Yes madam Speaker, We are stupid!

Hii habari nimeipata toka Mwanachi.

Jana Spika wa Bunge, Anne Makinda aliitisha mkutano wa waandishi wa habari na kusema: “Siyo kwamba tutaanza kutoa, tulishaanza kutoa na Rais (Jakaya Kikwete), ameshatoa kibali chake na mbunge atalipwa katika vikao tu.

Spika Makinda, jana aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake kwamba wabunge wameshaanza kulipwa posho mpya za Sh200,000 kwa kila kikao kuanzia Bunge lililopita akisema ni baada ya idhini ya Rais.Alisema posho hiyo iko katika waraka wa Serikali kuhusu posho uliotolewa Julai mwaka juzi akisema wenyeviti wanapata Sh200,000, wajumbe Sh150,000 na wengine Sh100,000"

My take:
1. Je, kuna uwezekano kwamba office ya Speaker kwa kushiriakina na office ya waziri mkuu wameamua kuwa posho mpywa zitalipwa with or without signature ya rais? sheria inasemaje kama jibu ni ndiyo?

2. Kuna uwezekano rais ameridhia posho mpya lakini anacheza 'cheupe chekundu' kwa makubaliano na Waziri mkuu ili asionekane mbaya? Binafsi naamini rais hawezi kuwakatalia wabunge wa CCM maana bila wao Ikulu hapatatosha.

3. La muhimu zaidi, kama ikigundulika kuwa kweli rais alibariki posho mpya (either kwa ku-sign yeye binafsi au kwa kumruhusu waziri mkuu a-sign) huku kurugenzi ya mawasiliano ikisema (kwa maandishi) kuwa rais haja-sign posho mpya nani awajibike? rais au waziri mkuu? au wote wawili?

Yes we are! Vinginevyo tukiulizwa "je posho za vikao vya wabunge zimeongezwa?" Tutajibu
vipi?
Wakati wote ni vigumu kutolea maelezo pesa zinazotoka kama RUSHWA!Ni ukweli usiopingika ya kua pesa za posho ilikua HONGO ili wabunge wa CCM na СUF ili wapitishe mswaada mbovu wa marekebisho ya katiba kwa kasi ya ajabu.CCM,SERIKALI,SPIKA,WABUNGE WA CCM NA CUF NA RAIS MWENYEWE JK Wanalielewa hilo hiyo kauli ya Ikulu ni propaganda na usanii wa CCM,JK baada ya kuona reaction ya jamii.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
kuna baadhi ya wabunge walishangaa kuona kuna ongezeko bila ya kuambiwa which means posho zimeongezeka na bila ya rais kusain na madam speaker akitegemea jamaa atasaign

tatizo ni kuwa anna makinda she is stupid she cant msoma jk, jk is smart na anaweza kukuchekea au kuongea na ww kumbe sivyo amanishavyo! yeye aliwaambia waangalie! umeona! so she took it for granted, na ndio maana ukiangalia taarifa ya ikulu ipo wazi kabisa jamani president hajaidhinisha kwa kusain, sasa inabidi huyu mama afunguliwe mashtaka pale kisutu kulipa pesa bila idhini ya president si kama tunavyopelekwa polisi huku kwenye private sector kwa kulipa bila idhini ya mkubwa wako!
 
Hii habari nimeipata toka Mwanachi.

Jana Spika wa Bunge, Anne Makinda aliitisha mkutano wa waandishi wa habari na kusema: "Siyo kwamba tutaanza kutoa, tulishaanza kutoa na Rais (Jakaya Kikwete), ameshatoa kibali chake na mbunge atalipwa katika vikao tu.

Spika Makinda, jana aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake kwamba wabunge wameshaanza kulipwa posho mpya za Sh200,000 kwa kila kikao kuanzia Bunge lililopita akisema ni baada ya idhini ya Rais.Alisema posho hiyo iko katika waraka wa Serikali kuhusu posho uliotolewa Julai mwaka juzi akisema wenyeviti wanapata Sh200,000, wajumbe Sh150,000 na wengine Sh100,000"

My take:
1. Je, kuna uwezekano kwamba office ya Speaker kwa kushiriakina na office ya waziri mkuu wameamua kuwa posho mpywa zitalipwa with or without signature ya rais? sheria inasemaje kama jibu ni ndiyo?

2. Kuna uwezekano rais ameridhia posho mpya lakini anacheza 'cheupe chekundu' kwa makubaliano na Waziri mkuu ili asionekane mbaya? Binafsi naamini rais hawezi kuwakatalia wabunge wa CCM maana bila wao Ikulu hapatatosha.

3. La muhimu zaidi, kama ikigundulika kuwa kweli rais alibariki posho mpya (either kwa ku-sign yeye binafsi au kwa kumruhusu waziri mkuu a-sign) huku kurugenzi ya mawasiliano ikisema (kwa maandishi) kuwa rais haja-sign posho mpya nani awajibike? rais au waziri mkuu? au wote wawili?

Hapa ndipo Raisi wetu anapaswa kuandikiwa barua ya wazi ajieleze kikamilifu na viongozi wake wa serikali wajieleze - wote watoe taarifa kutoa huu utatanishi. Raisi, anahoja ya kujibu hapa!
 
Rais asikatae maana aliwaambia watumie busara baada ya kuona kuna umuhimu wa kuziangalia hizo posho kwa upya. Busara waliyotumia ni hiyo ya kujiongezea. Sasa hapa nani wa kulaumiwa kama sio Rais.

Rais gani asiyekuwa na maamuzi. ok kajua wamejiongezea na yeye hajaidhinisha kwahiyo sasa anatamka nini?
 
Mwanakijiji bwana, wao wenyewe wanakuambia wameishaanza kulipwa toka kikao
cha Bunge kilichopita wewe unauliza kama zimeongezwa tena, au unazungumzia
kuongezwa kutoka TZS 200,000 to TZS 200,000+

Lakini pia naomba kusisitiza kwamba Wabunge wetu wana haki za msingi kabisa
za kuongezana posho kama ambavyo watumishi wengine wa UMA walivyo na haki
kuongezewa maslahi yao ili kukidhi mahitaji yao ya msingi na ziada, kama ambavyo
pia, wafanyabiashara na wakulima wana haki ya kuhakikisha kwamba wanapata
maslahi ya kutosha katika shughuli zao.

Na zaidi, naomba watanzania wote tuwe realistic katika hili na kuacha kupoteza muda
kwa kuwakama wabunge wetu.

Nadhani kitu cha msingi ni kama ongezeko hilo limefanyika kwa mujibu wa taratibu
zilizopo za kuongezana maslahi ndani ya serikali. Hili tulijadili na kama taratibu hazikufuatwa
basi tuzipinge.
 
ukisikia nyoka kakatwa kichwa anakosa uelekeo...hakuna kauli ya mwisho...kama darasa la primary
 
Sheria inakataza hivyo but Sitashangaa, kwani sheria gani zinawataka wezi kurudisha walichoiba?
wakuu, hii ni week ya 4 kati ya 52 za mwaka huu na ya 56 kati ya week 260 za kipindi cha pili cha JK, na safari inazidi kuwa ngumu. Leo gazeti la Mwananchi ni Tsh. 800/-
 
Kwa hili inaonekana hakuna ushiriikiano katika utendaji wa kazi serikalini,kila mtu anakuja na lakwake.....kaz kweli
 
jamani sie wadanganyika jamaa wanashindwa kutujali???
 
Nadhani kitu cha msingi ni kama ongezeko hilo limefanyika kwa mujibu wa taratibu
zilizopo za kuongezana maslahi ndani ya serikali. Hili tulijadili na kama taratibu hazikufuatwa
basi tuzipinge.

Mzee hata kama taratibu zimefuatwa,je,hali ya sasa ya uchumi inaruhusu kutolewa kwa malipo ya aina kwa wabunge? Je,hakuna sehemu (huduma za jamii) ambazo pesa hizi zingepelekwa na kusaidia kuziboresha? Je,kada zote za utumishi wa umma zinapata maslahi ya kuridhisha kama ya hao wabunge? Je,kwa wanayoyafanya wabunge bungeni (output),wanastahili kupata malipo makubwa kama hayo?

Mkuu hayo ndio mambo ya msingi ambayo tunapaswa tujiulize!
 
Jakaya mrisho kikwete hamuhitaji pinda katika safu ya uongozi wake......na hi inatokana na pinda kutokujua majukumu ya kazi zake....sasa hivi jk ameamua kumuadhibu pinda kwa kumuaibisha kwa wananchi kwa kila kitu pinda atakachosema basi ikulu itatoa tamko la kupinga.....kuna mamabo kama matatu ambayo ikulu tayari imeyakanusha mara baada ya kutolewa na pinda...pinda anapaswa kutambua hilo hatakiwi na hajui majukumu yake
 
Kwa hili inaonekana hakuna ushiriikiano katika utendaji wa kazi serikalini,kila mtu anakuja na lakwake.....kaz kweli

Mkuu sio kwa hili tu, serikali ya JK kila mtu ana uamuzi wake. Mwangalie Sitta anavyojibizana na NAhodha wakati wote ni mawaziri
Last time kwenye vikao vya CCM, EL alifunguka juu ya sakata la Richmond ambayo JK alisema haijui, kumbe alishiriki hata kuizuia isifukuzwe, Sakata la Luhanjo na Jairo. Pinda anasema angekuwa na mamlaka angemfukuza kazi, few days anarudishwa ofisini na Luhanjo and Ngeleja anampokea wizarani kwa mbwembwe.

Hii nchi haina serikali ila ina genge la vibaka kama wale Komando yosso wa miaka ile ya 90.
 
Hivi Tanzania hatuna sheria inayomkataza Rais, PM, Speaker kusema uongo chini ya kiapo (To lie under oath).
Kwanini tusitumia sheria hiyo kumfukuza mmojawapo kati ya hao. Maana kwa akili ya kawaida posho haziwezi
kuwa zimesainia au hazijasainia at the same time. Lazima kimojawapo kati ya hivyo lazima kiwe kimfanyika!
Hence mmojawapo atakuwa amesema uongo, either Rais or PM and Spekear
 
Ndipo watakapoona umuhimu wa kuweka makubaliano yote kwa "MAANDISHi" kama madaktari wajanja walivyowaambia.

Nasikitika tu kwamba they will get away with this again.
 
na mimi hii kitu inaniuma sana!!hawa watu wanatufanya sisi hamnazo!!wanatuchezea, ooh bado mara tayari!!nchi hii!!!!!!!!
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom