Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi ya Mbowe na wenzake: Kesi imeahirishwa hadi 28/01/2022, Luteni Denis Urio kuendelea na ushahidi wake

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,115
Habari Wakuu,

Leo tena shahidi wa 12 Denis Urio anaendelea kutoa ushahidi wake kwenye kesi inayomkabili Mbowe na wenzake 3.

Kujua Kesi ilipoishia fungua kiungo hiki: Yaliyojiri katika kesi ya Mbowe 26 Jan 2022. Shahidi wa 12 Luteni Denis Urio kuendelea kutoa ushahidi wake Jan 27, 2022

Fuatana nami kupata yatakayojiri

========

Jaji
ameingia Mahakamani Muda huu Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani Muda huu

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Ikikupendeza naitwa wakili wa Serikali Robert Kidando nipo pamoja na
  • Wakili Pius Hilla
  • Abdallah Chavula
  • Jenitreza Kitali
  • Nassoro Katuga
  • Esther Martin
  • Tulimanywa Majige
  • Ignasi Mwinuka
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja na
  • Wakili Nashon Nkungu
  • John Mallya
  • Dickson Matata
  • Michael Mwangasa
  • Paul Kisabo
  • Seleman Matauka
  • Alex Massaba
  • Maria Mushi
  • Khadija Aaron
  • Evaresta Kisanga
  • Michael Lugina
  • Sisty Aloyce
Jaji anaita Washitakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na tupo na Shahidi Mmoja ambaye Jana Alianza Kutoa Ushahidi Wake, Tupo Tayari Kuendelea

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji na sisi tupo tayari Kuendelea

Jaji nakukumbusha kuwa Jana Ulikuwa Kiapo, na Leo Utaendelea Kuwa Chini ya Kiapo

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Wakili Abdallah Chavula ataendelea Kumuongoza Shahidi

Wakili wa Serikali: Jana tuliishia 12 August 2020, Je Iambie Mahakama Wewe Ulifanya nini

Shahidi: Nilipeleka Simu ambazo sikwenda nazo Kwa Inspector Swila

Wakili wa Serikali: Ulimpeleka Wapi

Shahidi: Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Simu hizo tatu ulizo Mpelekea Inspector Swila Zilikuwa ni Mali ya nani

Shahidi: Zilikuwa ni Mali yangu

Wakili wa Serikali: Simu hizo tatu zilikuwa za aina gani

Shahidi: Tecno C9, Itel na Samsung ndogo ya Tochi

Wakili wa Serikali: Hebu tueleze Sasa nini Kilitokea Ulipofika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi

Shahidi: Baada ya Kufika Nilikutana na Inspector Swila Nikamkabidhi Simu zote, Kwa Kunikabidhi Nyaraka ambayo Niliandika Majina yangu, Ilikuwa ina IMEI namba Baada ya Hapo akaandika Majina yake, nikasaini na Yeye akasaini

Wakili wa Serikali: Kwa Hiyo Jumla Nyaraka Ngapi zilizokabidhiwa

Shahidi: Jumla ni Nyaraka Nne

Wakili wa Serikali: Kwa Siku hiyo ya Tarehe 12 August 2020 ziliandaliwa Nyaraka Ngapi

Shahidi: Nyaraka 3

Wakili wa Serikali: Nani aliziandaa zile Nyaraka

Shahidi: Aliziandaa Inspector Swila, Alinipa nikasaini akazitoa kopi akanikabidhi

Wakili wa Serikali: Shahidi Nikurejeshe Kwenye Nyaraka Iliyoandaliwa Tarehe 11 August 2020, Iliyoandaliwa na Inspector Swila, Ukiona Utaitambuaje?

Shahidi: Nitaitambua Kwa Majina Yangu Matatu, Denis Leo Urio, Nitaitambua Kwa Tarehe Niliyokabidhi ambayo ni Tarehe 11 August 2020, Nitaitambua Kwa Sahihi Yangu

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Kumuonyesha Shahidi Nyaraka aweze Kuitambua

Wakili wa Serikali: Shahidi Hebu Tizama hii Karatasi kwa Makini, halafu Iambie Mahakama Kama Unaifahamu

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Naitambua Nyaraka hii Kwamba Nilisaini Mimi, Kwamba ina Majina yangu Matatu, Ina IMEI namba ya Simu yangu ya Tecno,

Wakili wa Serikali: Majina yako Yapo

Shahidi: Ndiyo Yapo

Wakili wa Serikali: Je Tarehe ipo

Shahidi: Tarehe ipo

Wakili wa Serikali: Ulisema Utaitambua Kwa Sahihi yako, Je Ipo.?

Shahidi: Ndiyo ipo

Wakili wa Serikali: Sasa Ungependa Mahakama Ifanye nini Juu ya hiyo Nyaraka

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Ningependa Mahakama itambue hiyo Nyaraka

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shahidi anaomba itambue Kama Kielelezo

Wakili PETER KIBATALA: OBJECTION Mheshimiwa Jaji Shahidi hajasema Ipokelewe Kama Kielelezo, Bali amesema Anaomba Mahakama itambue Nyaraka

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji sisi ni Maafisa Wa Mahakamani tuna Wajibu wa kusaidia

Jaji: Wakili Kibatala

Kibatala: Mheshimiwa kama Anaomba Kwa ajili ya a Utambuzi Ibakie hivyo

Nashon Nkungu: Mheshimiwa Jaji Kwa sababu Nyaraka anaombwa kwa ajili ya Utambuzi Hatuna Pingamizi

Wakili John Mallya: Mheshimiwa Jaji na Mimi pia sina Pingamizi Juu ya Utambuzi

Wakili Dickson Matata: Mheshimiwa Jaji na Mimi Sina Pingamizi Juu ya Utambuzi

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji na mimi pia Sina Pingamizi Kama Nyaraka Inapokelewa kwa ajili ya Utambuzi Nyaraka Inatoka Benchi la Utetezi Kwenda Katika Meza ya Jaji Pale Juu

Jaji: Naipokea Nyaraka Kama ID namba 2

Mawakili wa pande zote mbili wanakubaliana na Uamuzi Jaji kwa Kusimama na Kumuinamia Kidogo

Wakili wa Serikali: Shahidi Awali Ulieleza Mahakama Kwamba Siku ya Tarehe 11 August 2020 Ulimkabidhi Simu TECNO CAMMON Inspector Swila Shahidi Je Simu hii Ukiona Utaweza Kuitambuaje

Wakili wa Serikali: Kingine kitachokufanya Utambue

Shahidi: Kama Ukiwasha inatoka Picha ya Familia Yangu Kwenye Screen Saver

Wakili wa Serikali: Unaposema picha ya Familia Unamaanisha Nini

Shahidi: Nime save Kwenye Screen Saver Ina Display Picha Ya Mke wangu

Wakili wa Serikali: Kingine

Shahidi: Nikienda Kwenye Program ya Telegram nitakuta Mawasiliano Baina yangu Mimi na Mbowe, Mawasiliano Ya Meseji

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Mahakama itupatie Kielelezo Cha Mashitaka Namba 34

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Kumkabidhi Shahidi Kielelezo hiki, Kwa ajili ya Utambuzi

Wakili wa Serikali: Shahidi Hebu Tazama hii Simu, Jaribu Kuangalia Yale uliyokuwa Unaeleza Mahakama Kama Yapo

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Kwa Mwonekano Wa Nje hii Ndiyo Simu Yangu yenyewe

Wakili wa Serikali: Mwonekano gani Wa Nje

Shahidi: Cover Jeusi Screen protector kupasuka Kwa Juu Simu yenyewe ni TECNO CAMMON

Wakili wa Serikali: Shahidi Vipi Kuhusiana na Yale Mengine

Shahidi: Mpaka niwashe Simu

Kibatala: Hatuna Pingamizi Mheshimiwa Jaji

Shahidi: Hii ndiyo picha ya mke wangu

Wakili wa Serikali: ionyeshe mahakama, mahakama ione

Jaji: Wakili Mallya, ungependa uone picha ya mke wake

Wakili John Mallya: hapana mheshimiwa Jaji, tunateta Jambo jingine kabisa

Shahidi: Mawasiliano yangu ya Ujumbe Mfupi Kati yangu Mimi na Freeman Mbowe haya hapa

Wakili wa Serikali: Hayo Mawasiliano yapo Kwenye nini

Shahidi: Tulikuwa tuna wasiliana Kwa Mfumo wa Telegram

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Wenzetu Wanaomba Kujiridhisha

SIMU ya Shahidi Inapelekwa kwenye Benchi la Utetezi

Wakili Kibatala Anaenda Kwa Shahidi Kizimbani Kuangalia Mawasiliano Ya Telegram Kwenye Simu

Wakili John Malya na Yeye anaomba Kwenda Kizimbani Kwa Shahidi Kushuhudia Mawasiliano ya Telegram ya Simu ya Shahidi

Wakili Dickson Matata Mheshimiwa Jaji namimi naomba Kwenda Kujiridhisha Matata anafika na Kukagua Simu ya Shahidi Bado Wakili Matata Yupo Kizimbani Wakili Nashon Nkungu Na Yeye anaenda Kizimbani Kwa Shahidi Kushuhudia Mawasiliano ya Telegram ya Simu ya Shahidi

Mawakili Wa Serikali Wanateta Kwa Pamoja


Wakili wa Serikali: Shahidi hizo Meseji Ulizo Onyesha Mahakama Unaweza Kuzisoma.?

Shahidi anasoma Meseji July 2020,

Kaka Mtu tatu ni Muhimu sana,

Yes Bro Kuna Members Wawili Mpaka sasa, Mmoja Yupo Tunduma na Mmoja Yupo Dodoma

Security Ni Muhimu Sana, Wasije kutelekezwa, Siwezi Kuwatelekeza..

Naomba Unitumie Nauli ya Kuwa Mobilise Niende nao Moro

Kwa Namba Ipi

Laki 5 inatumwa

Nashukuru Nimepata Usiwe Unatumia Namba yako Binafsi Kutuma, Tumia Watu wengine au Wakala

Wapo Wapi Bro

Nipo nao Njiani

Mkuu Shikamoo Vipi Maendeleo ya mgonjwa wako

Wale Watu wawili nipo nao nasubiri Maelekezo yako

Kaka Nashukuru,

Je wanaweza Kuja Dar Naomba Unitumie Nauli na Dar Wapi watafikia Wanaweza Kuja Dar na Kesho Wakaenda Hai

Nitumie Nauli

Kwa namba ipi

Kwa namba yangu

Usitume Kwa namba yako

Nitatuma Gari ya kuwapokea Ubungo

Namba ninayo watumia ni Ya Dereva Wangu anaitwa Willy yeye Ndiye atakaye Wapokea

Nashukuru Nimepata

Asante Bro Hope Wameondoka

Wawili Wapo Ruvu Wawili bado Uwe unatuma Pesa ya Kutosha ya akuwa Mobilise

Kaka bado Nipo Kamati Kuu,

Tuma Meseji

Shikamoo Kaka Vipi Mgonjwa wako Wale Wapo Tayari Kuondoka

Nilishindwa Kupokea simu yako sababu ya Deshi Deshi Naamini umenielewa,

Shahidi: Mwisho wa Kunukuu

Wakili wa Serikali: Hayo Mawasiliano Uliyokuwa Ukiyasoma Yalikuwa ni Baina ya nani na nani

Shahidi: Ni Baina yangu Mimi na Freeman Mbowe

Wakili wa Serikali: Shahidi Hebu Rejea Meseji ya Kwanza Kusoma

Shahidi: Kaka wale Mtu tatu au Nne ni Muhimu Sana, Siku zimekwisha

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Hao Mtu tatu au Nne Nini hasa a Kilikuwa kinazungumzwa

Shahidi: Nilikuwa Nimeongea naye hapo NYUMA kuhusu Kuwatafuta Khalfani Bwire, Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya na Moses Lijenje Kwamba hata hao waende Siku zinaenda

Wakili wa Serikali: Huo Ujumbe Ulikuwa Unatoka Kwa nani

Shahidi: Unatoka Kwa Freeman Mbowe Kuja Kwangu

Wakili wa Serikali: Nenda Kwenye Meseji ya Saa 2 na Dakika 14 na Sekunde 50

Shahidi: Ya Tarehe ngapi

Wakili wa Serikali: Tarehe 20 July 2020

Shahidi: Mmoja Kazaliwa Mwaka 1980 na Mwingine Kazaliwa mwaka 1986

Wakili wa Serikali: Tarehe hiyo hiyo 30 Mwezi July 2020, Nenda Kwenye Meseji ya Saa 2 na Dakika 2

Shahidi: Bro Kuna Members Wawili Mpaka Saa hizi, Mmoja Yupo Tunduma anahusika na Magari ya kwenda nje na Mwingine yupo Dodoma SGR

Wakili wa Serikali: Huyo aliyepo Tunduma anafanya Kazi ya Kusafirisha Magari Kwenda Nje ni nani

Shahidi: Ni Khalfani Bwire

Wakili wa Serikali: Na Mwingine anaye fanya kazi SGR Dodoma ni nani

Shahidi: Ni Moses Lijenje

Wakili wa Serikali: Ni nani alikuwa kazaliwa Mwaka 1980

Shahidi: Ni Moses Lijenje

Wakili wa Serikali: Ni nani kazaliwa Mwaka 1986

Shahidi: Ni Khalfani Bwire

Wakili wa Serikali: Haya Inayofuata Baada ya hiyo, Isome

Shahidi: Simu Siyo Salama, Niwezeshe niweze Kukutana nao

Wakili wa Serikali: Nani aliandika Hiyo kwenda kwa nani

Shahidi: Niliandika Mimi Kwenda Kwa Freeman Mbowe

Wakili wa Serikali: Ulimaanisha nini Kusema Simu Siyo salama

Shahidi: Simu Siyo Salama, Kum insure Kuwa Hakuna Mtu wa Kut' track

Wakili wa Serikali: Soma Inayofuata

Shahidi: Kikubwa ni Security ya Shughuli zao Wanazofanya Saa hizi, Wasije Kutelekezwa baadae

Wakili wa Serikali: Meseji hiyo ni ya nani

Shahidi: Inatoka Kwangu Kwenda Kwa Freeman Mbowe

Wakili wa Serikali: Shahidi Soma Meseji inayofuata

Shahidi: Hao wawili Kwa kuanzia Siyo Mbaya, Hawawezi Kutekelezwa, Wanakuwa na Mimi Full time, Wamekwambia Wanataka nini.?

Wakili wa Serikali: Meseji hii ilikuwa Imetoka Kwa nani

Shahidi: Imetoka Kwa Freeman Aikael Mbowe

Wakili wa Serikali: Neno hawa Wawili Kuanzia Siyo Mbaya ni akina nani hao

Shahidi: Ni Khalfani Bwire na Moses Lijenje

Wakili wa Serikali: Enheeeee Meseji inayofuata

Shahidi: Sema Tu Kaka nifanyeje

Wakili wa Serikali: Hiyo Meseji Imetoka Kwa nani

Shahidi: Imetoka Kwa Freeman Mbowe

Wakili wa Serikali: Meseji inayofuata

Shahidi: Mmoja kazaliwa Mwaka 1980 na Mwingine Kazaliwa mwaka 1986

Wakili wa Serikali: akiyezaliwa Mwaka 1986 ni nani

Shahidi: Ni Moses Lijenje na Mwaka 1986 ni Khalfani Bwire

Wakili wa Serikali: Soma inayofuata

Shahidi: Naomba Unitumie Nauli ni Mobilise nikutane nao Morogoro

Wakili wa Serikali: Nani hao Uwa Mobilise, na Meseji Imetoka Kwa na nani Kwenda Kwa nani

Shahidi: Meseji Imetoka. Kwangu Kwenda Kwa Freeman Mbowe, Wakukutanao Moro ni Khalfani Bwire na Moses Lijenje

Wakili wa Serikali: Shahidi naKurudisha Nyuma, Kuna a Meseji hao wawili Kuanzia Siyo Mbaya walikuwa wakina nani na Siyo Mbaya ni nini hasa

Shahidi: Alikuwa ni Moses Lijenje na Khalfani Hassan Bwire

Wakili wa Serikali: Meseji inayofuata

Shahidi: Kwani Kiasi gani na Kwa Simu ipi

Wakili wa Serikali: Nani aliandika Hiyo Meseji

Shahidi: Ni Freeman Aikael Mbowe

Wakili wa Serikali: Mlikuwa Mnazungumzia Kiasi cha Nini

Shahidi: Kiasi cha pesa

Wakili wa Serikali: Kwa ajili ya Shughuli gani

Shahidi: Kwa ajili ya nauli ya Kuwachukua Khalfani Bwire na Moses Lijenje Kwenda Kwa Freeman Mbowe

Wakili wa Serikali: Meseji ilikuwa ni ya nani na inaenda kwa nani

Shahidi: Ya Mbowe Kuja Kwangu

Wakili wa Serikali: Soma hapo

Shahidi: Laki 5, 0787 555200

Wakili wa Serikali: Nani aliandika Hiyo Meseji

Shahidi: Mimi Kwenda Kwa Freeman Mbowe

Wakili wa Serikali: Soma Meseji inayofuata

Shahidi: Sawa, Tayari kaka

Wakili wa Serikali: Meseji Imetoka Kwa nani

Shahidi: Imetoka Kwa Freeman Aikael Mbowe

Wakili wa Serikali: Soma Meseji inayofuata

Shahidi: Nashukuru Nimepata

Wakili wa Serikali: hii nayo imeandikwa na nani Kwenda Kwa Nani

Shahidi: Kutoka Kwangu Kwenda Kwa mbowe

Wakili wa Serikali: Tusomee Meseji ya Mwisho Kabisa

Shahidi: Hellow Bro Nilishindwa Kupokea Simu yako Sababu ya Deshi Deshi Deshi naamini Umenielewa

Wakili wa Serikali: Imetoka Kwa nani

Shahidi: Imetoka Kwa Freeman Mbowe Kuja Kwangu

Wakili wa Serikali: Shahidi izime hiyo Simu alafu Irejeshe Mahakamani

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba nirejeshe Kielelezo P34

Wakili wa Serikali: Shahidi Ulimpeleka Simu Kwa Inspector Swila aina ya Techno C9 Je Simu hiyo Ukiona Kipi Kitaku fanya Utambue

Shahidi: Upande wa Kushoto Juu Housing Imepasuka, Ukiwasha haiwezi Kuwaka, Haiwezi Ku Display Kitu, Vilevile Ina rangi Nyeusi

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba nipatiwe Kielelezo P28

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Kwa Ruhusa yako naomba ni Muonyeshe shahidi Kielelezo

Wakili wa Serikali: Shahidi habu itizame hii Simu

Shahidi: Hii ni Simu yangu aina ya Tecno C9, Sababu Nimeitambua Kwenye Housing yake Juu Kushoto imepasuka, halafu Ina Rangi Nyeusi, na Uki switch On haiwezi Kuonyesha

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba kwa Ruhusa ya Mahakama Shahidi aweze Kuiwasha Simu

Shahidi: Haiwaki

Wakili wa Serikali: Shahidi Siku hiyo Tarehe 12 August 2020 kwa Inspector Swila, simu aina ya Itel, Je Utaitambuaje

Shahidi: Mfuniko, Cover ina Rangi Ya Blue Nyuma, Screen Protector Yake Mbele Juu Imepasuka, Ukiwasha itakuwa Na Picha Kwenye Screen Saver Either Mke wangu au Watoto Wangu au Wote

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba tupatiwe Kielelezo namba 33

Wakili wa Serikali: Shahidi Hebu Tizama hii Simu, Tuambie

Shahidi: Nimeitambua hii Simu aina ya Itel, Kama Nilivyosema Kuwa Ina Housing ya Blue na Juu Kwenye Screen Kioo Chake Kimebanduka

Wakili wa Serikali: Shahidi Vilevile Unasema Siku ile ya Tarehe 12 August 2020 kwa Inspector Swila Ulikabidhi Simu aina ya Samsung Je Ukiona Utaitambuaje

Shahidi: Ni simu Ndogo, Samsung ya torch lakini Pia Chini Kwenye eneo la Earphone Kulia Imekatika

Wakili wa Serikali: habu Shika Simu hii, utueleze

Shahidi: Naitambua ndiyo Simu yangu ndogo Samsung ya Torch, nyeupe na lakini Kwenye earphone Plug ni nyeupe

Wakili wa Serikali: Shahidi Hebu tuambie, awali wakati tunakuhoji Uliambia Mahakama Kwamba Ulifahamiana na FREEMAN MBOWE Kuanzia Mwaka 2012 Mpaka Mwaka 2020, Je ilikuwa Ina Maana Gani

Shahidi: Nilikuwa na Maana Kwamba, Baada ya Kuhitaji Vijana Wa kwenda Kuchukua Dola na Kuwapata alikata Mawasiliano na Mimi Kuanzia Tarehe 24 July 2020 alikata Mawasiliano na Mimi

Wakili wa Serikali: Shahidi tuambie Mahusiano yenu Baina yako wewe na Freeman Mbowe Kiujumla yalikuwaje

Shahidi: Yalikuwa ni Mahusiano Mazuri, lakini alikata Mawasiliano na Mimi, Wala sijui kwanini alikata Mawasiliano na Mimi

Wakili wa Serikali: Jumla ya Kiasi gani Cha Fedha Ulicho pokea Kutokana Kwa Freeman Mbowe Uliyokuwa Unapokea Kwa ajili ya Kumpelekea wale Watu

Shahidi: Jumla ni Tsh 699,000

Wakili wa Serikali: Umekuwa Unamtaja Freeman Mbowe Mara Nyingi Sana, Je ukimuona unaweza kumtambua

Shahidi: Ndiyo naweza Kumtambua

Wakili wa Serikali: Sababu ipi itakupekea kumtambua

Shahidi: Body Morphology, anapenda kuvaa miwani, mnene Kiasi na mweusi kiasi

Wakili wa Serikali: Sasa tuambie kama yupo hapa mahakamani

Shahidi: Yule pale kavaa T-shirt, kavaa miwani

Mahakama: Kicheko kwa maana Freeman Mbowe hajavaa miwani leo

Wakili wa Serikali: Shahidi eleza basi, unasema ulipopokea ujumbe kutoka kwa Freeman Mbowe, ujumbe ule wewe ulienda kutolea taarifa kwa Boazi DCI na Ramadhan Kingai, ukiacha hao wawili nani mwingine uliyewahi kumpelekea taarifa hiyo?

Shahidi: Sikuwahi kumpa mtu yoyote taarifa

Wakili wa Serikali: Shahidi Ieleze Mahakama ni Kwanini Hukwenda Kutoa Taarifa Kwa wakubwa wako wa kazi Jeshini

Shahidi: Si kwenda Kutoa Taarifa Kwa wakubwa zangu wa kazi Kwasababu ni Taarifa za Uhalifu, Ndiyo Maana Nilienda Moja kwa Moja Kwa DCI Kwenye Vyombo Vya Uchunguzi

Wakili wa Serikali: Shahidi Iambie Mahakama Ni wakati Gani Ulipeleka Taarifa Kwa Viongozi wako

Shahidi: Nilipeka Taarifa Kwa Viongozi...........

Wakili JOHN MALLYA... Mheshimiwa Jaji hiyo ni Leading Question, Hakuna Sehemu shahidi anasema Kuhusu Viongozi wale

Wakili wa Serikali: Abdallah Chavula Mheshimiwa Jaji Kwa Heshima Zote Labda alikuwa hanifuatilii, Mwanzo Niliuliza Kabla Wakili

JOHN MALYA: bado hajaJibu Hoja

Jaji: Rudia Swali

Wakili wa Serikali: Baada ya Ukamataji Taarifa hizo Ulimwambia nani

Shahidi: Baada ya Ukamataji Taarifa hizo nilimwambia Kiongozi wangu

Wakili wa Serikali: Unaposema Kiongozi Wako Una maanisha nini

Shahidi: Ni Mkuu wa Kikosi ninacho fanyia Kazi cha 92KJ

Wakili wa Serikali: Abdallah Chavula Mheshimiwa Jaji Kwa Upande wetu ni hayo tu Anaketi..

************************************************

Wakili Nashon Nkungu: Nimesikia Mwanzo Unasema Wewe ni Mkristo

Shahidi: Ndiyo

Nashon: Dhehebu gani

Shahidi: Roman Catholic

Nashon: Unasali Wapi

Shahidi: Huko Ngerengere

Nashon: Unasali Jumuiya

Shahidi: sababu Ya Majukumu siudhurii Mara kwa Mara

Nashon: Unafahamu a kwamba Baada ya Kesi hii Unaweza Kutoka Kama shujaa au Mtu asiye na Thamani Duniani

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Nashon: Unafahamu Msemo unaosema Kuwa ni Heri Kufa Jasiri Kuliko Kuishi Katika Utumwa, Unafahamu Kwamba Kesi hii Inafuatiliwa Nchini na Duniani Kote

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Nashon: Unafahamu Kwamba Ukieleza Ukweli yaliyo Nyuma ya Pazia, Hata Jeshi Litakulinda

Shahidi: Ndiyo

Shahidi: Naomba Mheshimiwa Jaji arudie hapo

Nashon: Unafahamu Kwamba Ukieleza Ukweli yaliyo Nyima ya Pazia, Hata Jeshi Litakulinda

Shahidi: Hata sasa Nipo Pamoja na Jeshi

Nashon: Baada ya Kueleza hayo, Naamini Umetafakari Vizuri

Nashon: tuanze hapo Unaposema Jeshi lipo na wewe, Kivipi

Shahidi: Wanafahamu Kuwa nimekuja Kutoa Ushahidi

Nashon: Nikisema Kwamba Hujatoka kazini Kwako Utakataa

Shahidi: Ndiyo Nimetoka Kazini Kwangu

Nashon: Je Unaruhusa au Movement Order

Shahidi: Ndiyo ninayo

Nashon: Unayo hapo Mahakamani

Shahidi: Hapana Nimeiacha Hotelini

Nashon: anaitwa Nani

Shahidi: CO wangu

Nashon: Anaitwa nani

Shahidi: Siwezi Kumtaja hapa Mahakamani

Nashon: kwanini uwezi Kumtaja

Shahidi: Mpaka Nipate Maelekezo Ya Kutaja Viongozi Wa Ulinzi

Nashon: Maelekezo Kutoka kwa nani

Shahidi: Mahakama

Nashon: Mheshimiwa Jaji naomba apewe Ruhusa anitajie

Jaji: Shahidi Kwani Mahakama Imekukataza

Shahidi: Anaitwa Light Keno CJP

Nashon: Twende sehemu nyingine, Je kwa mwaka mnatoa makomandoo wangapi?

Shahidi: Siwezi kusema pia

Nashon: huwezi Kusema kwa sababu hutaki au Kiburi chako tu?

Nashon: Kwa sababu ni Siri

Nashon: Tutajie siri zingine ili tusikuulize

Shahidi: Siwezi kusema

Nashon: Nimesikia Unasema Kwamba Kikosi Chako Cha 92 KJ, Je Kuna kikosi +kingine

Shahidi: Ndiyo

Nashon: Kitaje

Shahidi: Siwezi Kutaja Mambo ya Jeshi

Nashon: Kwanini

Shahidi: Kwa sababu Kesi Inafuatiliwa ndani na Nje ya Nchi na Nina Kiapo

Nashoni: Hapa Umekula Kiapo Kingine

Shahidi: Ndiyo siwezi Kutaja sasa

Nashon: Mheshimiwa Jaji Naomba atutajie

Jaji: Naona Kashasema Hawezi Kusema

Nashon: Haya na wewe kozi yako ya mwisho ya ukomandoo ulifanya lini

Shahidi: Mwaka 2010

Nashon: Kozi zipi ulifanya

Shahidi: SIWEZI KUSEMA

Nashon: Mheshimiwa Jaji naomba Sasa Mahakama, Section 364 ya Sheria ya Ushahidi, Inahusu General Jurisdiction ya Mahakama

Mheshimiwa Jaji ni 264 ya CPA ambayo inasema Mahakama Kuu Itakuwa na Mamlaka, Kuwa Shahidi anapofika Shahidi aweze Kutoa Ushahidi, Na Shahidi amefika

Hataki Kutoa Majibu, Tunaomba Mahakama Yako itoe Mwongozo na pia Imuonye..

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji tunaomba Muda Kidogo tupitie Mahakama Ipo Kimyaaa

Wakili wa Serikali Abdallah Chavula: anasimama Ikupendeze Mheshimiwa Jaji, Tumemsikiliza Wakili Msomi Mwenzetu Wakili Nashon Nkungu, Kwa Heshima Zote Siye hatukubaliani na Maombi yake anayoyataja kwa kuwa hayana Mashiko Kisheria

Mheshimiwa Jaji Wakili anaomba Mahakama Imlazimishe Shahidi Kujibu swali lake la Level gani ya Mafunzo aliyo yafanya, Shahidi amemueleza hilo Suala la Siri Hawezi Kutamka hadharani Yeye ni Wa level gani Katika fani yake

Na Wakili kabla ya hapo amekuwa aliuliza Maswali Kadhaa kuhusu Ikama ya Jeshi la Tanzania, Shahidi amemueleza Kwamba hawezi Kueleza Kutokana na Kiapo Chake

Ameeleza Pia Kuhusu Kifungu Cha 264 cha Criminal Procedure Act, Ambapo Wakili anasema Mahakama Inaweza Kumlazimisha Shahidi Kupitia Kifungu hiki, Naomba Nikisome.......... Anakisoma...

Tafsiri ipo wazi Hapa, Kwamba Subject to the Provision of this Act...... Maana yake description Ya Mahakama Katika hili Inategemea na Sheria zingine. Masuala ya kiushahidi, Kupokelewa Kwa Ushahidi Mahakamani Kuna Sura yake Maalum ambayo ni Sura Ya 6 ya Sheria ya Ushahidi ya 2019

Na Sheria hiyo Ina vifungu Mahususi Kinacho Elekeza ni Mazingira Yepi Shahidi anaanza Kulazimishwa Na Mahakama Kujibu Swali.. Mhe Jaji Kifungu Cha 158 cha Sheria hiyo kimeeeleza Ni wakati gani Mahakama, na Mazingira Yepi hasa Mahakama Inaweza Kumlazimisha Shahidi Ajibu Swali

Na si hicho tu, lakini hata Kifungu cha 156 Cha Sheria hiyo hiyo nacho Kinatoa Mazingira Yepi,, Mheshimiwa Jaji Mimi nitajielekeza Kifungu cha 155 Kifungu Kidogo Cha Kwanza....... Nanukuuu

Mheshimiwa Jaji Swali la level ya Mafunzo ya Shahidi Ni swali ambalo halina Mahusiano na Kinacho Jadiliwa Mbele ya Mahakama au Kilichopo Mbele ya Mahakama

Mheshimiwa Jaji Maswala ya namna hii, labda yawe yanapelekea Ku Injure character ya witness basi Shahidi anaweza Kulazimishwa Kuyajibu. Kinyume na hapo Shahidi hawezi Kulazimishwa

Mhe Jaji, Wakili hajaonyesha Mahakama Lengo la suala lake la Kufahamu Mafunzo ya Shahidi Ni Ku' Injure Character yake. Suala la Forces inatoa Makomandoo Wangapi, Force Ina vituo Vingapi Vya Makomandoo, Ni Maoni yetu Maswali ya Namna hiyo hayalengi Ku Distort Character Ya Shahidi

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji siysi tunachokiona hapa Inawezekana msomi ameshindwa kumtingisha Shahidi, Anataka kumlazimisha shahidi azungumze masuala ya ikama ya jeshi..

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Samahani ukisoma Kifungu Cha 155 Sura ya 6, kinasema.. Anasoma..

Wakili wa Serikali: Hata Maswali Yenyewe haya follow under 155, Untest Velacity Ya Shahidi Kwa Kutaka Kufahamu Kuna Vituo Vingapi Vya Makomando, Unatest Velacity ya shahidi Kutaka Kujua Mafunzo yake ni ya level gani, Unatest Velacity Kwa Kutaka Kujua Makomando Wanazlishwa Kwa Mwaka Mara ngapi

Wakili wa Serikali: Shahidi amekuja Mahakamani Kwa Kusema Yeye ni Askari Wa Jeshi la Wananchi, Kutoka Kikosi cha 92 KJ, Cheo Chake ni Luteni na Jukumu lake anasimama Askari Walio Chini yake 30..

Shahidi amekuja Kutoa Ushahidi Kwa Kile Kilichopekea Kesi Hii Kuwapo Mahakamani, Katika Ushahidi Wake Hakuna Mahala ameeleza Kwamba Jeshi La Wananchi Tanzania lilihusika Kwa namna Yoyote Ile

Wakili wa Serikali: Sasa Mheshimiwa Jaji Katika Mazingira hayo, Utaona Maswali la Wakili hayana Relevance, Hata Ukiangalia Kwa Namna Yoyote Ile haya Affect Character Ya Shahidi..

Baada ya maelezo hayo marefu kutoka kwa Wakili wa Serikali Abdallah Chavula, mawakili wa serikali wametana wote na wanajadiliana kwa dakika kadhaa...

Anaendelea

Wakili wa Serikali: Wakili wa Serikali Kwa hiyo Mheshimiwa Jaji Kwa Heshima Zote Hoja ya Wenzetu haina Msingi, ajielekeze Katika Masuala ambayo anaweza Kutest Velacity ya Shahidi.. Ni Hoja yetu Kwamba Shahidi Yupo sahihi..

Kwa namna ambayo Maswali yameulizwa Mahakama haina Mamlaka ya Kumlazimisha Shahidi ayajibu kamwe... Mheshimiwa Jaji naomba nimkaribishe Mwenzangu Pius Hilla aendelee

Wakili wa Serikali: Hata Kama angejielekeza Mahakama Katika Utaratibu Huu, haingefaa, Na Mahakama Haiwezi Kujiwekea Utaratibu Wake Pale ambapo Kuna Utaratibu Uliowekwa Kisheria..

Jaji: karibu, Bila Kurudia Kile ambacho amezungumza Mwenzako..

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji nitajitahidi Kuwa Brief Mheshimiwa Jaji Shahidi aliyepo Kizimbani aliulizwa swali Kuhusiana na level yake Ya Ukomando, haaieleza Mahakama Kwamba Kwa Kiapo Chake

Hawezi Kueleza level ya Mafunzo yake. Mheshimiwa Jaji tunakazia Maneno Kwa Kiapo chake Mheshimiwa Jaji ni kosa LA Jinai Ku' Communicate Information ambayo ni Confidential Mhe Jaji sect 4(1) ya CAP 47 ya National Security, Inasema Ni Kosa la Jinai Ku Communicate Information

Na hauruhusiwi Kufanya hivyo, Kwakuwa Shahidi amesha eleza Kwa Kiapo Chake Harusiwi Ku Communicate Kwa Kiapo Chake Kusema Level ya Mafunzo ambayo amefanya, Kuna Maswali ambayo Shahidi anaweza Kujibu na mengine hatakiwi Kujibu.

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji nimalizie Kwa Kusema Kwamba Taarifa Ya Kuhusiana na Level Ya Ukomando wa shahidi Kwa Mujibu wa Kiapo Chake hawezi Kusema.. Na Kwa kuwa Kuna Backup Ya Sheria, Remedy siyo Kulazimishwa, Bali wakili aelekezwe Wakili Kuuliza Maswali Sahihi

Mheshimiwa Jaji naomba Mahakama Itupilie Mbali Maombi ya wakili (Nashon Nkungu)

Wakili Nashon Nkungu: Mheshimiwa Jaji, it's Very Interesting, Leo nimeshuhudia OBJECTION Ya kupinga Identification ya Shahidi, Kama Nilikuwa namuuliza Shahidi ana Elimu gani........

Anakatishwa na Objection..

Wakili wa Serikali Pius Hilla: OBJECTION Mheshimiwa Jaji Samahani, Hakuna suala la Identification ya Shahidi, Kilichopo hapa Ni Kutaja Kumlazimisha Shahidi Kusema Mambo ambayo hawezi Kusema..

Nashon Nkungu: Mheshimiwa Jaji, Niendelee Kwenye Submission yangu, Naomba Mahakama Kwa Wivu Mkubwa Mahakama ilinde Mamlaka yake, Hapa shahidi amekula Kiapo Kimoja, la sivyo Mwanzoni Wakati wa Kiapo angesema anakula Kiapo Lakini anakiapo Kingine kinamkataza Kusema Yeye ni nani

Sisi tunaomba Kiapo alichokula hapa Mahakamani Kiwe Juu Ya Viapo Vingine Vyote, Hakuna Sheria ambayo Wametoa Kwamba Inakataza, Bali Tunaona Kwamba Ni Vifungu Vinavyoruhusu Kujua Shahidi Ni nani Na Elimu yake ni Ipi..

Mheshimiwa Jaji Nikienda Kwa Section Moja Moja Kama ambavyo imetajwa hapa, Naona Vyote ni Permissive, Vyote ni Relevant kwa Sababu Lengo lake Ni Kutaka Ku Establish Je ana ujuzi Wa Kile anachokiongea, anatoka Kweli Ngerengere?

Hatuoni kwa namna Gani suala Hilo lina kuwa Relevant, Mheshimiwa Jaji Kiusalama Hakuna Mambo ambayo yanakiuka, Hatuoni Shida Kusema Mtu fulani na Kusema Yeye ni nani, Wamekuja Hapa Watu Wakasema Wao Nia Inspector, Wao ni Ma RCO

Nashon: Mheshimiwa Jaji Hizo Section ambazo wame zitaja Zina refers Kwenye Kifungu cha 151.. Kwamba Hapatakuwa na Excuse Juu ya Kutoa Ushahidi.. Tunahitaji accuracy, Tunahitaji Conformity, Kwa sababu Watakuja Hata Washtakiwa Watasema wao Wana Kiapo..

Nashon Nkungu: Kuna msemo mmoja unasema "Muosha huoshwa", Mahakama hii hii Wakili aliyesimama Abdallah Chavula ndiye aliyesimama kuhoji mashahidi Wakina Adamoo kwamba komandoo mmoja anapiga askari wangapi.. Hatuku' Object, tulimuacha aulize Maswali yake hapa..

Tunaomba Haki iwe pande zote Mbili, Mheshimiwa Jaji Kwenye kutumia Kifungu Sahihi au siyo Sahihi, Ni Kifungu ambacho tunaona ni sahihi...

Nashon: Kuhusiana na Powers Kuhusu Ku' Compel Shahidi, Kwa Kuweka hii Hoja Vizuri Mahakama Kwa Kutumia hivi Vifungu Vya 141, 156, 155, 158 Vyote ni Vifungu Wezeshi ambavyo vinaipa Mahakama Mamlaka Wajibu wa Kutoa Ushahidi

Nashon: Kama Hakuna Kifungu Kinachokataza, Ni Msimamo Wetu Kwamba Shahidi Yupo Compellable Kuweza Kujibu.. Mheshimiwa Jaji Kwenye Hoja Nyingine Kwenye 158 cha Sheria ya Ushahidi Kifungu Kipo Subject kwenye Subsection Two ya 158 ya Sheria ya Ushahidi

Narudia Kumuomba Shahidi ajibu swali langu Kama alivyoulizwa

Wakili Nashon Nkungu: Anakaa Chini Mahakama Ipo Kimya Kidogo

Jaji: Mme' site sheria kadhaa na vifungu kadhaa, Ili niweze kutoa maamuzi ambayo ni sahihi naomba kupitia kidogo hivi, kwa dakika 30 kisha tutarejea..

Jaji anatoka..

======

Jaji ametoa taarifa kuwa kesi itaendelea saa 8 na nusu...

=======

Jaji amerejea Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani


Wakili wa Serikali Robert Kidando: Kwa Upande wetu tupo Kama Awali na tupo tayari Kuendelea

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Kwa Upande wetu tupo Kama Awali Hakuna Mabadiriko, na Tupo tayari Kupokea Uamuzi Mdogo na Cross examination

Jaji: Wakati Uliopoita Mahakama Ilitoa Hairisho la Muda Kufuatia Hoja Iliyo letwa na Wakili Nashon Nkungu.. Hoja Ilikuja baada ya Upande Wa Mashtaka Kumalizia Kumuuliza Maswali Shahidi Ndipo Bwana Nkungu akapokea na Kuuliza Maswali

Ndipo Baada Ya Maswali Kadhaa a Shahidi alisita Kujibu Kwa Kusema Kwamba awezi Kujibu Maswali Kadhaa, Kwamba Yupo Mtu anaye weza Kuzungumzia

Moja ya Swali ni Kikosi Vipi ambavyo Vinafunisha Makomandoo, Aeleze Mafunzo aliyofikia Level yake ya Ukomandoo.. Ambapo Shahidi alisema hawezi Kujibu.. Ndipo wakili Nashon Nkungu akaomba Mahakama Imlazimishe Shahidi Ajibu Maswali Kwa sababu Mahakama ina Mamlaka hiyo

Upande wa Mashitaka Walipinga Hoja hiyo Kwa Kusema Kwamba Kwanza Kifungu Kilochotumiwa Kuleta Ombi hilo Kimekosewa.. Wakataja Kifungu Namba 158 na 156 kwa Kueleza Vifungu ambavyo Vina eleza kwamba ni Mazingira Yap Shahidi anaweza Kulazimishwa Kutoa Ushahidi..

Kwa Mazingira haya Jambo hilo halipo.. Shahidi ameulizwa Na ameshasema Kwamba Yeye ni Komandoo na Kwamba Yeye ana jukumu la Kuongoza Afisa Mmoja na Askari Kadhaa.. Wakaendelea Kusema Katika Mazingira Hayo Mahakama Imkatalie Kumlazimisha Shahidi

Upande Wa Mashitaka Waliendelea Kusema Kuwa Shahidi amesha Ulizwa ana akasema anakatazwa kwa Mujibu wa Sheria ya usalama wa Taifa na Kwamba Kwa Mujibu wa Sheria hiyo Mtu anakatazwa Kutoa Siri au Taarifa anazokatazwa..

Wakasema Kuwa Shahidi asilazimishwe.. Kwamba Remedy Siyo Kumlazimisha Shahidi Bali Wakili aelekezwe Kwenda Katika Eneo Lingine.

Wakili Nashon Nkungu akasema Kwamba Vifungu Vyote Vya 158,155 na 156 ni Vifungu Muafaka na Kwamba akaomba Mahakama Itumie hivyo Vifungu Kujibu swali lake.. Akasema Kwamba Sheria inasema Kuwa Shahidi hatoachwa Bila Kuulizwa Swali

Na Kwamba Shahidi amekula Kiapo hapa Mahakamani, na Hakusema Kwamba ana kiapo Kingine, Na akaomba Shahidi Ajibu swali lake..

Jaji: Jaji Ni Walikubalina na Wakili Nashon Nkungu Kwamba Kifungu Cha 264 Kinatoa Mamlaka ya Jumla Juu ya Mahakama Juu kuendesha Shughuli zake.. Kifungu hiki hakitoi Mamlaka Kwamba ni Kwa namna gani Mahakama Itamlazimisha Shahidi Kujibu Swali lake

Kwa Mujibu Wa Kesi Mbalimbali, Hoja Kwamba Sheria ambayo Maombi yameletwa Kwamba Sheria SIYO Muafaka basi Maombi yatupwe Siyo Muafaka, Basi Mahakama Inaendelea Kusikiliza.. Wao Wenyewe Wameieleleza Mahakama Vizuri Katika Vifungu ambavyo anaweza kutumia

Kifungu Cha 151 kinasema Shahidi hatoachwa Bila Kujibu swali Lolote Kama swali hilo ni Relevant Na Kesi hiyo.. Mahakama Inatakiwa Kuhakikisha Shahidi anajibu Swali hilo Moja kwa Moja ambapo Swali hilo Linabishaniwa Mahakamani..

Kifungu Namba 155 kinasema Shahidi anaweza Kuulizwa Maswali Yoyote, ambayo Yanalenga Kutest Velacity Yake, Ambapo Pia Kama Maswali ambayo siyo Relevant Kama Kutaka Kumtambua Yeye ni nani au Kutaka Kumtikisa Ushahidi wake

Kifungu 156 kinasema Maswali yote ambayo Yanaulizwa katika Kifungu Cha 156.. Kifungu Namba 158 kinaelekeza Kwamba Maswali ambayo yanaelekeza Mahakamani yawe ni Relevant Au Maswal hayo Mahakama Italazimika Kujibu kwa Msingi..

Jaji: Kitu Cha Msingi Ni swali Kama Lipo relevant.. Jambo la Pili Kutest Velacity Yake. Jambo la Tatu Kutaka Kujua yeye Ni Nani. Na la Nne ni Kutaka Kumtikisa.

Suala ambalo lipo Mahakamani Ni Swali ambalo linataka Kujua Shahidi Ni nani, Ni kweli Swali siyo Relevant Ila linalemga Kujua Shahidi yeye ni nani... Katika Mazingira ya Shauri hili ambalo linalemga Kutaka Kujua Shahidi Yeye Binafsi ni nani, Basi Mahakama Inaona anaweza Kujibu

Kama Maswali Mengine yataendelea Nje ya Mipaka basi anaweza Kuzuiwa Kujibu swali.. Nafahamu Kama Yapo Maswali kuhusu Jeshi hawezi Kujibu Basi Nita Elekeza kuwa Asijibu.. Katika Mazingira haya basi Swali ambalo Shahidi Unaulizwa Kuhusu Mazingira Yako unapaswa Kujibu

Jaji: Lakini Kama utaulizwa kuhusu mitaala ya mafunzo yako au vitu ambavyo wewe siyo mhusika unaweza kusita kujibu.. Kwa maana hiyo natoa AMRI, utajibu swali uliloulizwa.

----------


Wakili Nashon Nkungu: Shahidi Unakumbuka Swali nililokuuliza

Shahidi: Sikumbuki

Nashon: Nakuuliza Level ya Mafunzo Yako ni Ipi

Shahidi: Kimyaaaaaaaa

Nashon: Nakuuliza tena, Level ya Mafunzo Yako ni Ipi

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Kwa Sababu nipo Chini ya Kiapo Cha Mwajiri Wangu, Mafunzo ya Kijeshi itakuwa ni Shida Kwangu, Naomba Mwajiri Wangu, Nisije kutoka hapa Nikapelekwa Court Marshall

Jaji:Jibu swali Bila kumuathiri Mwajiri Wako Sasa

Shahidi: Nilifanya Mafunzo Ya Advanced Parachute niliopata South Africa

Shahidi: Pia Ina Certificate Of Diesel Engine

Nashon: Ulipata wapi

Shahidi: Moshi

Nashon: Ulisoma lini

Shahidi: Mwaka 2000 pale RVTCS

Nashon: Kabla ya hapo ulikuwa na Elimu gani

Shahidi: Form Four

Nashon: Unaweza Kueleza Namna Ulivyo ingia Jeshi Mpaka Ukapata Cheo Cha Luteni

Shahidi: Nimeingia Jeshini Mwaka 2003, Ni kafanya Kozi ya Basic, 2004 Basic Komando, 2005 Mpaka 2006 nikasa Advanced Komandoo. 2009 Mpaka 2010 Nikaenda Special Operation

Nashon: Unakumbuka Ulisema Mwaka 2011 kwenye Operation Sudani

Shahidi: Ndiyo

Nashon: Unaweza Kukumbuka Askari Yoyote Uliyekuwa naye Huko Sudan

Shahidi: Siwezi Kukumbuka

Nashon: Je Unakumbuka Askari Yoyote Wa Tanzania aliyekuwa Sudan

Shahidi: Siwezi Kukumbuka

Nashon: Jibu lako Pia litakuwa hivyo Kwa Operation ya 2012 Kwamba hukumbuki Jina la Mtanzania yoyote?

Shahidi: Siwezi Kukumbuka

Nashon: Mwaka 2019 Wakati Khalfani Bwire anafukuzwa Wewe hukuwepo Ulikuwa Sudan

Shahidi: sahihi

Nashon: Na Adamoo Wakati anafukuzwa kazi Pia Hukuwepo Ulikuwa Kozi Arusha

Shahidi: sahihi

Nashon: Pia wakati Mohammed Ling'wenya Anafukuzwa Kazi Pia wewe Hukuwepo

Shahidi: sahihi

Nashon: Kwanini Uliongelea Kuhusu Kufukuzwa Kwao Wakati wewe hufahamu kwa sababu Ulikuwa na Nia Ovu Dhidi Ya Washtakiwa?

Shahidi: Siyo Sahihi

Nashon: Lakini ni sahihi Kwamba Wewe hufahamu Kuhusiana Kufukuzwa Kwao Jeshini, Na Tuhuma zao

Shahidi: Nafahamu ni Utovu Wa Nidhamu

Nashon: Ni sahihi Kwamba Utovu wa Nidhamu Lenyewe Siyo Kosa Ila Ndani yake ndiyo Kuna Kosa Sahihi

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Kwa hiyo Specifically hujaiambia Mahakama Kwamba Khalfani Bwire alifukuzwa Kwa Kosa gani

Shahidi: Siyo Wajibu Wangu Kusema hilo, Ni Wajibu Wa Msemaji Wa Jeshi

Nashon: Kwa hiyo Siyo Wajibu wako pia Kwa Mtuhumiwa Wa Pili na watatu

Shahidi: Miye Nimeishia Kusema Utovu wa Nidhamu, Mengine Ni Siri zao

Nashon: Ni sahihi Ujataja Pia Mahakama Iliyotumika kuwasikiliza na Kuwafukuza Kazi watu hawa Jeshini

Shahidi: Sijaeleza Ndiyo

Nashon: Na wala Ujaeleza Kuwa aliye Wafukuza ni Service Kamanda wao au Tribunal Court Marshall

Shahidi: Sifahamu

Nashon: Na wala Ujaeleza Mahakama Tarehe Waliyo Fukuzwa

Shahidi: Ndiyo Sifahamu

Nashon: Ni kweli hukumtajia Jaji Jina la Admin officer aliyekutajia hawa Kufukuzwa Kazi

Shahidi: Mh Jaji Naweza Kutoa Maelezo

Nashon: Hakuna cha maelezo huu ni muda wa maswali mafupi

Nashon: Ni kweli hukumtajia Jaji Jina la Admin officer aliyekujia Hawa Kufukuzwa Kazi

Shahidi: Ndiyo Sikutaja

Nashon: Na ni kweli Ujamwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Huyo Admin Officer ni Mmoja au Watu tofauti

Shahidi: Umenisikia Vibaya Nilisema Nilienda Ofisini Nikapitia File

Nashon: Ni Ushahidi Wako Ulipitia File

Shahidi: Ndiyo

Nashon: ilikuwa Tarehe ngapi

Shahidi: Sikumbuki

Nashon: Lilikuwa ni Faili namba Ngapi

Shahidi: Sikumbuki

Nashon: Ni wazi Kwamba Uwezi Kusema alifukuzwa Kazi na Chombo Kipi

Shahidi: Walifukuzwa kazi na Mwajiri Wao

Nashon: Kwani Shahidi Unafahamu Kwamba Ili Askari afukuzwe Kazi anatakiwa apitie Procedure Zipi

Shahidi: Sifahamu

Nashon: Turudi Kwenye Ile Siku ambayo Ulikutana na Mheshimiwa Freeman Mbowe ambapo alikutafuta Kwa Njia ya Simu na Baadae Mkakutana Kwenye Mgahawa

Unakumbuka Baada ya Kukueleza Mipango Yake Ya Kuchukua Nchi na Ugaidi, Ukasema Ulitafakari na Ukakubali

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Je Wakati huo Ulikuwa Upo Sober na Malta Yako au Ulibadiri kinywaji

Shahidi: Ilikuwa Kwenye Mgahawa siyo Sober, Sijui Kama Palikuwa panaitwa sober

Jaji: Wakili Uliza Katika Namna Rahisi ambayo Shahidi atakuelewa

Nashon: Nakuuliza Ulikuwa Timamu Kiakili au Ulitumia Kilevi

Shahidi: Nilikuwa timamu

Nashon: Muda unaosema Ulikuwa smart Sana na Ukakubali, Si Ulikuwa hujawasiliana na Chombo Chochote cha Ulinzi Kuhusiana na hiki Kikao?

Shahidi: Ilikuwa Bado

Nashon: Nikiwaambia Kwamba Kwa wewe Kukaa Kile kikao na KUZUNGUMZIA Masuala ya Ugaidi, Utakuwa Ulikuwa Umeshiriki Kikao cha Kigaidi

Shahidi: Sitakubali

Nashon: Ulikubali Kwenda Kumtafutia Vijana, Kwa sababu Ulikuwa na Uchu wa Madaraka

Shahidi: Siyo Kweli

Nashon: Lakini Ulihaidiwa Cheo

Shahidi: Nilihaidiwa Cheo

Nashon: Kuna Kitu Kinaitwa Chain Of Information Jeshini

Shahidi: aaahhh! Kinaitwa Chain Of Command

Shahidi: Ni Mtiririko Wa Amri Kutoka Mtu Wa Juu Mpaka Chini

Nashon: Ulisema Kwamba Ulitoka Mgulani na Ukarudi Mgulani

Shahidi: Ndiyo ni sahihi

Nashon: Jeshini unafahamu Mtu anaitwa Intelligence Officer

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Nashon: Kikanuni Taarifa Kama hizo Ulitakiwa Kupeleka Kwa Intelligence Officer, Admin Officer au Mkuu wa Kikosi

Shahidi: Siyo Sahihi

Nashon: Ni sahihi Hukupelekaa Taarifa Hizo Jeshini Kwa Sababu uwaamini

Shahidi: Hapana ni Kwa sababu, Taarifa zilikuwa zinahusika na Raia

Nashon: Kwahiyo Wewe Ulikuwa Raia

Shahidi: Ni Askari siyo Raia

Nashon: Ni sahihi Kwamba Ushahidi Wako Kuwa Uwezi Kupeleka Taarifa Hizo Kwa Intelligence Officer

Shahidi: Hapana Si Kweli, Sema Nilifanya Analysis Ya Threat

Nashon: Kwahiyo wewe Ulibunja Chain of Command Kwa sababu Unaharaka

Shahidi: Sikweli

Nashon: Tukio Kubwa la wewe Kwenda kwa DCI Ilikuwa Tarehe ngapi

Shahidi: Sikumbuki Tarehe, Ilikuwa katikati ya Mwezi Wa Saba

Nashon: Kwa hiyo hufahamu Tarehe ngapi

Shahidi: Tarehe Kamili sikumbuki

Nashon: Unafahamu Kwamba Unapoenda Kwenye Ofisi za Umma Unaandikisha

Shahidi: Nilichofanya ni Kutoa Kitambulisho Wakanitambua na Tayari Nilikuwa na Appointment na DCI

Nashon: Umeeleza Kwamba Freeman Mbowe alikueleza Kwamba Wanataka Kuchukua Dola Kwa Namna yoyote ile

Shahidi: Ndiyo

Nashon: Alikwambia Watachukua bila Uchaguzi?

Shahidi: Sifahamu, Hakuniambia Watachukua Kwa Namna gani

Nashon: Alikwambia Watachukua Dola Kwa kukata Miti

Shahidi: Hayo yalikuwa Matendo ya Kuleta Taharuki

Nashon: Kwa Uelewa Wako hayo Yakitokea Upinzani Wanachukua Nchi?

Shahidi: Sifahamu sasa yeye

Nashon: Kipi Kitaku %wa sahihi Kulingana na Habari Yako, Mbowe Kuchukua Wanajeshi Ex Soldiers au Wanajeshi Ambao Wapo Kazini katika Kuchukua Nchi

Shahidi: Sijui

Wakili wa Serikali: Abdallah Mheshimiwa Jaji Pamoja na Shahidi Katoa Majibu, lakini linataka Opinion zake

Nashon: Shahidi Unasema Baadae Ulianza Kuwatafuta Vijana ambao Freeman Mbowe anatafuta Walinzi na Kama Wapo Tayari

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Wakati Huo Wewe Ulikuwa Unafahamu Kuwa Mbowe Haitaji Vijana Wa Ulinzi Bali Vijana Wa Kufanya Ugaidi

Shahidi: Ni Vijana Wa Kuambatana naye Kufanya Ugaidi

Nashon: Wakati ule unampigia unamuuliza upo tayari kuna kazi ya ulinzi, wewe moyoni ulikuwa unajua kuwa haitaji walinzi bali ni vijana wa kuambatana naye?

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Kwa hiyo ni sahihi uliwadanganya pia watuhumiwa wa pili na watatu?

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: kwanini Uliwadanganya?

Shahidi: sikuwadanganya, Isipokuwaaaa....

Nashon: Tuliaa... Huko bado sijafika

Nashon: Kama Uliwaambia Kitu ambacho halikuwa Kweli na Sahihi, Inawezekana Hata Leo unaidanganya Mahakama

Shahidi: Sivyo

Nashon: Shahidi Ulisema Kwamba Ulikutana na Watuhumiwa Wa Kwanza na Wa pili na watatu Morogoro, Ni sahihi

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: katika hichi Kikao Chenu Morogoro Hakutaja Ugaidi Wala Kikao Chenu Hakikuwa na Nia mbaya

Shahidi: Kimyaaaaaaaa

Nashon: Hebu tuisaidie Mahakama, Unafahamu Muda wowote Mwingine Mtuhumiwa Wa Kwanza, Wapili, watatu na wanne Walikutana Morogoro Kwa ajili ya Kula Njama Hizo

Shahidi: Sifahamu

Nashon: Kwa hiyo, Vipi Kuhusu Moshi, Unafahamu Kwamba Walikutana Aishi Hotel Moshi Wakala Njama Kufanya Njama Hizo

Shahidi: Sifahamu

Nashon: Unafahamu Kwamba Walikutana Arusha Wakapanga Mikakati ya Kupanga Mipango ya Ugaidi

Shahidi: Sifahamu

Nashon: Kwani Shahidi Mwaka 2012 ulikuwa na Rank gani

Shahidi: Nilikuwa na Rank ya koplo

Nashon: Ni sahihi Kwamba Ulipokutana na Freeman Mbowe akakudodosa Kuhusu Rank yako ukamdanganya huna Rank

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Jibu ulilompa lilikuwa ni Sahihi

Shahidi: Ni sahihi Kwangu

Nashon: Lilikuwa Jibu la Ukweli

Shahidi: Sijui

Nashon: Scenerio zinazojitokeza za wewe Kudanganya Mara Kadhaa Unataka Mahakama Ikuamini wewe ni Shahidi Mkweli

Shahidi: Ndiyo Mimi ni shahidi Mkweli

Nashon: katika Ushahidi Wako Umesema Kwamba hufangamani na Chama Chochote Isipokuwa na Kiongozi aliyepo Madarakani, Ni sahihi

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Na Huyo Kiongozi aliyepo Madarakani, Hukusema Kwamba ni Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya au Rais

Shahidi: Nilisema Kwamba naheshimu Mamlaka zilizopo Madarakani

Nashon: Mwambie Mheshimiwa Jaji Kuwa wewe hukusema unaheshimu na siyo Kufungamana

Shahidi: Kimyaaaaaa

Nashon: Na Shahidi ni sahihi Kwamba Mara zote Freeman Mbowe alipokuwa anakutafuta alikuwa anakutafuta Kwa Njia za simu

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Na hata asipotumia namba yake Basi atatumia namba ya mtu Mwingine

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Hii Fact pia Iliwashirikisha Wapelelezi Waliokuwa Wanaopeleleza Kesi hii

Shahidi: Sijaelewa

Nashon: Ulipoenda Kwa DCI ulipewa nani awe Mpelelezi Wa Kesi yako

Shahidi: Kingai

Nashon: Je ulimueleza Swala hilo kuwa Mbowe akinitafuta lazima atatumia Namba ya Mtu Mwingine, Je Ulimwambia Kingai

Shahidi: Ndiyo Nilimwambia

Nashon: Na wewe Ulikuwa na Simu Nne, ambazo Umeziorodhesha Hapa Mahakamani

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Wewe na mpelelezi wako hamkuona umuhimu wa kuweka simu Moja Chini ya Surveillance, kuweza kurekodi pindi Mbowe atakapopiga

Shahidi: hapakuwa na umuhimu

Nashon: sasa shahidi umetoa hapa meseji, Je unaweza kutoa meseji hata moja yenye mwelekeo wa kupanga UGAIDI??

Shahidi: hakuna meseji ya neno GAIDI

Nashon: hayo ya Kwako, Nauliza Je kuna Meseji Kwamba inaonyesha Kuna Mwelekeo Wa Ugaidi

Shahidi: kuna Meseji ya Kuwasafirisha

Nashon: Kwa hiyo Meseji hiyo ina mwelekeo wa Ugaidi, inasemaje

Shahidi: Wale mtu tatu Wana uharaka

Nashon: naomba Kupatiwa Kielelezo namba 23

Nashon: naomba nikukabidhi Kielelezo hiki, unitafutie Meseji ya Kupanga Ugaidi

Shahidi: "Kaka Wale Mtu 3 au 4 ni muhimu sana, Siku zimeisha"

Nashon: Wewe ulivyosoma Kuna Ugaidi, ukaona Kuna Umuhimu sana wa kuleta mahakamani

Shahidi: Kwa sababu walikuwa wanahitajika na Mbowe

Nashon: Soma Meseji ya Tarehe 20 July 2020

Shahidi: Mmoja Yupo Tunduma anasafirisha Magari Kwenda Nje Ya Nchi na Mmoja yupo Dodoma kwenye SGR

Nashon: Na Meseji ya Saa 2 na Dakika 3

Shahidi: Simu Siyo Salama Sana, Niwezeshe nikakutane nao

Nashon: Ilikuwa siyo Salama kwa nani

Shahidi: Siyo Salama Kwa sababu Hatuelewani

Nashon: Soma Meseji ya hapo Chini ya Saa 2 na Dakika 5

Shahidi: Naomba Unitumie Nauli niweze Kuwa Mobilise Tukutane Morogoro

Nashon: hiyo Meseji ya nani

Shahidi: Ya Kwangu Mimi

Nashon: kwa hiyo Wewe ulikuwa Una mobilise Magaidi

Shahidi: Hapana Siyo Mimi ni Mbowe

Nashon: Freeman Mbowe ndiyo alikutana nao Morogoro?

Shahidi: Hapana ni mimi nilikutana nao Morogoro

Nashon: Kwa hiyo ulienda hadi Morogoro kukutana na magaidi nakuwa Mobilise wafanye ugaidi?

Shahidi: HAPANA SIYO MAGAIDI

Mahakama: Kicheko

Nashon: Unasema Kwamba Khalfani Bwire Alikwambia Kazi Imebadilika, Je ilikuwa ni Lini

Shahidi: Asubuhi ya Tarehe 4 August 2020, Saa 2 Asubuhi

Nashon: Kwa hiyo Bwire ndiye aliye +kwambia Ni lini Shughuli imebadilika

Shahidi: Hakuniambia ni Lini Imebadilika

Nashon: Kwa hiyo Ni sahihi Kwamba Bwire Alikwambia Tarehe 4 August 2020 alipofahamu Shughuli Imebadilika

Shahidi: Sijui

Nashon: Je Bwire Kwa kukupigia Simu wewe, Je alifanya Kitu sahihi?

Shahidi: Alifanya Kitu sahihi

Nashon: Kwa Mujibu wa Bwire Ndiyo Taarifa Yake ilipelekea Wenzake Kukamatwa Rau Madukani

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Je Ulirudisha Taarifa Kuwa Kijana Wangu Bwire Ndiyo amenipatia Taarifa hizi

Shahidi: Ndiyo ni sahihi

Nashon: Baada ya pale wewe ilikushangaza Bwire kukamatwa

Shahidi: Hapana Sikushangaa

Nashon: Kwani wewe Kwa uelewa wako Kwenye Scenerio hii, Kosa la Bwire lipo wapi

Shahidi: SIJUI

Nashon: Kwa hiyo, hufahamu kipande cha Bwire wala involvement (uhusika) wa Bwire katika kupanga matendo ya kigaidi?

Shahidi: MIMI SIJUI

Nashon: kwamba Shahidi Wewe Upo Nje, Na Bwire alikuwa informer Wako Yupo Gerezani, Wewe upo Nje Unakula Maisha?

Shahidi: Sifahamu aliyemkamata

Nashon: Kwani wewe Una u-Maalum au una mkataba na Serikali

Shahidi: Hapana

Wakili Nashon Nkungu: Mheshimiwa Jaji naomba Kuishia Hapa

Wakili John Malya: Mheshimiwa Jaji nitakuwa na Maswali Machache, Jibu kwa Sauti Mteja wangu Adamoo aweze Kusikia

Nakuonyesha Kielelezo hiki Kama Meseji hizi kama zinafanama na za Kwenye simu

Shahidi: Zinafanama

Malya: Nionyeshe Humu Kwenye Meseji Sehemu aliyokuita HOMEBOY

Shahidi: Hakuna

Malya: Umetutolea Sauti au uliyomrekodi Sauti ambayo Mbowe anakuita Homeboy

Shahidi: Sijaonyesha

Malya: Sababu Ya Kusema Maneno ambayo Kwenye Ushahidi Hakuna ikiwa ni Sababu Ya kujipendekeza tu Uonekane Mtu wa karibu Wa Mbowe?

Shahidi: Mimi Sina Device Ya Kumrekodi

Malya: walikuja watu wa Airtel hapa tukawaambia Kuwa wanatoa Siri za Watu Wakabisha, Nakuonyesha Kielelezo Namba 19. Ni sahihi hizi Taarifa ni za Kwako

Shahidi: Ni sahihi

Malya: Nakuonyesha hapa Muamala umepokea TSh 199,000, Kwenye Kielelezo P19 Tarehe 2 Mwezi July 2020

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Pamoja ni kwamba ni Kielelezo Cha Mahakama naomba Wakili awe ana Introduce

Malya: Kielelezo namba 20, inasemekana ni Miamala ya kwako, Kwa namba 0787 555200 Je ni Namba yako

Shahidi: Ndiyo Ni namba yangu

Malya: Kwenye Ukurasa Wa Pili wa Hii Nyaraka, Kuna Miamala Hapa, Unazungumzia 199,000

Shahidi: Ni namba Yangu

Malya: Ulipokea Kutoka Kwa Nani

Shahidi: Sikumbuki Imetoka Kwa Nani

Malya: Inaonekana Balance Yako Ilikuwa 121,000 baada ya Kupokea 199,000 Ikawa ni Tsh 302,0296 Shahidi Ndiyo naona

Malya: Kesho Yake Ulituma TSh 190,000 Kwenda Kwa GODSON MNURU Je ni nani

Shahidi: Simfahamu

Malya: anayefuata Ukamtumia URIO

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Sisi Kwenye Nyaraka Hakuna Majina, Mheshimiwa Jaji naomba Wakili atuambie Majina anatoa wapi

Malya: Shahidi tueleze Wew basi hizo namba Unazifahamu 0787000027

Shahidi: Namba hiyo naifahamu

Malya: Je huyo unayesema Unamfahamu, Je Mtu huyo ni Baina ya Wale Washtakiwa

Shahidi: Siyo Baina ya Wale Washitakiwa

Malya: Muamala Wa Tarehe hiyo hiyo 20 Muamala Wa 3 kutoka Juu

Shahidi: Ndiyo naifahamu

Malya: na Shahidi unasema Ulitoa Cash Kuwapa TSh ngapi Khalfani Bwire na wenzake

Shahidi: Niliwapa Cash TSh Laki 3 siyo Kutoka Kwa Wakala, Ilikuwa Mfukoni kwangu, Nilikuwa nayo Mimi

Malya: Pale usangu Mlikuwa Kidogo

Shahidi: Nisahihi

Malya: Wewe Ulikula Supu ya mbuzi na Chapati Mbili

Shahidi: Nilikula ila Sikumbuki

Malya: na Adamoo na Ling'wenya Walikuwa Supu ya Samaki na Chapati

Shahidi: Sikumbuki

Malya: Ila Unakumbuka Kuwa Mlikula

Shahidi: Ndiyo

Malya: nani alilipa Chakula

Shahidi: Nililipa Mimi

Malya: Ulitoa Wapi Pesa ya Kuwalisha Magaidi

Shahidi: Kwa Freeman Mbowe

Malya: Soma Maelezo Yako hapo Unasema Kwamba Ulitumia pesa ya na Mbowe ya Nini

Shahidi: Ya Kuwaita na na Nauli ya Kwenda Moshi

Malya: Kuna sehemu ambayo Freeman Mbowe alikwambia anakupa pesa ya kuwapa chakula

Shahidi: Hapana

Malya: Ila wewe ukaona uwalishe magaidi?

Shahidi: Nilikuta wanakula na mimi nikajiunga kula, kisha nikalipa bili

Mahakama: Kicheko

Malya: Twende Kwenye Mhamala Wa TSh Laki Tano.. Kwamba Mwanzo ulikuwa na balance ya 49,000 na Baadae ukatumiwa Tsh Laki 5 Ikawa 549,000

Shahidi: ni sahihi

Malya: nani alikutumia hii pesa

Shahidi: Freeman Mbowe

Malya: Hii Cash Out watu wa Simu walisema ni Kutoa Kwa Wakala

Shahidi: Upo sahihi

Malya: Ulitoa TSh 300,000

Shahidi: Ni sahihi

Malya: Ulielezea Mahakama Kwamba hii lako Mbili ulimpa nami

Shahidi: Nilimpa Adamoo na Ling'wenya

Malya: Kuna sehemu umesema Kwamba Ulitoa TSh ngap

Shahidi: Nilikuwa na Cash Mfukoni

Malya: Wakati Wa Ushahidi Wako Ulisema Kama Ulikuwa na Cash Mfukoni

Shahidi: Sikuulizwa

Malya: Twende Kwenye Kielelezo Namba 26 Ni sahihi Kwamba Ulisema Baada ya Vijana Wanne Kufika Kwa Mbowe ukakata Mawasiliano tena Bwana Mbowe

Shahidi: Ni sahihi

Malya: Ni sahihi Kwamba Siku Uliyomtembelea Mbowe alikuwa anatembelea na Magongo

Shahidi: Ilikuwa Jioni sikuona

Malya: Unakumbuka Kama alikuwa Mgonjwa

Shahidi: Ndiyo aliniambia Kwamba alipigwa na Wahuni

Malya: Ulikuwa unafahamu alikuwa nauguliwa na Mtoto wake na Yeye anaitwa Denis kama wewe

Shahidi: Aliniambia Kuwa nauguliwa tu.. Hakusema ni nani

Malya: Nikikuonyesha Nyaraka ya Hospital ambayo Inaonyesha Kwamba alikuwa na P. O. P na. Kwamba alikuwa anatembelea Magongo, Ukasema Kuwa Kaka wanakuonea Sana

Shahidi: Hapana Miye sifahamu

Malya: na wakati huo nauguliwa na Mwanaye

Shahidi: Aliniambia Kuwa Bado anauguliwa

Malya: Ni sahihi Kwamba Ukasema Kuwa Kaka Wanakuonea sana Ngoja Nikutafutie Vijana

Shahidi: Hapana Sikusema

Malya: Je unafahamu kwamba Mwaka 2020 ulikuwa Mwaka Wa Uchaguzi

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Malya: Je Unafahamu kwamba Maandalizi ya Uchaguzi yalikuwa yanakaribia

Shahidi: Sifahamu

Malya: kuanzia Mwezi Wa Saba Mpaka Mwezi wa 10 Kuna angalau Miezi Miwili

Shahidi: Ndiyo

Malya: Ushawahi Kusikia Kwenye Uchaguzi Kuna Vurugu kati ya Chama Kingine na Chama Kingine

Shahidi: Ndiyo Nishawahi Kusikia

Malya: Je ni Vibaya Mtu Kutafuta Ulinzi Kwa ajili yake

Shahidi: Sijui Kama Ni Kosa au Siyo Kosa

Malya: Lakini wewe Uliwatafuta Vijana Ukawaambia Waende kwa Mbowe Kufanya nini

Shahidi: Kuambatana kazi ya Ulinzi

Malya: Kwa hiyo Mtu Kuwa na Walinzi ni Kosa siyo Kosa

Shahidi: Sijui Kama Siyo Kosa

Malya: Kwa hiyo wewe wakati unawatafuta hawa akina Khalfani Bwire unawapa pesa au unawapeleka kwa Mbowe kuwa walinzi, hujui kuwa kosa siyo kosa?

Shahidi: SIYO KOSA

Mahakama: Kicheko

Malya: Sasa Kutafuta hawa Vijana Wanne Kwa ajili ya Ulinzi Kuna Kosa gani

Shahidi: Shida siyo Vijana... Inategemea Wanaenda Kufanya Kazi gani

Malya: Kwani Wewe Uliwatafuta Vijana Wanne Kwa ajili ya Nini

Shahidi: Hakuna Sehemu ambayo amesema Walinzi

Malya: Soma hapa Shahidi anasoma Kielelezo

Shahidi: Kaka Wale Watu watatu au wanne Ni Muhimu sana

Malya: hao Vijana sio Ndiyo hawa

Shahidi: Ndiyo

Malya: Wakati Unawatafuta Ulisema Kwamba Unawatafuta kwa kazi gani

Shahidi: Ya Ulinzi

Mahakama: Kicheko

Malya: Sasa wewe umeshaenda kwa DCI na DCI amekupa jukumu la kutekeleza huo mpango

Shahidi: Ni sahihi

Malya: Kuna sehemu kwenye meseji ya Mbowe inasema kwamba tukafanye uhalifu au ugaidi?

Shahidi: HAKUNA

Mallya: Soma hapa

Shahidi: Usiwe Unatumia namba yako binafsi tumia namba ya wakala au wasaidizi wako

Malya: Umeme lekeza Mbowe cha kufanya, Ni sahihi akitekeleza unachosema, haitoonekana namba yake bali namba yako wewe?

Shahidi: Ni sahihi

Malya: Mheshimiwa Jaji Sina Swali Zaidi Kwa Jioni hii, Muda siyo Rafiki naomba Hairisho Muda Umeshakimbia Naomba Kuendelea Kesho ambapo Wakili wa Mshtakiwa Wa Pili ataendelea na Maswali yake kwa Shahidi

Jaji: Kufuatili Maombi ya Wakili John Malya nahairisha Mahakama Mpaka Kesho Tarehe 28 January 2022 Shahidi ataendelea Kutoa Ushahidi Wake akiwa Kizimbani Washtakiwa wataendelea Kuwa Rumande chini ya Magereza Mpaka Kesho Asubuhi Saa 3

Jaji anatoka
 
Kabla mjumbe hujatuletea habari, naomba msaada wa kujua mambo yafuatayo.

1. Ni mamlaka gani huwa inaamua kutegeneza michongo, mamlaka ambayo hakuna chombo kingine kinaweza kuhoji? Hii mamlaka husimamiwa na chombo gani kisichoweza kutambua kwamba mamlaka hazifanya sawa?

2. Kesi za michongo kama hizi hutumia gharama kubwa sana. Juzi Mama amewaambia polisi waache kubambikia watu kesi, na PCCB wakafuta kesi kama sikosei 300 za michongo. Ninategemea kwa dhamira hiyo hiyo, Mamlaka zinatakiwa ziwawajibishe watu wote wanaohusika kwenye hiyo michongo kwa matumizi mabaya ya madaraka, uzembe kazini, uvunjaji wa katiba, kula njama na uhujumu uchumi.

3. Baada ya PCCB, kufuta kesi 300 za michongo, hatua gani zimechukuliwa kwa wachongaji?
 
... kabisa Mkuu; majina yao yameandikwa kwenye kitabu cha kumbukumbu; historia ikiandikwa imeandikwa. Watakumbukwa daima.
Siku moja, nchi itakapokuwa kwenye utawala na mamlaka ya wenye hekima, hawa wazalendo wa kweli itabidi tuwatambue kwa majina yao halisi, ili Taifa la watu wa haki na ustaarabu, liwajalie tuzo sawa na matendo yao mema.
 
Back
Top Bottom