Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,200
- 10,938
Historia huwa inapitia msururu mrefu wa matukio.Yapo matukio ambayo mwanzoni huenekana ni sehemu ya historia nzuri lakini kadri muda unavyokwenda watu hujutia historia hiyo na hatimae kuamua kubadili hisia.
Matukio ya aina hiyo ni kama yale ya utumwa barani Amerika na ukoloni uliofanywa na baadhi ya mataifa kwa mataifa mengine hasa Afrika.Ipo pia historia ya ubaguzi wa rangi kwa Afrika kusini.
Matokeo ya kuzingatia hisroria hizo hatimae hupelelekea baadhi ya jamii na mataifa kuombana msamaha ili maisha yaende kama kawaida.
Jambo la kushangaza mpaka leo Zanzibar na Tanzania kwa ujumla wanasherehekea siku ambapo maelfu ya watu waliuliwa Zanzibar.
Wasimulizi wa historia hizo wanaeleza kwamba lilikuwa ni tukio la kushtukiza na kwamba karibu wote waliouliwa walifanyiwa hivyo hawakuwa na silaha na waliuliwa wakiwa majumbani mwao.Na kwamba kwa ujumla hakukuwa na uhasama baina yao na wale waliokwenda kuwaua.
Mzee Muhammed Said naamini anajua habari hizi kwa undani.