Nifanye nini Kaka yangu hamtaki mchumba wangu

mamamzungu

JF-Expert Member
Nov 17, 2019
2,374
3,887
Anasema ikitokea tumeoana hatutoboi miaka 5…. Namnukuu “ Mkitoboa miaka 5 niko pale uniite mbwa”

Ni kaka yangu mtoto wa mama yangu mdogo alielelewa nyumbani kwetu… yeye tayari ana familia yake mke na watoto yuko under 30 .. Ni kaka ambaye tumekuwa tukishirikishana mambo ya mahusiano yetu mpk sasa..

Sikujua kuwa mpenzi wangu anafahamiana na kaka yangu mpk siku nilipompost status nikimuwish happy birthday..

Kaka yangu alinifungukia kuwa wanafahamiana na wamepiga kozi wote kiufupi wanafanya kazi zinazofanana na wanajuana mpk vyumba wanavyoishi japo hawana urafiki ni ile wakikutana ndio wanakuwa marafiki..

Mpk Kaka yangu anakuja kufahamu nina mahusiano nae ilichukua mwaka mzima kumfahamu na sikumwambia kuwa tuna mahusiano nilimwambia tu marafiki

Kwa sasa tunaelekea hatua nzuri kaka yangu amenishikia king’ora kwamba huyo mwanaume hanifai niachane nae simuwezi.. ninapomuuliza sababu haniambii nikazielewa

Sababu mpk sasa nilioiona kubwa aliyoniambia ni kuwa

  • kabila la watu wa mwisho wa dunia sio kabila la kuolewa nao ( yeye ameishi sana huko so ana wafahamu)
  • Ni washirikinaa sanaa ( anaamini kwamba huyu mpnz wangu kanipata kwa madawa) alinipa kielelezo Kuna rafiki yake mwingine wa kabila hilo alimpata mwanamke kwa madawa matokeo wamezaa watoto wawili mwanamke akili imefunguka kakimbiaa

Kubwa la Leo ambalo limenifanya niombe ushaurii ni hili

Amesema kuwa huyu mpzn wangu alishawahi kutoa posa mahali halafu akahairisha kuoa.. na alimpa ujauzito huyo mwanamke ila aliukataa akasema atoe ujauzito,, mwanamke alipokataa kutoa mimba alimtumia hawara yake ampelekee Zawadi ya juice kumbe ndani ya juice kaweka dawa ya kutoa mimba

Hiyo story bro anadai kahadithiwa na ex wa mpnz wangu

Kiukweli nimeshindwa kuelewa nifanye nini.. Kijana nampenda na amekuwa mtu mwema kwangu mpk sasa tuna miaka 2 ya mahusiano sijaona bays kwake

Ushaurii wenu wakuu
 
Wanaume tuna sheria zetu, hatutaki marafiki zetu wawaonje dada zetu.

Nishawahi shuhudia urafiki unavunjika na hata kupigana pale marafiki ama kundi la marafiki moja wao ikibainika kaonja dada wa mwengjne.

Ila yawezekana kweli ana hizo tabia.
 
Mtoto wa mama mdogo awe mkubwa au mdogo hana haki / wajibu wa kukuchagulia aina ya maisha au mienendo.
Ameniambia nitulie yeye ana marafiki wazuri tyu wananifaa… sasa mimi mwanaume wa kutafutiwa siwatakii
 
[mention]Moderator [/mention] niwekeeni uzi vizuri umejirudiarudiaa
 
Wanaume tuna sheria zetu, hatutaki marafiki zetu wawaonje dada zetu.

Nishawahi shuhudia urafiki unavunjika na hata kupigana pale marafiki ama kundi la marafiki moja wao ikibainika kaonja dada wa mwengjne.

Ila yawezekana kweli ana hizo tabia.

Sasa kama ananioa si ndio urafik unadumu maana hanichezei
 
Labda kama wewe no mamaafrica, lakini mamamzungu umelowa huna akili binafsi duuh pole, ushauri sio shuruti Vaa koti hilo ujionee
 
Back
Top Bottom