Yericko Nyerere atoa ushauri kwa serikali na TISS zianze kufanya biashara ya taarifa za kijasusi

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,866
Katika mahojiano yaliyofanyika kwenye Channel ya YouTube ya Simulizi Na Sauti (SNS) kati ya Sky Walker, DJ Smaa na Yericko Nyerere. Nguli wa uchambuzi wa mambo ya Siasa na uchumi wa kivita na ujasusi, Yericko Nyerere amesikika akiishauri Serikali ya Tanzania na Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) kuhusu kuanza kufanya biashara ya taarifa za kijasusi kwa ajili ya kujipatia kipato na kununua taarifa muhimu ili kuweka nchi katika nafasi nzuri kwenye biashara hiyo. Kati ya dakika ya 56 hadi 58 ya Video alisikika akisema;
"....Kwanza Dunia imebadilika. Kuna biashara inaitwa biashara ya ujasusi, Duniani. Mataifa ya Uingereza, Marekani, Urusi yanafanya sana biashara ya Ujasusi. Hata vita vya Ukrein, Ukrein hata taarifa za ujasusi alikuwa ananunua kutoka Uingereza, na mpaka leo Uingereza kashikilia tender ya Ujasusi. Kwamba nyie mnataka kupiga wapi, nyie tutakuuzia taarifa. Hata kwenye kitabu hiki wakati naandika nilisema inabidi ifike tubadilike sasa hivi. Tunataka tuone leo idara yetu ya usalama wa taifa inafanya biashara ya ujasusi, ni biashara ambayo hiko halali duniani. Mfano Congo kuna migogoro kila siku, mnafanya nini Tanzania hili kuonesha mnaweza kuingiza kipato kwetu huku. Kuna makundi mengi huko yanapigana, serikali hiko inaangaika kupata taarifa za kijasusi, tumieni watu wetu, tumieni watu wetu tufanye biashara. Hamasi ndio walichokuwa wanakifanya, kwenye vita vya siku sita Urusi ndio walikuwa wanauza taarifa kwa wale jamaa...."
Mahojiano hayo yalijikita katika kuzungumzia vita vinavyoendelea huko Palestina na Israel huku wakigusia vita vya Urusi na Ukrein, na ushawishi wa mataifa mengine katika vita hivyo kwenye nyanja mbalimbali.

Video kamili

View: https://youtu.be/ak3D89O4Gz4?si=tG5SxX8pTElGKfR0
 
Katika mahojiano yaliyofanyika kwenye Channel ya YouTube ya Simulizi Na Sauti (SNS) kati ya Sky Walker, DJ Smaa na Yericko Nyerere. Nguli wa uchambuzi wa mambo ya Siasa na uchumi wa kivita na ujasusi, Yericko Nyerere amesikika akiishauri Serikali ya Tanzania na Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) kuhusu kuanza kufanya biashara ya taarifa za kijasusi kwa ajili ya kujipatia kipato na kununua taarifa muhimu ili kuweka nchi katika nafasi nzuri kwenye biashara hiyo. Kati ya dakika ya 56 hadi 58 ya Video alisikika akisema;

Mahojiano hayo yalijikita katika kuzungumzia vita vinavyoendelea huko Palestina na Israel huku wakigusia vita vya Urusi na Ukrein, na ushawishi wa mataifa mengine katika vita hivyo kwenye nyanja mbalimbali.

Video kamili

View: https://youtu.be/ak3D89O4Gz4?si=tG5SxX8pTElGKfR0

YERICKO mdogo wangu unavuka red-line.
 
Back
Top Bottom