Inasikitisha sana kuona kwamba Wadanganyika kwa kawaida yao leo tunajiita Stupid kwa kebehi wakati sisi ni stupid kweli!.. Tuwe stupid mara ngapi ikiwa wazungu husema Stupid is what stupid does (Forrest Gump). Sisi wote hapa ni reflection ya viongozi wetu na tumeonyesha u stupid wetu kwa kuwaunga mkono madaktari nao wapewe posho maadam wabunge wanapata..Hatujui kusema No is NO! kumbe ni ile NO ya kiswahili ukisema wakati mwingine ndio YES, kukubali mchezo.
Mwaka juzi kabla ya Uchaguzi TUCTA, walitaka kufanya maandamano ya mgomo ili kuongezewa mishahara kwa watumishi wa Umma hasa kima cha chini. Watu walisema sana hadi kiongozi wao akatafutiwa uchawi na kuitwa kibaraka na mchonganishi...akaachwa solemba ajkijiuma na kujificha huku na huku bila msaada. Baada ya hapo hakuna mtu hata mmoja aliyeinua kidole kukemea maamuzi ya serikali wala kuandaa Upinzani wa nguvu kutokana na maamuzi ya serikali na hasa hotuba ya JK kwa wazee wa Dar - es - Salaam... Ukwa ndio mwisho wa kila kitu.
Majuzi tu tumeshuhudia Katiba ikipatiwa sheria kinyemela na tukalazimishwa kuikubali kama ilivyo na kufuata masharti yaliyopitishwa na Bunge, tumafanya nini ? zaidi ya kuendeleza - Parapanda limelia parapanda na kumshukuru Mungu kuwa yeye ndiye mwamuzi! Ati Jk asingeweza kutoweka saini kwa sababu wanaCCM wenzake wasingemwelewa.. Mijitu ikatoka pale na furaha kwamba JK kasema anakubaliana nao ila....
Leo hii Madaktari wasiokuwa na hata na chembe ya Uzalendo wanaweka mgomo nchi nzima kuhatarisha maisha ya wananchi wanapewa support japokuwa mishahara ya watu wengine midogo sana, huduma za Hospital acha mbali kutowepo kwa vitendea kazi na madawa hizo huduma zenyewe haziridhishi lazima uhonge kiasi kukutana na daktari Tsh 5,000 hadi 10,000 kwa zahanati na Hospital ndogo, Tsh 40,00 hadi 50,000 kwa zile za Rufaa. haya hatuyaoni kama mzigo kwa wananchi lakini tupo radhi kuikosoa serikali kwa kutowalipa madaktari posho zao. Kama hakuna vitendea kazi kwa nini mnatutoza fedha za kuwaona?.
Hizi ndizo athari za UTUMWA. kwa wale waliopinga kwamba Kutawaliwa haikuwa athari kubwa ktk maendeleo yetu inabidi wafikirie upya maana tumezoea kuendeshwa kwa mabora na kukemewa. Hii ni mifano mizuri sana kuonyesha kwamba mtumwa akikemewa mara moja huacha kudai haki yake kwa hofu ile ile alorithi toka kwa mababu zake. Na tunapopewa Unyapala hujiona sisi miungu na wenye nafasi nzuri kuliko mtumwa shambani.. Wewe nyapala kupewa wadhifa huna lolote bado ni mtumwa tu.
Nitaendela kusema kwamba siasa za Bongo ni za kudanganyana tu hakuna mkombozi wala hakuna mtu mwenye uchungu na Taifa hili hivyo tukubali matokeo na kuishi ndani ya giza kama tulivyolelewa - Na ukweli utabakia kwamba UBEPARI hatuuwezi wala hatujui miiko na maadili yake zaidi ya ku copy na ku paste mifumo ya watu kama vazi la suti..Tunavaa ili nasi tuonekane kama wazungu japokuwa nje ni jua kali nyuzi 40 na kumcheka yule alovaa kanzu kwa sababu ni vazi la waarabu.
- Tunadai, ni Kudai, kudai, kudai tu...