Yericko Nyerere: Serikali ianzishe customer care service maalum, Wizara ya Habari na Mawasiliano haina manufaa

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,866
Anaandika Yericko Nyerere katika Mitandao yake ya kijamii;

"Nashauri Serikali ianzishe kituo maalumu cha huduma kwa wateja (special customer care) mitandaoni ambacho kitapokea shida na matatizo yote ya watz. Wizara ya Habari na Mawasiliano kinadharia haina manufaa kwa umma, na haina tija ya kuwa Wizara, haisaidii umma kufikia serikali kuu, bali ipo kama room tu ya Serikali kutoa matamko kwa umma sio umma kufikisha sauti zao.

Kwa muda mfupi niliojaribu kupokea matatizo na kero za watz mitandaoni nimebaini Serikali kunzia chini hadi taifa iko mbali na umma, ni watz wachache sana wanaopata huduma za serikali kwa ufanisi na kuridhika na ngazi ya serikali inayomhudumia mtu huyo. Walio wengi hawapati utatuzi wa kero zo kwenye ngazi husika na hivyo wangetamani kuhudumiwa na ngazi za juu zaidi ikiwemo kumuona Rais moja kwa moja.

Nimezunguma na watu mbalimbali, wengi wanaohitaji msaada tayari ngazi flani za kiserikali wameshapita na kushindwa kusaidiwa. Wizara ya Maendeleo ya Jamii kwa nadharia ndio inkabiliana na matatizo mengi ya kijamii lakini wengi wa watu wenye matatizo hayo wanatamani kumfikia Waziri husika au Rais. Wizara ya Ardhi vilevile, Wizara ya mambo ya ndani vivyo hivyo nk.

Serikali ifungue kituo cha wazi cha kupokea matatizo na malalamiko ya umma kupitia mitandao ya kijamii ambacho kitakuwa na uwezo wa HARAKA kuifiki serikali KUU na kutatua tatizo lolote la wananchi."
 
Mimi binafsi kiukweli anachosema Yericko Nyerere naona ni sahihi kwa asilimia nyingi, wananchi wanapitia kero ila hazitatuliwi au hawasikilizwi au kujibiwa kwa ufasaha kulingana na hawa watumishi wa serikali kwenye ofisi za umma, yani wanakumbana na vikwazo ambapo inawagharimu wananchi kutaka kufika moja kwa moja kwa waziri au rais kutatuliwa kero zao...
 
Back
Top Bottom