Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumatano Tarehe 26 Machi 2014

Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumatano Tarehe 26 Machi 2014

Toka achaguliwe kuwa mwenyekiti wa Bunge la katiba Mh. Sitta amepata upinzani mkubwa katika kuendesha bunge. Heshima aliyokuwa nayo na hata waliomsifia kama Jussa leo wanamnanga kwa kukiuka kanuni. Kumbe basi katika kuongoza bunge Mh Makinda, Ndugai na Sitta hawana tofauti!!! Sitta alijiamini sana kwakuwa aliungwa mkono na wajumbe wa pande zote!
 
Mkuu wananchi waoga sana ndo maana wanasiasa wanatudharau sana na kuchezea akili wanavyotaka

Huu ni woga wa kupiliza, vijana wadogo pale Taiwan wamesimamisha shughuli za Bunge wakitaka Rais aweke wazi mkataba aliosahini na China. Sisi Rais alisahini mikataba 11 tukanyamaza kimya. Ujinga wetu utatumaliza.
 
Mh. Samwel Sitta ameuthibitishia umma wa watanzania na ulimwengu kwa ujumla kuwa sio yule wa Bunge la Tisa japo alijigamba kuwa ni sawa na Chura anayerudi majini. Imedhihirika wazi kuwa Chura yule wa Bunge la Tisa alijali Kasi na Viwango kwa Haki na Usawa. Lakini Chura huyo inaonekana Kazeeka au Kachakachuliwa baada ya kutaka kunyang'anywa kadi ya uanachama wa CCM wakati wa Bunge la Tisa.

Baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Bunge la Katiba alianza kwa kuchakachua kanuni iliyotaka Rais azindue Bunge kwanza alafu Warioba ndo awasilishe rasimu kwa bunge hilo. Mambo yakaanza kwenda mrama. Leo hali imekuwa mbaya pale aliporuhusu CCM kutaka kuchakachua kanuni ambazo hata hazijaanza kutumika. Badala ya kushughulikia kanuni zilizosalia wao wameleta lundo la kanuni ili zirekebishwe wakati ni kanuni zilizopitishwa kwa maridhiano. Swali la kujiuliza ni kuwa hayo maridhiano yalikuwa ni unafiki tu? Na je, ni upungufu gani ulioonekana kwa sasa wakati hata hizo kanuni hazijaanza kutumika?

Huyo ndiye Sitta na nadharia ya Chura anayerudi majini. Kwa Mwendo huu Chura huyu amezeeka ama kachakachuliwa? Je atamudu kuogelea maji hayo tena kwa mwendo huu? Funguka.
 
Wakuu,
ni dhaili sasa kuwa mh.Samwel Sitta ameshindwa kazi ya kuliongeza bunge la katiba ambalo lingewaletea watanzania katiba waitakayo.

Kwa kadri siku zinavoenda Sitta anaonekana kupwaya sana kwenye kiti hasa katika eneo la upindishaji kanuni .Mtakumbuka Sitta alipindisha kanuni tena nje ya utaratibu ili kumwezesha Kimwete aje kumjibu Walioba na sasa anataka kuzipindisha tena kwa kile anachokiita kuziboresha.Ahiingii akilini kuona kanuni zilizotumia wiki tatu kutengenezwa zinaanza kubadilishwa hata kabla ya kuanza kutumika.Hii inaleta dhana moja tu,nayo ni kuwa kuna watu wamejipanga kuendesha mambo kwa kadri wanavyotaka.

Sitta ulikuwa umejenga imani kwa watanzania kwa yale uliyowai kuyafanya,lakini kwa mwendo huu unaweza kushuka mpaka ziro.Kaka CCM walikusudia kukudhoofisha sasa wamefanikiwa .

MY TAKE;
Kati ya haya mawili chagua moja la kusimamia na kamwe usikae katikati
.Simama upande wa wananchi na uliongoze bunge viwango,weledi na hatimae tupate katiba.upande chati
.Simama upande wa CCM ili uendeshe bunge kama roboti na ujiporomoshe kisiasa.

Huyu mzee wa kutokwa jasho hata kwenye viyoyozi vikali.. Ni MNAFKI SANA.. Tangu alipoanza vigeugeu amekuwa kama kinyonga...(siyo amekuwa ni KINYONGA MWENYE NDIMI MBILI) NIMEMCHUKIA SANA HUYU MZEE.. Kwanza ni jinsi wanavyopoteza muda.. Kila mara anaahirisha vikao... HAFAI
 
UKAWA ni nini? Kuuliza si ujinga.

Ni Umoja wa Katiba ya Wananchi. Ni Umoja unaojumisha wapinzani wanaotetea rasmu ya Jaji Warioba na kuitafuta kwa udi na uvumba katiba ya wananchi tofauti na rais na wana ccm wanataka katiba iwe ya ccm! Shame on them!
 
Amepoteza mvuto kabisa.Ila ni vizuri wananchi wakamjua mapema,kwamba sio mtu wa kutabirika,hafai kuwa na ndoto ya uraisi kwa namna hii.
 
ila hata raia wa tz wamelala sana; kuna nchi huu ushenzi hauvumiliki kabbisa!

Nyerere aliipumbaza tanzania na watanzania wote. Mijitu imellala kama vile ni mitaahira- Ujamaa ni sumu mbaya sana sana. Just look at the former soviet states, utaahira huo huo kama wa watanzania, ndio maana bado CCM wanazoa kura vijijini ambako watu ni kama magunia ya viazi aliyoyasema Lenin- Peasants are like sacks of potatoes, they will never make revolution-even a peaceful one!, only the working class can!!!
 
Tangu nilipoona 6 kapita kugombea ccm, nilijua kuna jambo, nakatika watu waonweza kuuza mke kwa uchu wa madaraka ni huyu mzee, maana sas hivi anafany jitihaada za kupitishwa mgombea urais ccm.Kwahiyo yupo tayari kuuza nchi kwa ahaadi ya urais! Shame on him!

Kwangu mie hii katiba inayotengenezwa sasa ni katiba ya ccm na siyo ya nchi.
 
Back
Top Bottom