Yanga ndio timu pekee iliyotoa wachezaji wengi kucheza AFCON 2024, timu bora inaendana na usajili bora

Majok majok

JF-Expert Member
Aug 3, 2023
609
1,563
Ni ngumu sana kupenya kwenye vikosi vya timu za taifa kwenda kucheza michuano mikubwa barani afrika, ubora pekee wa mchezaji husika ndio umpelekea kocha kumjumuisha mchezaji kwenye kikosi chake Cha mapambano!

Kwa Tanzania ni klabu moja pekee iliyofanikiwa kupeleka wachezaji wengi kwenye timu za taifa zinazokwenda kushiriki AFCON 2024, ambayo ni yanga!

Na kuitwa kwa wachezaji hao akukuja kwa bahati mbaya bali ni ubora wao ndio umewabeba na si vinginevyo, usajili Bora na wa kisasa uliofanywa na viongozi kwa kuzingatia uweledi ndio chachu kubwa ya mabingwa hao kuendelea kutamba Kwenye medani ya soka kwa sasa!

Wachezaji wafuatao wa yanga wanakwenda kukiwasha AFCON 2024;-

1)Djigui Diarra-Mali
2)Stephen Aziz ki-Burkinafaso
3)Kennedy musonda-Zambia
4)Ibrahim baka-Tanzania
5)Mudathir yahya abbas-Tanzania
6)Metacha mnata-Tanzania
7)bakari nondo mwamnyeto-Tanzania
8)Dicksoni job-Tanzania

Ubora wa timu yako unapimwa pia na makocha tofauti tofauti wa mataifa tofauti na sio sandakarawe, timu Bora inatoa kilicho Bora ni sawa na mkulima akitumia mbegu Bora kwenye kilimo chake basi atavuna mazao Bora vile vile!

YANGA kwa sasa ni alama ya soka la Tanzania mwendo wao sio wa kitoto ni suala la muda tu kukita mizizi yake kwenye soka la Afrika kiujumla!

N;B povu ni ruksa lakini uje na data pia timu yako imetoa wachezaji wangapi wanaokwenda AFCON,
No data no right to speak!
 
Oyaa mbona hujaweka Al ahly na mamelod? Au umepima Kwa clubs za Tanzania tuu?

Hao yanga wamebebwa na stars so far sioni maajabu ya stars wakifika mbali Ila bado tunawaombea
 
Oyaa mbona hujaweka Al ahly na mamelod? Au umepima Kwa clubs za Tanzania tuu?

Hao yanga wamebebwa na stars so far sioni maajabu ya stars wakifika mbali Ila bado tunawaombea
Kwani Simba wameshindwa Nini kubebwa na stars? Kocha awaoni?
 
Kuna watu kazi yenu kuu ni kutafuta furaha ndogo ndogo kupitia vitu vya namna hii.

24/7 ni kusifu Yanga Yako tu? huna kazi za kufanya?

Duhh! Hata kama jamani.

Hivi unataka kusema Yanga imekuwa timu tishio sana na inafahamika duniani kote?.
 
Kuna Yule mgonjwa mwingine anaandika Majina marefu ya utani Kwa Simba simuoni sijui amepona wazimu au Hana bando😄😄😄. Bado kidogo na huyu atapona😂😂.
 
Oyaa mbona hujaweka Al ahly na mamelod? Au umepima Kwa clubs za Tanzania tuu?

Hao yanga wamebebwa na stars so far sioni maajabu ya stars wakifika mbali Ila bado tunawaombea
Ukiondoa wa taifa staz wachezaji wengine wanaotoka ligi kuu ya Tanzania ambao wapo afcon ni musonda, diara, inonga na aziz ki
 
Back
Top Bottom