Yes madam Speaker, We are stupid!

Haya mambo ya Serkali hii ni aibu, I thot kua level ya aibu isha fika to the Maximu; But this tops it up for it is really stupid. kuna mambo ambayo ni mazito na twajua kabisa kua as much as wataka control iende the way Uongozi unataka kweli inashindikana, but such contradictions kama hii ambayo wangeweza control .... ni aibu mno! Na it shows kua hakuna mahusiano mazuri kati ya uongozi waoote, kila mmoja anafanya vitu independently ama kuna wanaoingilia wizara ambazo haziwahusu kabisa. Sad.
 
Kinachoisumbua jamii sio kwamba posho ni legal, illegal or anything of a kind. Tunaangali is it fair kwa wabunge kujilipa kaisi hichi chini ya lindi la umaskini huu unawakumba Watanzania? Sekta ya afya wanalia na hatuhitaji macho ya darubini kila aliyetembelea hospitali za umma anajua hilo. Hospitali ya Taifa-Muhimbili wagonjwa wanalala wanne kwenye kitanda cha mtu mmoja na kila mmoja ana ugonjwa wake. Walioko chini ni wengi zaidi waliopo vitandani. Sasa kama Muhimbili kuko hivi mikoani kukoje. Madaktari na wauguzi wanalia wako lowly paid. Hujaenda sekta ya elimu. Nenda sijui wapi kote ni vilio. Sasa kuna fairness kweli kwa wabunge kujiongezea mishahara. Na hili la posho ni moja.Tupanue wigo tuangalie safari za viongozi nje zisizokuwa lazima na mabilioni yanayoteketezwa. Tuangalie na posho ktk sekta ya umma ambayo watu wanalipana. Yawezekana ni legal but is it right? Is it fair amidst poverty?
?
 
Zimeongezwa bila idhini ya rais wa jamhuri :lol:

What a President.....!!!! na bado anatabasamu na kutoa taarifa ya kukanusha kwamba hajasaini sijui sijui hajafanya nini, hata simuelewi .....namhurumia Rais wangu, sijui anaogopa au amerogwaaa...

Mr President wake up, you have the power, and its not too late......
 
Not the president, not the prime minister not the speaker! They are all lies and betrayers .

There is one day we shall ask you to pay back.
 
Yes we are! Vinginevyo tukiulizwa "je posho za vikao vya wabunge zimeongezwa?" Tutajibu vipi?

Mwanakijiji,

Tatizo kubwa tilonalo TZ si huyu mama pamoja na mapungufu yake, lakini lazima tukubali hatuna BUNGE, kama ni hili hili BUNGE Mh Mungai alikuja na muswaada wa kusimamisha michezo mashuleni na mitala na wakakubali kwa kishindo, anakuja JK akrudisha muswaada na ikapita tena kwa kishindo.

Sitashangaa kama akija mwingine akaleta muswaada kuwa wanafunzi wanaruhusiwa kuonana shuleni, utapita tuuuu, kama wakati wa bunge , spika anakubali wabunge kufanyiwa tafrija na mashirika, yaani wanaacha kumaliza usiku wa manane ili kuokoa pesa ,badala yake wanawahi kwenye sherehe?

Bunge hatuna mkuu, kwani kama tungekuwa na BUNGE imara wangemtimua si sheria inaruhusu yeye nani kwani?
 
Inasikitisha sana kuona kwamba Wadanganyika kwa kawaida yao leo tunajiita Stupid kwa kebehi wakati sisi ni stupid kweli!.. Tuwe stupid mara ngapi ikiwa wazungu husema Stupid is what stupid does (Forrest Gump). Sisi wote hapa ni reflection ya viongozi wetu na tumeonyesha u stupid wetu kwa kuwaunga mkono madaktari nao wapewe posho maadam wabunge wanapata..Hatujui kusema No is NO! kumbe ni ile NO ya kiswahili ukisema wakati mwingine ndio YES, kukubali mchezo.

Mwaka juzi kabla ya Uchaguzi TUCTA, walitaka kufanya maandamano ya mgomo ili kuongezewa mishahara kwa watumishi wa Umma hasa kima cha chini. Watu walisema sana hadi kiongozi wao akatafutiwa uchawi na kuitwa kibaraka na mchonganishi...akaachwa solemba ajkijiuma na kujificha huku na huku bila msaada. Baada ya hapo hakuna mtu hata mmoja aliyeinua kidole kukemea maamuzi ya serikali wala kuandaa Upinzani wa nguvu kutokana na maamuzi ya serikali na hasa hotuba ya JK kwa wazee wa Dar - es - Salaam... Ukwa ndio mwisho wa kila kitu.

Majuzi tu tumeshuhudia Katiba ikipatiwa sheria kinyemela na tukalazimishwa kuikubali kama ilivyo na kufuata masharti yaliyopitishwa na Bunge, tumafanya nini ? zaidi ya kuendeleza - Parapanda limelia parapanda na kumshukuru Mungu kuwa yeye ndiye mwamuzi! Ati Jk asingeweza kutoweka saini kwa sababu wanaCCM wenzake wasingemwelewa.. Mijitu ikatoka pale na furaha kwamba JK kasema anakubaliana nao ila....

Leo hii Madaktari wasiokuwa na hata na chembe ya Uzalendo wanaweka mgomo nchi nzima kuhatarisha maisha ya wananchi wanapewa support japokuwa mishahara ya watu wengine midogo sana, huduma za Hospital acha mbali kutowepo kwa vitendea kazi na madawa hizo huduma zenyewe haziridhishi lazima uhonge kiasi kukutana na daktari Tsh 5,000 hadi 10,000 kwa zahanati na Hospital ndogo, Tsh 40,00 hadi 50,000 kwa zile za Rufaa. haya hatuyaoni kama mzigo kwa wananchi lakini tupo radhi kuikosoa serikali kwa kutowalipa madaktari posho zao. Kama hakuna vitendea kazi kwa nini mnatutoza fedha za kuwaona?.

Hizi ndizo athari za UTUMWA. kwa wale waliopinga kwamba Kutawaliwa haikuwa athari kubwa ktk maendeleo yetu inabidi wafikirie upya maana tumezoea kuendeshwa kwa mabora na kukemewa. Hii ni mifano mizuri sana kuonyesha kwamba mtumwa akikemewa mara moja huacha kudai haki yake kwa hofu ile ile alorithi toka kwa mababu zake. Na tunapopewa Unyapala hujiona sisi miungu na wenye nafasi nzuri kuliko mtumwa shambani.. Wewe nyapala kupewa wadhifa huna lolote bado ni mtumwa tu.

Nitaendela kusema kwamba siasa za Bongo ni za kudanganyana tu hakuna mkombozi wala hakuna mtu mwenye uchungu na Taifa hili hivyo tukubali matokeo na kuishi ndani ya giza kama tulivyolelewa - Na ukweli utabakia kwamba UBEPARI hatuuwezi wala hatujui miiko na maadili yake zaidi ya ku copy na ku paste mifumo ya watu kama vazi la suti..Tunavaa ili nasi tuonekane kama wazungu japokuwa nje ni jua kali nyuzi 40 na kumcheka yule alovaa kanzu kwa sababu ni vazi la waarabu.
- Tunadai, ni Kudai, kudai, kudai tu...
Unaishi nchi gani ndugu yangu!! wanyonge wa nchi hii unaowatetea ni bahati mbaya sana hawajui haki zao otherwise wangekuwepo wooote leo barabarani kwa yanafofanywa na watawala wa nchi hii......believe me.....sasa hivi imebaki kila mtu kuanza kuitafuta haki yake kwa nafasi yake......when your basic employment rights are not met by the employer(despite persistent requests)kinachobaki ni strikes tu...there is no point for morality here....kwani madaktari wao malaika wanaoishi mbinguni??madaktari ni employees wenye madai ya msingi yasiyosikilizwa na waajiri....Mbona huwazungumzii wabunge wanaopokea 200,000 na wanakaa kimya...wakati hao ndio tungetegemea wawe wa kwanza kuwazungumzia raia maskini waliowapa kura??........unawalaumu madaktari bure kwani wao robots!!......ndugu yangu..udaktari ni fani ambayo inadharauliwa sana na watawala hapa tz(just do a research on how doctors are treated in other countries in africa alafu linganisha na tz).My brother...of all the people you should throw stones at are your pathetic Government and not the doctors who are just fighting for their rights....just like any other employees who know their unsatisfied rights.....
 
Hatuwezipata inside information za kama wamelipwa au la? na kama wamelipwa kwa idhini ipi? kama ni ya Mkuu imesainiwa lini tukalinganisha na kanusho la Salvatory Rweyemamu kisha tukachukua hatua? kama tarehe zinapishana tutajua cha kufanya

Watanzania (lawama zangu ni kwetu sie tunaojiita wasomi) tuna kesi ya kujibu kwa watanzania wenzetu ambao hawajapata fursa ya kwenda shule, fursa ya kuielewa siasa ya Tanzania, fursa ya kuielewa serikali yetu.
 
Zimeongezwa bila idhini ya rais wa jamhuri :lol:

Kama zimeongezwa bila idhini yake, ikulu haioni kuwa imedhalilishwa?
Nadhani ingekuwa hajaidhinisha asingenyamazia kubezwa kwa kiasi hicho,vinginevyo rais wetu anadharauliwa sana na wasaidizi wake kitu ambacho ni kibaya huenda kuliko hata kuidhinisha posho ambayo anataka kunawa mikono kuwa hahusiki.
 
Hadi kutufikiria kwamba hatujui wabunge wanalipwa posho za vikao wanapokuwa kwenye vikao kama siyo kutuona wajinga ni nini?
 
Inasikitisha sana kuona kwamba Wadanganyika kwa kawaida yao leo tunajiita Stupid kwa kebehi wakati sisi ni stupid kweli!.. Tuwe stupid mara ngapi ikiwa wazungu husema Stupid is what stupid does (Forrest Gump). Sisi wote hapa ni reflection ya viongozi wetu na tumeonyesha u stupid wetu kwa kuwaunga mkono madaktari nao wapewe posho maadam wabunge wanapata..Hatujui kusema No is NO! kumbe ni ile NO ya kiswahili ukisema wakati mwingine ndio YES, kukubali mchezo.

Kaka Mkubwa, at least tunakubaliana kuwa kweli tu stupid kwa kukubali kuwa reflection ya watawala wetu. Ila hapo kwenye madai ya madaktari well, I think we are stupidy but with our stupidity making sense. Id rather allow madaktari wadai posho (even if that is not the only madai) na wapewe kwa kuwa impact ya kazi zao wa watanzania wa kawaida tunaifeel zaidi kuliko impact ya mbunge ambaye baada ya kupata kura za miaka mitano sijamwona tena akitia mguu jimboni na wala sijui huko bungeni anafanya nini kunisaidia mimi mtanzania wa kawaida ambaye nilimpa kura yangu (kama hakuiiba/foji).

Mwaka juzi kabla ya Uchaguzi TUCTA, walitaka kufanya maandamano ya mgomo ili kuongezewa mishahara kwa watumishi wa Umma hasa kima cha chini. Watu walisema sana hadi kiongozi wao akatafutiwa uchawi na kuitwa kibaraka na mchonganishi...akaachwa solemba ajkijiuma na kujificha huku na huku bila msaada. Baada ya hapo hakuna mtu hata mmoja aliyeinua kidole kukemea maamuzi ya serikali wala kuandaa Upinzani wa nguvu kutokana na maamuzi ya serikali na hasa hotuba ya JK kwa wazee wa Dar - es - Salaam... Ukwa ndio mwisho wa kila kitu.

Hapa tupo pamoja tu stupid.

Majuzi tu tumeshuhudia Katiba ikipatiwa sheria kinyemela na tukalazimishwa kuikubali kama ilivyo na kufuata masharti yaliyopitishwa na Bunge, tumafanya nini ? zaidi ya kuendeleza - Parapanda limelia parapanda na kumshukuru Mungu kuwa yeye ndiye mwamuzi! Ati Jk asingeweza kutoweka saini kwa sababu wanaCCM wenzake wasingemwelewa.. Mijitu ikatoka pale na furaha kwamba JK kasema anakubaliana nao ila....

I salute you for this too, Sir,

Leo hii Madaktari wasiokuwa na hata na chembe ya Uzalendo wanaweka mgomo nchi nzima kuhatarisha maisha ya wananchi wanapewa support japokuwa mishahara ya watu wengine midogo sana, huduma za Hospital acha mbali kutowepo kwa vitendea kazi na madawa hizo huduma zenyewe haziridhishi lazima uhonge kiasi kukutana na daktari Tsh 5,000 hadi 10,000 kwa zahanati na Hospital ndogo, Tsh 40,00 hadi 50,000 kwa zile za Rufaa. haya hatuyaoni kama mzigo kwa wananchi lakini tupo radhi kuikosoa serikali kwa kutowalipa madaktari posho zao. Kama hakuna vitendea kazi kwa nini mnatutoza fedha za kuwaona?.

Ninachofikiria hapa ni kuwa tunaunga mkono the WHOLE PACKAGE na si posho tu. Na je suala la ukosefu wa vifaha na madawa lawama zinafaa kwenda kwa nani? Mkuu mimi si Daktari na wala kazi ya uuguzi siijui but ninajaribu tu kuwaza anguish, fear na guilty anayoipata daktari pale ambapo anajikuta anapoteza maisha ya mgonjwa wake kwa sababu tu amekosa kifaa au dawa husika, kama binadamu kuwa anajihisi kuwa amesababisha yeye kwani mgonjwa amepoteza maisha akiwa mikononi au chini ya uangalizi wake na yeye kama binadamu si atajihesabu moja kwa moja kuwa anahusika na kifo kile??

Hivi ni kweli serikali imeshindwa kutuwekea huduma stahiki mahospitalini? wanadai haina fedha, kwa nini hawataki kupanua tax base yao? wafanyabiashara wangapi wanakwepa kuylipa kodi kwa mibaraka ya ndugu, rafiki na ten percents? kuna wananchi kiasi gani wanaofanya biashara za kupangisha nyumba ambao hata kufikiriwa kuingizwa kwenye tax pool bado?

Mbona walimu tunawapigia debe kuwa wanaishi maisha magumu, wanafundisha katika mazingira magumu lakini hatuhoji ukosefu wa madawati, chalka na vifaa vingine vya kufundishia?

Kaka Mkubwa mimi si mwanasiasa, wala sina uelewa wowote katika haya niliyoyahoji kwa hiyo ninatanguliza samahani kama kuna nililouliza ambalo ni swali la kijinga. Wewe ni mojawapo ya kisima cha elimu ninayoihitaji hapa JF hasa kwenye ukumbi huu. Ninaomba unisaidie kuelewa. Aksante
 
kuna thread ya zamani kuhusu JK kukimbia Monduli, mleta mada alisema "si mnamjua JK anavyojua kupiga fitna?" leo nimekubali mshkaji mkali, chezea ****** veve
 
Hili la madakatari linaonekana kutukera zaidi ya mengine pengine ni kwasababu kazi yao inagusa maisha yetu moja kwa moja.
Kumekuwa na kauli kama za 'kukosa uzalendo', kazi ya wito n.k.
Kwa vile tunaogopa kukosa huduma zao na kupoteza maisha basi lawama ni juu ya kukosa uzalendo na kazi ya wito.

Nimeuliza maswali haya na wale wanaopinga mgomo wa madaktari hawalijibu. Hivi uzalendo unaanzia kwa nani na unaishia kwa nani.
Pili, hivi kazi ya udaktari haiuruhusu mtu kuwa na maisha ni mpaka akanyagwe kichwani kwa 'kosa' la kuwa mtaalam muhimu sana.

Ninavyofahamu, uzalendo ni suala la kila mtu. Wabunge ambao wanatembea juu ya zulia lenye bendera ya taifa na kula sehemu kubwa ya keki ya taifa ndio wangetuongoza katka uzalendo.
Wabunge si wataalam na yoyote yule mwenye mdomo anaweza kuwa mbunge, lakini si kila mtu aweza kuwa mwalimu au daktari. Uwepo wa wabunge ni heshima ya uzalendo wanaopewa na jamii ndiyo maana hakuna qualification.

Kama mbunge anayepata ( 130,000 kwa sasa) bado anataka apewe 330,000 KWA SIKU kwasababu maisha ni magumu hatuoni hili tunaona 'stupidity' ya yule anayeuliza kwanini wagonjwa walale chini basi we're real stupid.
Kama hatuoni kuwa mbunge anapaswa kuwa mzalendo bali tunaona madai ya masilahi kama usaliti, we're real stupid

Endapo hatuoni mil 64 kwa siku kwa posho za wabunge tu zingeweza kununua vitanda katika wodi moja basi we're stupid.

Hivi kwanini ukisema sijatosheka ionekane ni ukosefu wa uzalendo, lakini yule aliyekula na kusaza na sasa anatupa jalalani aonekana shujaa!!


Off topic: Comment number 55 imetumwatumwa na Bakuza kwa kutumia avatar yangu. Nakanusha ya kuwa hayo si maoni yangu
 
ndio, sisi wajinga, na ndivyo tulivyo, na rais wetu, wabunge wetu na wanasiasa wote kwa ujumla wake wanatufahamu kuwa sisi tu wajinga, mimi mjinga zaidi.
 
Hadi kutufikiria kwamba hatujui wabunge wanalipwa posho za vikao wanapokuwa kwenye vikao kama siyo kutuona wajinga ni nini?
Mama Spika anapambana na dhamira yake. Anayoyafanya au kuyasema hayaamini. Hayatoki moyoni mwake. Amesoma uhasibu halafu anakwambia "take home" ya Wabunge ni ndogo sana kwa sababu ya madeni waliokopa wenyewe! Anakwambia pia kwamba Wabunge wanagawia watu pesa hizi! Maisha ni magumu Dodoma.
Najua hataki kuwa "one term Speaker" kama mtangulizi wake. Atafanya kila kitu anachooona kitawafurahisha hawa jamaa. Sioni anahofia nini kama Lowasa ndie ajae baada ya huyu "Yohana Mbatizaji".
 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni jamhuri ya kigeografia...yes! Ni nchi ya matumaini na maisha wanaoyexperience wazawa ni ya kusadikika...Sijui lini tutaishi maisha halisi!

Rais Kikwete ni Rais kwa kua alikua alishikilia mpini wakati wa uchaguzi (na si utamaduni kwa kiongozi aliyeko madarakani kuondoka kabla ya muda "wake" wa miaka kumi)...Ni Mtawala asiyefaa kuwa hata mjumbe wa nyumba kumi..Yes! Amani anayohubiri huko duniani ni Documentary tu...tumechoka sema tunahofia uhai wetu kwani kudai haki ni uhaini!

Tabasamu la Mgonjwa leo halitangazi "amani tuliyonayo Tz" bali ni mshangao kwamba imewezekanaje kua hai hadi muda huu....Madaktari tunaona wamekosa uzalendo na utu kibinadamu kwa kuzingatia unyeti wa kitengo chao ila frankly ni tusi kugawiana fedha zetu ilihali hakuna la maana mnalosimamia Bungeni zaidi ya blah blah na kuuza tu sura ilihali Mahospitali yakikosa vifaa vya uuguzi na madawa!...

We are Stupid Mkuu MM...hata ubongo niliotumia hapa sio wangu..
 
Back
Top Bottom