Mh. Samwel Sitta ameuthibitishia umma wa watanzania na ulimwengu kwa ujumla kuwa sio yule wa Bunge la Tisa japo alijigamba kuwa ni sawa na Chura anayerudi majini. Imedhihirika wazi kuwa Chura yule wa Bunge la Tisa alijali Kasi na Viwango kwa Haki na Usawa. Lakini Chura huyo inaonekana Kazeeka au Kachakachuliwa baada ya kutaka kunyang'anywa kadi ya uanachama wa CCM wakati wa Bunge la Tisa.
Baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Bunge la Katiba alianza kwa kuchakachua kanuni iliyotaka Rais azindue Bunge kwanza alafu Warioba ndo awasilishe rasimu kwa bunge hilo. Mambo yakaanza kwenda mrama. Leo hali imekuwa mbaya pale aliporuhusu CCM kutaka kuchakachua kanuni ambazo hata hazijaanza kutumika. Badala ya kushughulikia kanuni zilizosalia wao wameleta lundo la kanuni ili zirekebishwe wakati ni kanuni zilizopitishwa kwa maridhiano. Swali la kujiuliza ni kuwa hayo maridhiano yalikuwa ni unafiki tu? Na je, ni upungufu gani ulioonekana kwa sasa wakati hata hizo kanuni hazijaanza kutumika?
Huyo ndiye Sitta na nadharia ya Chura anayerudi majini. Kwa Mwendo huu Chura huyu amezeeka ama kachakachuliwa? Je atamudu kuogelea maji hayo tena kwa mwendo huu? Funguka.