Yanayoendelea Zanzibar tusubiri majibu ya Wahanga na kuzaa gharika

Jason Bourne

JF-Expert Member
May 11, 2011
200
438
Nimestushwa na kuogopa tena nikalazimika kuisoma Katiba ya Zanzibar mara mbili.

Leo Waislamu wa Zanzibar wanawavamia na kuwapiga vibaya Wazanzibar wenzao ambao sio Waislamu kwakuwa tu wanakula kwa mama lishe mchana mda ambao wale waislamu wanakuwa wamefunga.

Vipigo vimeenea kila kona ya mji wa Zanzibar na uhasama unakua kila kukicha, serikali ipo kwenye mfungo mtukufu, Wakristo hawa Wazanzibar hawana msaada, nani awaokoe vijana wa kikikristu ambao hawajao wanaotegemea kwa mama lishe na migahawani kupata mlo wao nao wafunge?

Nini tutarajie majibu ya wahanga hawa kama sio gharika? Serikali inasubiri kuunda tume baada ya mauaji??

Nimeisoma na kuipekua katiba ya Zanzibar kuona kama kuna kifungu kinachowapa haki waislamu kudhibiti uhuru wa watu wengine,

Zaidi nilitaja kujua kama Zanzibar ni nchi ya kidini au ni nchi inayotawaliwa kwakufuata sharia.

Sehemu mhimu ya katiba ya Zanzibar ni hii hapa, jioneeni kama ni haramu kula chakula hadharani nchini Zanzibar.

SURA YA KWANZA- ZANZIBAR
Sehemu ya Kwanza

1. Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na Visiwa vidogo vilivyoizunguka na bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

2. Zanzibar ni miongoni mwa Nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 2A. Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali, Rais aweza kuigawa Zanzibar katika Mikoa, Wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi.

3. (1) Kutakuwa na Muhuri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambao alama yake itakuwa kama itavyokubaliwa na sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi.

(2) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itakuwa na uwezo wa kuweka kitu chochote kitachokuwa kielelezo cha Serikali kama itavyokubaliwa na sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi.

4. Katiba hii ni Katiba ya Zanzibar na itakuwa na nguvu za kisheria nchini kote na isipokuwa kutokana na kifungu 80 ikiwa sheria yoyote inatofautiana na Katiba hii, basi Katiba hii ndiyo itayokuwa na nguvu na sheria hiyo itakuwa batili kwa kiwango kile ambacho kinahitilafiana.

5. Zanzibar itafuata mfumo wa Kidemokrasia wa Vyama Vingi vya Siasa wenye kuheshimu utawala wa sheria, haki za binaadamu, usawa, amani, haki na uadilifu.

5A. (1) Zanzibar itafuata mfumo wa mgawanyo wa madaraka kati ya mamlaka tatu, Mamlaka ya Utendaji, Mamlaka ya Kutunga Sheria na Kusimamia Utekelezaji wa Shughuli za Umma na Mamlaka ya Kutekeleza Utoaji Haki.

(2) Mamlaka ya Utendaji ni Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mamlaka ya kutunga Sheria na Kusimamia Utekelezaji wa Shughuli za Umma ni Baraza la Wawakilishi na Mamlaka ya Kutekeleza Utoaji Haki ni Mahkama.

(3) Hakuna mamlaka itakayoingilia Mamlaka nyengine isipokuwa kama na kwa kadri ilivyoelezwa katika Katiba hii.

Pia soma:
Vitu vingine vilivyowahi kupigwa marufuku Zanzibar
 
Mbona haijatokea gharika Tanganyika ambako wenye macho mekundu wanauliwa, au maalibino kukatwa viungo vya mwili na watu kuchunywa ngozi!!!????

Au katiba ya TZ inaruhusu haya? Na mbona hauyashangai haya na badala yake unakuja kushangaa watu wanaopigwa bakora ZNZ kwa kosa LA kula mchana wa mwezi wa Ramadhani!!??? Acha unafiki name kumbuka hicho kitabu chako unachokifuata kinasema ukitaka kutoa kibenza kwenye jicho la mwenzako basi anzia kutoa boriti kwenye jicho lako

Lakini sikushangai sana maana mfumo kristo ndivyo ulivyokulea kulifanya kubwa lolote lile ambalo waislamu watalifanya name kuliona dogo lolote lile ambalo wakristo watalifanya hata kama ni mapdri kulawiti watoto
 
Umejuaje kwamba hao wanaopigwa na Wakristo? Kwani kwa kuwa huu ni mwenyezi mtukufu ndo unadhani kila anayejiita mwislamu anafunga?

Ni sahihi kabisa kukemea kitendo hicho lakini kusema wa-Islamu wanawapiga Wakristo bila kuwa na uhakika ikiwa wanaopigwa ni wa-Kristo, nashawishika kuamini huko ni kuvuka mipaka.
 
Hata kama angekuwa muislam hauna haki ya kumlazimisha kufunga. Mahusiano ya kiroho ni ya mtu binafsi na Mungu ndio maana kuna Jehanam na Pepo. Huwezi kumlazimisha mtu ili aende peponi nyie vichwabuta.

Mbona uulizi kwanini makanisa mengi sana huko Tanzania Bara yanazuia kwa nguvu zote waumini kuingia na vimini wakti wa ibada? Je hujui kwa nini?

 
Mbona uulizi kwanini makanisa mengi sana huko Tanzania Bara yanazuia kwa nguvu zote waumini kuingia na vimini wakti wa ibada? Je hujui kwa nini?

Kwani hao wanaenda kulia chakula chao msikitini? Halafu kama unashindwa kuvumilia tamaa ya chakula eti kwa kuwa umemuona mtu anakula wakati wewe umefunga, sasa hapo umefunga kitu gani? Waisilamu bwana hawatambui logic behind wanachokitekeleza katika ibada yao, vinginevyo wangeweza kutenganisha mambo ya mwili na roho!
 
Mbona uulizi kwanini makanisa mengi sana huko Tanzania Bara yanazuia kwa nguvu zote waumini kuingia na vimini wakti wa ibada? Je hujui kwa nini?


Huo ni ustaarab tu wa kibinaadam na kuheshimu eneo na haina uhusiano wowote na roho ya mtu. Watu wanavaa hijab na wanakwapua vile vile. Je hijab inamhalalisha mtu kama huyo kwamba hawezi kuwa kibaka?
 
hakuna anaelazimishwa kufunga hapa zanzibar.kwa wale ambao hawadungi wanakatazwa wasile hadharani kakini.kwa maana hiyo wanatakiwa wale majumbani kwao.kutokana na huvo viongozi wa serikali,mashekhe na waumini hutangaza kwamba si.ruhusa kula hadharani ndani ya mwezi mtukufu wa ramadhani.suala hilo halipo ndani ya sheria lakini serikali ina haki ya kutoa amri ya kitu fulani kisifanywe iwapo kinaonesha kuleta madhara fulani.suala la serikali kukataza watu wasile hadharani ni sawa na kukataza maandamano kutofanyika.serikali hii leo iseme ni ruhusa zanzibar wasio waislamukula hadharani hapo patatokezea ugomvi mkubwa usio zuilika
 
Kwani zanzibar kufunga wameanza leo??

Ukristo zanzibar umeanza leo??

Tusisikie hayo mambo miaka yote tuje tuskue leo??

Hivi Kukaa bila kuwachokonoa waislam hamjiskii raha.

Hii id ya jason bourne nakumbuka Mods hapo awali walishawahi kuiuunganisha na Yericko Nyerere.

Hivi huyu jamaa anasumbuliwa na nin hasa??

Kutwa kucha kuanzisha ids za kijinga na kuanzisha mijadala isiyo na tija.

Mods angalieni hivi vitu baadae huja kusababisha taharuki zisizo na maana.
 
Uislamu haupendi kibri! We we unajua watu wako katika funga sasa kama hutaki kufunga basi kula chakula chako kwa kujificha sio uoneshe jeuri....
Na anayetoa adhabu kwa mwenye kibri ni mwanadamu, sio Mungu! Ha ha haaa, dini ya allah yenye kutegemea hukumu itolewe na mwanadamu!
 
Kwani zanzibar kufunga wameanza leo??

Ukristo zanzibar umeanza leo??

Tusisikie hayo mambo miaka yote tuje tuskue leo??

Hivi Kukaa bila kuwachokonoa waislam hamjiskii raha.

Hii id ya jason bourne nakumbuka Mods hapo awali walishawahi kuiuunganisha na Yericko Nyerere.

Hivi huyu jamaa anasumbuliwa na nin hasa??

Kutwa kucha kuanzisha ids za kijinga na kuanzisha mijadala isiyo na tija.

Mods angalieni hivi vitu baadae huja kusababisha taharuki zisizo na maana.
Nakubaliana na wewe wakiristo Zanzibar wapo hata kabla ya Tanganyika na hawajalazimishwa kufunga waulizeni akina Charles Hilarry kinachogomba hapa ni kula hadharani jambo ambalo limekatazwa usitake kuleta fitna sisizo maana
 
Hivi kuna sababu watu kutukanana? Tumedhindwa kuhedhimiana watanzania wenzangu? Mbona dini hizi mbili hazifanani na hazitakaa zifanane ila ninaimani tunaweza kuhedhimiana, kupendana, kujaliana na kushikanamana pamoja.
Kwa matusi haya tunatengeneza hukumu na kujitsyarishia jehanamu huko tuendako. Mods mko wapi wakati hii kadhia inaendelea? Tupo tusiopenda matusi yanayoambatana na imani za dini zetu.
 
Nakubaliana na wewe wakiristo Zanzibar wapo hata kabla ya Tanganyika na hawajalazimishwa kufunga waulizeni akina Charles Hilarry kinachogomba hapa ni kula hadharani jambo ambalo limekatazwa usitake kuleta fitna sisizo maana

Kwani wakila hadharani kinakuuma nini wewe ambae umefunga.
 
Amri kumi za Mussa zinasemaje?
Hakuna uhusiano na swali nililokuuliza, labda nirudie tena,
Anayetoa adhabu kwa mwenye kibri ni mwanadamu, sio Mungu! Allah gani huyo mwenye kutegemea hukumu itolewe na mwanadamu!
 
Kwa nini waisilamu huwa wanapagawa sana kwenye mambo ya misosi, hasa pilau? Isije ikawa ndio sababu ya kupata hasira kuona wengine wanawamalizia chakula mchana wakati wenyewe hadi wakisubiri usiku!
 
Back
Top Bottom