Kipindi cha Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12, 2023 na Mohamed Said, Radio One

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,920
30,263
MOHAMED SAID RADIO ONE KIPINDI CHA MAPINDUZI YA ZANZIBAR 1964 KESHO 12 JANUARY ASUBUHI SAA MBILI
Kichwa cha.habari kinajieleza.
In Shaa Allah...

Nasikia, ‘’Hodi, hodi, hodi.’’

Nafungua nawaona watu wa stesheni moja maarufu sana wako mlangoni pangu wananiambia wamekuja kunihoji kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka wa 1964.

Nikawakaribisha ndani.

Si wageni hawa vijana wameshafika kwangu mara kadhaa kwa kunihoji.
Wananiambia kuwa wangependa wanihoji kuhusu sherehe za mapinduzi.

Akili yangu inajisemeza yenyewe kuhusu hili neno, ‘’sherehe.’’
Sherehe ndani ya msiba.

Mimi kwa haraka sana nikawaambia kuwa suala la mapinduzi ya Zanzibar ni historia inayotakiwa ichukuliwe kwa tahadhari kubwa sana kwani kwangu mimi na kwa wengine si suala la kuchukuliwa kwa sherehe kama wanavyotaka kunihoji.

Nikawaambia kuwa mapinduzi kwa baadhi ya watu huwakumbusha vifo vya ndugu zao siku ya mapinduzi na baada ya mapinduzi.

Historia ya mapinduzi si jambo jepesi kama wanavyolichukulia.
Wale vijana hawakutegemea maneno yale kutoka kwangu.

Nikaona sura zao zina mchanganyiko wa kushangaa na mashtuko.

Nikawaambia, ‘’Mimi baba yangu alikuwa na rafiki zake wawili, Jaha Ubwa na Abdulaziz Twala wanamapinduzi na wana ASP kindakindaki.

Hawa waliuliwa baada ya mapinduzi na baba yangu alikuwa na picha walipiga wote watatu picha hii baba alikuwa ameitundika ukutani nyumbani kwetu.

Baada ya kuuliwa hawa rafiki zake wawili picha ile aliitungua pale pengine kwa uchungu kuwa hakuweza kuitazama ile picha kwa majonzi yaliyokuwa moyoni kwake na pia pengine kwa hofu ya yeye kuogopa asije kuhusishwa na wale watu ‘’wabaya,’’ ambao kwa ubaya wao hukumu yao ilikuwa ni kuuliwa.’’

Niliwaonyesha hawa vijana kitabu cha Dr. Haritht Ghassany, ‘’Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,’’ nikawauliza kama wamepata kusoma kitabu hiki.
Hata kukiona au kukisikia ilikuwa bado.

Niliwaeleza kuwa kitabu kile kina maneno ya yale yaliyotokea Zanzibar wakati wa mapinduzi kutoka kwenye vinywa vya wahusika wenyewe na wengi wao wametangulia mbele ya haki wakiwa na majuto kwa yale ambayo mikono yao imetanguliza.

Nikawaambia wao kama waandishi wajitahidi sana kusoma.

Juu ya haya yote tulifanya kipindi kifupi kuliko kawaida cha mapinduzi lakini yale maswali ambayo naamini walikusudia kuniuliza hawakuniuliza.

Hawakuweza tena kuwa na moyo wa kuniuliza nilikuwa nimewafanulia pazia
kuona upande mwingine wa jukwaa.

May be a cartoon



8Kheri Chomba, Rassanye Rassanye and 6 others
 
MOHAMED SAID RADIO ONE KIPINDI CHA MAPINDUZI YA ZANZIBAR 1964
Kichwa cha.habari kinajieleza.
In Shaa Allah...
Wana bodi, japo tuko kwenye harakati za kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge, kuna swali linanitatiza kuhusu Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, ambapo majibu yake sahihi, pia yanaweza kuwa ni kiashiria tosha cha mshindi wa urais wa Zanzibar, iwapo uchaguzi utakuwa huru na wa haki.

Swali hili lahusu ukweli haswa kuhusu Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 12, 1964, baada ya kuibuka kwa kitabu kingine kiitwacho "Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru"
View attachment 2077603
kilichoandikwa na Mwanazouni wa Zanzibar, Dr. Harith Ghassany, kama kilivyofanyiwa mapitio na mwandishi Mohamed Said kwenye gazeti la Al-Nuur la leo.

Ghasanny anasema kumbe Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yalitekelezwa na askari mamluki wa Kimakonde (Wakata Mkonge) ambao waliongozwa na Mzee Mohamed Omar Mkwawa (Tindo) chini ya Amiri Jeshi wa jeshi la mamluki hao Victor Mkello (RIP). (kumbe amiri jeshi hakuwa Mganda John Okello pekee, bali pia Mkello yumo?!.

Mamluki hao walitumia zana zao za kukatia mkonge, zile sime za makali kuwili, walizisunda kwenye nguo zao za ndani na kusafirishwa kwa mitumbiwi usiku usiku kupitia Kipumbwi. Jee wale mashuhuda wa Mapinduzi yale Matukufu ya Zanzibar, wanayakubali haya?.

Pia mwandishi anamalizia kwa kusema hata mauaji ya Karume, hayakutekelezwa na wapinga Mapinduzi, bali ni miongoni mwa hao hao wanamapinduzi, baada ya kupishana kauli fulani fulani za uendeshaji wa Zanzibar baada ya Mapinduzi.

Nimesoma kitabu cha John Okello kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar,
View attachment 2077618
yeye anasema yake, vitabu kadhaa vya waandishi wazungu wanasema yao, historia tukuka ya Mapinduzi Matukufuya ya Zanzibar nayo nayo inasema kivyake, hivi hakuna any straight line yoyote kuhusu Mapinduzi hayo, ya Zanzibar?.
Jee yalipangwa na nani? Yalitekelezwaje?.
Nini haswa kilichotokea usiku ule wa Januari 11?.
Nani alifanya nini wapi?
Na mwisho tuzungumzie wafaidika wa Mapinduzi hayo Matukufu ya Zanzibar na bila kuwasahau wahanga wa Mapinduzi hayo ambao kwako yatakuwa sio Matukufu, ni kina nani haswa?, na kama kuleta amani na utangamano wa Zanzibar kuhusu Mapinduzi hayo kutahitajika kuundwa kwa Tume ya Ukweli na Upatanisho, "Truth and Reconciliation Commission" ili waliohasimiana kutokana na Mapinduzi hayo, wapatanishwe kwa maslahi mapana ya Zanzibar?.

Majibu ya maswali haya yatasaidia kujua mustakabali wa matokea ya uchaguzi wa Zanzibar kudhirihisha kuwa Wazanzibari ni wamoja, hakuna kundi la walishiriki Mapinduzi ndio wenye uhalali zaidi kuitawala Zanzibar kuliko wasioshiriki, after all kumbe Mapinduzi yenyewe, yametekelezwa na askari mamluki wa Kimakonde, toka mashamba ya mkonge Tanga!.

Pasco
Rejea za Mwandishi huyu kuhusu Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
  1. Miaka 50 Ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Bado Kuna Maswali Bila Majibu -1
  2. Neno "Matukufu" Katika Mapinduzi ya Zanzibar, Lilitoka Wapi, na Yana Utukufu Gani?!,
  3. Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar: Kumbe Waarabu Hawakufukuzwa! Walikimbia Wenyewe - Mzee Sukari
Tarehe kama ya leo 11/01/1964 miaka 60 iliyopita, ndio Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yalifanyika!. Alfajiri ya Tarehe 12 Januari, 1964 ilikuwa ni kutangazwa tuu!.

Nawatakia maadhimisho mema ya miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Paskali
 
Back
Top Bottom