpaka katuni za watoto nyingi zimewekwa ushoga,yaani hapa ni kuomba Mungu tu asimame mwenyewe,watoto wetu watapitia katika kizazi kichafu sana
 
Tupo kwenye kipindi cha majatibio makubwa kuwahi kutokea, Novemba mwezi uliopita walianza kuruhusu kubatiza waliobadili jinsia, juzi wameruhusu kutoa baraka kwa wapenzi wa jinsia moja, kwa speed hii tutegemee mwakani wataruhusu maaskofu kuoana wao kwa wao.
 
Hili kanisa msipoangalia kuna siku mtalishwa mikate na divai za ki rainbow
Ni heri wale karismatic walioshtuka.
 
Ukisoma hapo,

Aliyebadili JINSIA haguswi, Wala kuambiwa kitendo Cha kubadili JINSIA ni makufuru/ Abomination.

Nimewambia Wakatoliki,

Solution ni kuhama, hakuna kitu inaitwa Formal na Informal blessing - Rabbon.
Hapa solution siyo kuhama. Bali suluhisho lisilo na zengwe ni kwa Bara la Afrika kuanzisha Kanisa, na hivyo kujitenga na Kanisa la wenzetu wenye ngozi nyeupe. Maana mila na tamaduni zao, haziendani kabisa na hizi za kwetu. Wenzetu wamekuwa na uhuru uliopitiliza.

Kwa hiyo hakuna sababu ya msingi ya kuishi kinafiki baina ya watu wenye mitazamo tofauti, mila, tamaduni na desturi tofauti kabisa, nk.
 
Tukiegemea Mila za kiafrika, Kuna watu watakwambia habari za matambiko ya Mizimu yaruhhsiwe sababu ni asili yetu.

KANISA ni mtu mmoja mmoja.

Mila na asili yetu ni Mbinguni,

Ukiokoka na Kuzaliwa mara ya pili, unakuwa raia wa Mbinguni,

Unakuwa mtu mwingine kabisa, tofauti na watu wa Dunia katika Kila kitu.

KATIBA yetu na mwongozo ni Neno la Mungu na ROHO MTAKATIFU.

Ubarikiwe
 
Wahame wahamie wapi?

Mimi Mkatoliki napenda ibada za Kanisa langu kwa sababu zina utulivu,zina mpangilio maalumu wenye mantiki nahubiriwa neno la Mungu kwa ajili ya mustakabali wa maisha yangu ya baadae (siyo ahadi za maisha mazuri au kumiliki vitu vizuri pasipo kufanya kazi au kusengenya wengine).

Sihubiriwi chuki kwamba wale wana dhambi ile au hawamuabudu Mungu kwa njia inayopaswa na kwamba sisi ndiyo tupo sahihi sana,mambo ni mengi ambayo kwa wengine siwezi kuyapata ilikuwa at least Anglican lakini nao wameshaenda tofauti na aliyoyaagiza Mungu KKKT huwa naingia lakini ibada za kelele siziwezi huwa naona kama sala zangu hazifiki.

Ukweli ni kwamba hili ni shambulio baya sana kwa kizazi chetu kiimani (yalishakuwepo mengine mengi tu na yalipita) ila naamini hata hili litapita.
Jua na mwezi vinaenda kuungana na kuanzisha dini Moja ya Ibilisi.

Soon utaanza kuona utekelezaji.

Solution ni kukimbia, kuhama, kimbilia mlimani, watakatifu, wakristo wa Kweli wataanza kuwindwa, kufungwa na kuuwawa kama ilivyokuwa Kanisa la kwanza.

Tusubiri.
 
Waraka huu mpya umewasilishwa bado tukiwa kwenye sintofahamu ya waraka wa mwezi uliopita ulioruhusu maaskofu kubatiza waliobadili jinsia na kuwaruhusu wawe wazazi wa kibatizo bila kutoa msisitizo mkali kwamba suala la kubadili jinsia ni chukizo kwa Mungu.

Chanzo cha uhakika cha kupata matamko, waraka, speech, barua, n.k. huwa ni tovuti ya makao makuu ya kanisa katoliki Vatican, lugha za uwasilishaji huwa ni kiitaliano, kiingereza, kifaransa, kijerumani, kihispania, n.k.

Tamko hili liliwekwa 3 November 2023 na unaweza kulisoma hapa >> Answers to Several Questions from His Excellency, the Most Reverend José Negri, Bishop of Santo Amaro, Brazil, Regarding Participation in the Sacraments of Baptism and Matrimony by Transgender Persons and Homosexual Persons (3 November 2023)

1. Je, mtu aliebadili jinsia anaweza kubatizwa ?

Mtu aliebadili jinsia ambaye amepitia matibabu ya homoni na upasuaji wa kubadilisha jinsia anaweza kupokea ubatizo kama ilivyo kwa waumini wengine wa kanisa katoliki ikiwa hakuna hali ambayo italeta taharuki kwa kwenda kinyume na utaratibu wa zoezi la ubatizo. Kwa watoto au vijana wadogo wenye mashaka katika ubadilishaji wa jinsia, wakiwa tayari na wanapotaka wanaweza kupokea ubatizo.

Kwa wakati huo huo, Vifuatavyo ni muhimu kuvizingatia, hasa wakati panapokuwa na shaka kuhusu hali ya maadili, lengo au kuhusu nia yake kuelekea neema.

Katika Ubatizo, Kanisa linafundisha kwamba, wakati sakramenti inapopokelewa bila toba kwa dhambi kubwa, anaebatizwa hawezi kupokea utakatifu wa kiroho, ingawa atatambulika kapata ubatizo. Katekisimu inasema: misingi ya Kristo na Kanisa iliyofikiwa na Roho, haifutwi bali inabaki milele ndani ya Mkristo kama hali chanya kuelekea neema kama ahadi na uhakikisho wa ulinzi takatifu na kama wito wa ibada ya kimungu na utumishi wa Kanisa.

Mtakatifu Thomas wa Aquinas alifundisha kwamba wakati kitu kilichokuwa kikizuia neema ya Mungu kabla ya ubatizo kinaondolewa kwa mtu ambaye aliebatizwa bila kuwa na nia sahihi, alama maalum ya kiroho wanayoipata wakati wa ubatizo inawasaidia kuwa wazi zaidi kupokea neema ya Mungu. Mtakatifu Augustine wa Hippo alikumbusha hali hii akisema kwamba, hata kama mwanadamu anajikuta katika dhambi, Kristo haangamizi alama aliyopokea kwake katika Ubatizo, alama hii imemweka wazi kama mali yake.

Hivyo, Inatupasa tuelewe kwamba Papa Francis alitaka kusisitiza kwamba ubatizo ni mlango unaomruhusu Kristo kujiweka ndani yetu na sisi tuweze kuzama katika imani yake. Hii inamaanisha kwa vitendo kwamba hata milango ya Sakramenti haipaswi kufungwa kwa sababu yoyote ile hata kama mtu kabadili jinsia ama anafanya mapenzi ya jinsia moja. Hii ni kweli hasa linapokuja suala la sakramenti ya mlango wa ubatizo...., Kanisa katoliki si ofisi ya forodha, ni nyumba ya baba ambapo kuna nafasi kwa kila mtu na maisha yao yenye taabu.

Hivyo, hata wakati shaka zinabaki kuhusu hali ya maadili ya mtu au nia yake kama ni nzuri ama mbaya kuelekea neema ya Bwana, hatupaswi kamwe kusahau upendo wa dhati usio na masharti wa Bwana, Hata pale mtu anapokosea mara kwa mara, Mapenzi ya Mungu yapo wazi na anaweza kumrudia kutengeneza uhusiano imara. Mapenzi haya yapo wazi ila hubadilika kwa maana hatuwezi kutabiri matendo yetu ynavyoweza kuathiri uhusiano. Hata ale ambapo mtu anaefanya juhudi kumrudia Bwana ana uwezekano wa kuendelea kufanya makosa, hatuwezi kubeza jitihada zake za kutaka kubadilika. Hivyo yatupasa tuthamini jitihada zao kila moja wetu anaetaka kubatizwa na kuungana nao kwenye safari ya kikristo

2. Je, mtu aliebadili jinsia anaweza kuwa mzazi wa ubatizo katika Kanisa Katoliki ?

Mtu mzima aliebadili jinsia anaweza kuruhusiwa kuchukua jukumu la kuwa mzazi wa ubatizo. Hata hivyo, busara ya kichungaji inahitaji isiwezeshe zoezi hili ikiwa kuna ukiukaji wa utaratibu wa ubatizo unaoweza kuleta taharuki ama kuidhinisha kwa njia isiyofaa.

3. Je, mtu aliebadili jinsia anaweza kuwa shahidi wa ndoa?

mtu aliebadili jinsia anaweza kuwa shahidi wa ndoa za kikatoliki chini ya misingi sawa na ile inayotoa ubatizo kwa waumini wengine.

4. Je, watu wawili wa jinsia moja wanaweza kuwa wazazi wa ubatizo kwa mtoto ambaye anapaswa kubatizwa, ikiwa mtoto huyo wamemuasili ?

Ndio inawezekan, Ili mtoto apate ubatizo, lazima kuwe na matumaini yenye msingi kwamba ataelimishwa katika dini ya Katoliki (angalia kanuni ya 868 1, 2 au CIC; kanuni ya 681, 1, 1st CCEO).

5. Je, watu wenye jinsia sawa wanaoishi pamoja wanaweza kuwa kuwa wazazi wa ubatizo kwa mtu ambae tayari kabatizwa ?

Kulingana na kanuni ya 874 1, 1o na 3o CIC, yeyote mwenye uwezo na "anaishi maisha yanayolingana na imani na jukumu analochukua" anaweza kuwa mzazi wa ubatizo. Hali ni tofauti ambapo kuishi pamoja kwa watu wawili wa jinsia moja siyo tu kuhusiana na kuishi pamoja, bali ni wawe na uhusiano thabiti unaofahamika na jamii.

Kwa hali yoyote, busara ya kichungaji inahitaji kuzingatia kwa busara kila hali, ili kuhifadhi sakramenti ya ubatizo na hasa upokeaji wake, ambao ni mali yenye thamani inayopaswa kulindwa, kwani ni muhimu kwa wokovu.

Kwa wakati huo huo, ni muhimu kuzingatia thamani halisi inayotolewa na jumuiya ya Kikristo kwa majukumu ya wazazi wa kibatizo, jukumu walilonalo katika jumuiya, na heshima wanayoiweka kuendana na mafundisho ya Kanisa. Mwishowe, inapaswa pia kuzingatiwa kwamba kuna uwezekano wa kuwepo kwa mtu mwingine kutoka familia ambaye anaweza kuhakikisha uhamisho sahihi wa imani ya Katoliki kwa mtu anayebatizwa, huku wakijua kwamba wanaweza bado kumsaidia mtu anayebatizwa, wakati wa ibada, si tu kama wazazi wa kibatizo bali pia kama mashahidi wa tendo la ubatizo.

6. Je, wapenzi wawili wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja wanaweza kuwa mashahidi wa ndoa ?

watu wenye jinsia zinazofanana wanaopendana na kuishi Pamoja wanaweza kuwa mashahidi wa ndoa za kikatoliki chini ya misingi sawa na ile inayoruhusu waumini wengine kuwa mashahidi wa ndoa.
Pole hamna tafuta bwana tu uolewe
 
Siku Papa alipotangaza kuwa Biblia imepitwa na wakati na kwamba inatakiwa kuandaliwa Biblia mpya,ili kuwa ni kielelezo tosha kuwa yafuatayo ni machafuko. Sasa mpinga Kristo yu dhahiri.
 
Tukiegemea Mila za kiafrika, Kuna watu watakwambia habari za matambiko ya Mizimu yaruhhsiwe sababu ni asili yetu.

KANISA ni mtu mmoja mmoja.

Mila na asili yetu ni Mbinguni,

Ukiokoka na Kuzaliwa mara ya pili, unakuwa raia wa Mbinguni,

Unakuwa mtu mwingine kabisa, tofauti na watu wa Dunia katika Kila kitu.

KATIBA yetu na mwongozo ni Neno la Mungu na ROHO MTAKATIFU.

Ubarikiwe
Halafu sijawahi kuamini mpaka leo hii na Ukatoliki wangu kama kufanya matambiko ni dhambi!! Yaani kuiomba mizimu kutuletea mvua, kuondoa mikosi, kutuletea mavuno mengi, nk. eti ni dhambi!!

Na pia siamini kama kama unaweza kuokoka hapa duniani. Zaidi naona tu watu wanahangaika tu kwenda huku na kule, kutafuta kitu cha aina ile ile.
 
Back
Top Bottom