Chabruma
JF-Expert Member
- Sep 19, 2013
- 5,660
- 1,782
Wadau, ni matumaini yangu kuwa hamjambo na Mwenyezi Mungu amewaamsha mkiwa salama. Kwa wale wagonjwa tuwaombee kwa Mwenyezi Mungu awajaalie wapone mapema. Kwa wale waliofikwa na mauti, tuwaombee kwa Mwenyezi Mungu ili wawe na makazi mema huko waendako.
Baada ya zoezi la kuchagua Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa Kamati za Bunge Maalum kukamilika ambapo majina yao yametangazwa jana asubuhi, kazi ya leo kwa mujibu wa ratiba iliyotangazwa juzi Jumatatu na Mwenyekiti, Sammuel Sitta ni kwamba leo asubuhi zile kanuni za 37 na 38 za Bunge Maalum ambazo ziliwekwa kiporo zitafanyiwa maamuzi. Vifungu hivi vinahusu namna ya kufanya maamuzi wakati wa vikao vya Bunge Maalum. Ni maamuzi gani yamefikiwa, sote tuwe sambamba kwenye mjadala huu.
Vilevile, ni kwamba siku ya leo, Wabunge watapata fursa ya kujadili hotuba za Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba aliyoitoa Bungeni Dodoma Jumanne tarehe 18 Machi 2014 pamoja na ile ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete aliyoitoa Bungeni Dodoma Ijumaa tarehe 21 Machi 2014. Mjadala huu utategemea hali itakavyokuwa kwenye zoezi la kupitisha kanuni za 37 na 38. Kwamba, ikiwa hakutakuwa na mivutano mikubwa wakati wa kupitisha kanuni hizo, ni wazi kuwa wabunge watapata muda wa kutosha kujadili hotuba hizo. Ama ikiwa mivutano iliyozoeleka itajitokeza, ni wazi kwamba wabunge watajinyima fursa hiyo kwani muda uliotengwa wa kujadili hotuba hizo ni leo tu.
Kama kawaida, ni matumaini yangu kuwa wadau mbalimbali watashiriki kwenye mjadala huu .
Stay Connected.
------------------------------
- Mwenyekiti anasema kuwa kwa mujibu wa taarifa aliyotoa woki iliyopita, alisema kuwa kwa siku ya leo wangeweza kujadili hotuba ya JK na ya Warioba. Hata hivyo amesema kuwa hiyo ingekuwa ni sawa na kutanguliza mjadala. Pia inapingana na kanuni za bunge hilo ambazo zinasema kuwa bunge litajadili vifungu viwili vya kanuni. Kwa vile wabunge wasingeweza kuzuiliwa ya kuongea, sasa ametangaza kusitisha mjadala huo.
- Bunge limeahirishwa mpaka leo saa kumi jioni.
-------------------------------
BUNGE JIONI YA LEO
- Bunge linaendelea tena muda huu. Mwenyekiti ametoamnafasi kwa wenye miongozo. Lissu amesimama na anazungumza. Anasema kuwa kanuni zimekuwa zikivunjwa na Mwenyekiti amekuwa akiyumba sana katika kusimamia kanuni hizo
- Lissu anasema kuwa wameletewa jedwali la marekebisho ya kanuni ya bunge maalum. Kwamba marekebisho kuhusu kanuni za 14, 32,33,35,37,38,58,61(1),64(1), 85(4). Anasema kuwa mabadiliko haya yanaletwa na Katibu wa Kamati ya Uongozi. Alisema kuwa hiyo si sahihi kwa vile kanuni inaeleza bayana. Anasema kuwa kanuni hazina hata wiki tatu na bado zinaanza kuchakachuliwa. Anasema kuwa viporo vya 37 na 38 ndivyo vinavyotakiwa viwasilishwe. Alisema kuwa hayo marekebisho hayatakiwi kuwasilishwa. Pia anasema kuwa kamati ya uongozi haina mamlaka ya kuleta mabadiliko ya kanuni. Anasema kuwa hii takataka, uchafu nk hataki iingizwe kwenye bunge hili. Mwenyekiti anasema kuwa tuhuma za Tundu Lissu ni nzito na amezitoa bila yamkuwa na karatasi ya marekebisho hayo. Anasema kuwa Kamati ya Uongozi imefanya kazi ya kuandaa kazi za kila siku. Anasema kuwa kamati ya kanuni ndiyo inapaswa kuwasilisha marekebisho ya kanuni. Anasema kuwa tusubiri hicho kinachopaswa kuwasilishwa na kikionekana ndipo bunge litaamua.
- Abubakar Hamisi Bakar anasema kuwa utaratibu wa kubadilisha kanuni upo kwenye kanuni ya 87. Anasema kuwa mtu anayetaka kurekebisha kanuni afuate taratibu. Anasema kuwa chochote kitakachofanyika kinyume cha sheria hakitakubalika
- Jaji Werema amesimama na kusema. Jambo analoliona ni kwamba, wabunge wanawahisha hoja. Kwamba kanuni ya 87 inasomeka hivi;
- Ismail Jusa naye amesimama kumuunga mkono Tundu Lissu
- Mwenyekiti ameagiza Kamati ya Kanuni kushughulikia jambo hilo na walifanyie kazi baada ya kikao cha leo. Amesema kuwa kamati hiyo itawasilisha kesho saa 10 jioni. Kwa hali hiyo, bunge linaahirishwa mpaka kesho saa 10 jioni. Sasa mwenyekiti anasoma dua ya kuliahirisha bunge.
Ahsanteni kwa kuwa pamoja nasi. Tukutane kesho saa kumi jioni

- Bunge maalum linaweza kuzifanyia mabadiliko au marekebisho kanuni hizi kwa azimio litakalowasilishwa kwenye bunge maalum na mwenyekiti wa kamati ya kanuni na hadhi za bunge. Hii ni kanuninya 87 (1). Anasema kuwa mchakato uliofanyika wa kupitisha kanuni haizuii kufanyia marekebisho
- kanuni ya 87 (2) ndiyo inayosema kuwa mjumbe yeyote anaweza kuwasilisha marekebisho ya katiba kama Tundu Lissu anavyosema. Hivyo Lissu amechanganya