Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika Kikao Kazi cha 18 cha Maafisa Habari, Uhusiano na Mawasiliano wa Serikali

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akishiriki katika Kikao Kazi cha 18 cha Maafisa Habari, Uhusiano na Mawasiliano wa Serikali kinachofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam, leo Jumatatu Machi 27, 2023.



Tulia Ackson anazungumza:
Maafisa Habari wa Serikali lazima mjipe nafasi ya kutoa habari kwa Wananchi, hilo ndilo jukumu lenu kubwa, mnatakiwa kutoa habari kwa kuwa Wananchi wanahitaji kujua habari na kupata taarifa sahihi.

Mnapokuwa kimya ni rahisi kutoa nafasi ya taarifa potofu kusambaa kwa wengi.

Hali kama hiyo ndiyo ambayo inawapa nafasi Waandishi wa habari kusema kuwa ‘alipotafutwa akazima simu’. Hivyo, inapotokea huna taarifa sema huna na ufanye jitihada za kutafuta.

“Lakini hili pia linawahusu Maafisa Habari wa Bunge, Bungeni tunahitaji taarifa sahihi pia.

“Wewe Afisa Habari ni kazi yako kujua chama kilichopo madarakani kinasema nini, mfano kwa sasa Chama Cha Mapinduzi ndicho kilichoiweka Serikali madarakani mnatakiwa kujua kinachoendelea na wanachokifanya.”


Waziri wa Habari, Mawasiliano wa Teknolojia ya Habari Nape Nnauye anazungumza
Baada ya kikao hiki Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kinatakiwa kianze rasmi kujitegemea na kuendesha mambo yake kama wanavyofanya watu wa vyama vingine, nadhani mmekomaa vya kutosha.

Wizara ya Habari ipo katika hatua za mwisho kukamilisha utayarishaji wa Mkakati wa Taifa wa Mawasiliano ya Umma

Utaainisha utaratibu na upatikanaji wa taarifa kwa umma, pia kuna mkakati wa upatikanaji wa taarifa wakati wa majanga na mkakati wa kujitangaza.

Kama Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa anaingia kwenye vikao vya Baraza la Mawaziri, kwanini mikoani, wilayani na kwenye taasisi maafisa habari wasiwe wanaingia kwenye vikao mada baada ya mkakati huu kukamilika?


TUZO KWA RAIS SAMIA
Nape anaendelea kuhutubia...: Tunakuomba Waziri Mkuu upokee Tuzo ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoka kwa Maafisa Habari wa Serikalini kwa kuimarisha sekta ya habari na Demokrasia Nchini, tuzo hiyo ni kwa mchango wake, tumeacha kufanya kazi kwa hofu.

Tutakapokuwa tayari tutamuomba tukutane naye, tuzungumze naye.

Tunatoa tuzo hii kwa kutambua kazi kubwa aliyoifanya ya Demokrasia Nchini, juzi alienda kwenye tukio lililoandaliwa na CHADEMA, mchango wake katika kuimarisha uwazi, fedha zinakopwa na zinatangazwa hadharani

Tunatambua mchango wake katika kutambua Watanzania wanapata taarifa za ukweli na sahihi, mchango wake katika kurdisha mshikamano furaha na umoja wa Watanzania.

Keshokutwa anakuja Makamu wa Rais wa Marekani, hiyo ni kutokana na kazi nzuri inayofanywa na Rais Samia.

Mwambie tumemwelewa, anaishi anayoyasema kwa vitendo, Watanzania wamemweleza na Dunia imemuelewa.

WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA ANAZUNGUMZA
Rais Samia ndiye alitakiwa akuwa mgeni rasmi lakini amenituma kuja kumuwakilisha.

Matarajio yetu ni kuwa mada zitakazowakilishwa hapa, zitaleta mabadiliko makubwa katika kuzisema taasisi zenu, pia maendeleo yanayopatikana ikiwemo miradi mbalimbali inayofanywa na Serikali ili kuwafikia Wananchi na kupata uelewa wenye tija.

Katika ziara zake kwenye Nchi 41, Rais Samia ameweza kusajili miradi 41 kupitia Kituo cha Uwekezaji yenye thamani ya Dola Miloni 339.2 ambazo pia zimeingia hapa Nchini.

Makatibu Wakuu, Wakurugenzi, Wakuu wa Halmashauri, hakikisheni taasisi zote za Serikali zikamilishe utaratibu wa kuwa na Maafisa Habari.

Naagiza Idara zote za Taasisi za Serikali, ili kuziba mianya iliyojitokeza, tengeni bajeti ya kuhakikisha taarifa katika uzoji wa taarifa unatimizwa, Maafisa Habari wasiachwe nyumba, washirikishwe katika mikakati ya miradi.

Rekebisheni utaratibu wa usafiri kwa wanahabari katika matukio, mfano inatokea katika tukio wanahabari wengi huwa hawana utaratibu wa kutengewa usafiri.

Makatibu Wakuu watengeneze njia ya kuwapa mafunzo na kukutana kama ikivyotokea leo.

Mbona katika taasisi binafsi tunawaona wanatoa taarifa na wanasikika, mfano kwenye michezo kina Ahmed Ally wa Simba, Ali Kamwe wa Yanga, Masau Bwire wa Ruvu mbona tunawasikia, nyie vipi mbona hamsikiki, inamaana mazingora yenu yamebanwa kiasi hicho cha kushindwa kutoa taarifa.

Wizara itawalipia Maafisa Habari wote kwenda kushuhudia mchezo wa Tanzania dhidi ya Uganda kwenye Uwanja wa Mkapa (Jumanne Machi 27. 2023).
 
99.9% ya Maafisa Habari wa Serikalini ( Wizarani, Idarani na katika Manispaa ) hawajui Majukumu yao na wapo wapo ndiyo maana Wakubwa Wao wanatumia Watu Wengine ( Nje ya Mfumo ) katika Kutangaza na Kuelezea Mafanikio na hata Kutuhabarisha Sisi Watu wa Kawaida wakiongozwa nami GENTAMYCINE.

Wabadilike kwakweli.
 
Kazi kazi!!
Sasa confidence, kama waziri mkuu, imemjaa pomoni. Safi kabisa!!
 
Back
Top Bottom