Yaliyomsibu kaka yangu

Yaliyomsibu kaka yangu

Huyo pichani ndio wewe?
Msiwe mnaharakisha kufanya mapenzi na watu mlokutana nao mitandaoni..iwe jf,fb or enewea!
Kazania kwenda kupiga ,weka uwoga pembeni kwani huwezi jua unaweza kuwa ni mzima halafu mwenzio anano akakumaliza..kisa muoga wako

Niliyasema mimi nkatukanwa mimi
Aggy nawaambia kuweni makini vijana wenzangu,kuna wapuuzi hawajali u salama wa wenzao when it comes to mapenzi..nkageuka mtoto..
Na ntaendelea kuwa kimya na msimamo wangu...awamalize wote..panya wajuaji nyie!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaka angetupatia na kapicha tuone walioathirika wanafananaje jamani.... Mbona msala huu...
Kaka yangu hajaoa ingawa alikuwa kwenye mahusiano ya muda mrefu yaliyompatia watoto wawili wakike. Yeye na girls mother waliachana dada yule alipata mtu na kufunga nae ndoa ya kanisani. Imefika wakati kaka alianza kutafuta.

Humu JF kaka alimpata mdada mmoja. Very independent woman, Ana career, nyumba na maisha yake kwa kweli. Hajawahi kuolewa na kwake mabinti wa kaka haikua shida.

Wameanza dating, kwa miezi sita, kumbe dada ni muathirika na yuko kwenye dawa pendwa. Wakiwa pamoja alimlia timing kaka akiwa msalani mdada anabugia vidonge.

Kaka alishtukia hilo, sikumoja wakiwa Bagamoyo weekend, kaka alijifanya anakwenda msalani, alijiegesha kwenye mlango wa choo, ile dada anafungua handbag na kuchukua dawa jamaa amejaa.

Mahusiano yaliishia hapo. Kaka alijicheck yuko poa. Alimshukuru Mungu maisha yakaendelea.
 
Kuna dada aliandika story yake, yeye alikaa five years baada ya kuwa diagnosed bila boy friend wala sex. Alikutana na mkaka walianza dating, mwisho waliamua kuishi pamoja. Kwa mwaka mmoja, kaka alinunua engagement ring. Siku moja anatoka kazini jioni alifanyiwa surprise ya engement. Dada alilia sana, ikabidi amueleze yule kaka ukweli.

Boxer aliyokuwa amevaa jamaa ilikuwa ndogo ghafla. Alikwenda ndani akapack begi lake alikwenda kucheck in hotelini.
Baada ya hapo alikwenda baa alikunywa mpaka baa inafungwa.

Asubuhi alipiga simu kazini kuwafahamisha hatakwenda siku ile, alikwenda kwenye kitengo. Alimueleza daktari hali halisi. Daktari alimwambia mara nyingi waathirika wakiwa kwenye control ya ugonjwa hawaambukizi na pia huwa hawahangaiki sana. Kana unampenda nenda nyumbani mkaongee. Majibu yalikuwa-ve.

Alirudi nyumbani na engagement iliendelea.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom