Yaliyojiri wakati wa hafla jiwe la msingi ujenzi wa meli mpya, chelezo na ukarabati wa meli Ziwa Victoria za Mv Victoria na Mv Butiama

Mungu Ni Mwema Wakati Wote





Waendelee Kujenga Zikamilike Kwa Wakati
 
Wanawaza kununua meli kwenda Comoro wakati usafiri wa kwenda Mafia - Nyamisati au Dar hakuna, Tanga - Pemba nako hakuna usafiri wa uhakika hata Unguja to Pemba ni changamoto....
 
Wanawaza kununua meli kwenda Comoro wakati usafiri wa kwenda Mafia - Nyamisati au Dar hakuna, Tanga - Pemba nako hakuna usafiri wa uhakika hata Unguja to Pemba ni changamoto....

Unguja Wana serikali yao, ya kwao hayatuhusu. Nadhani ujenzi sio wizara ya muungano
 
Kusema kuwa kuvuka hapo yanatumika masaa 2 ni uwongo wa hali ya juu. Nimevuka mara nyingi.

Ukipandisha gari lako MV Misungwi, inachukua kama dakika 15 mpaka 25. Na MV Sengerema huchukua daki 25 mpaka 30. Labda kama hayo masaa mawili wamejumlisha na muda wa kukaa foleni ikitokea kuna magari mengi au kivuko kimojawapo kikawa kimeharibika.
Sasa unaposubiria kama kuna daraja si ungekua umeshavuka huo muda wa kusubiri.
Daraja litatatua changamoto zote hizo.
 
Sawa nijambo nzuri sana kupata maendeleo ila hicho nikipaumbele cha kanda ya ziwa kuna tatizo makubwa la kuvuka hapo kweli kiasi kwamba nchi itumie karibu 700bn......ambozo ingeziweka kwenye kilimo au afya na elimu hizo wilaya zingefaidika kuliko dalaja la kuvuka mgambo wakati kuna vivuuko zaidi ya vitano hapo busisi na Kamanga vipo vivuko.....
Ndugu muda ni Mali kwa nijuavyo, kwamba watu watakaotumia daraja hilo ni wa wilaya mbili tu?
Kuwekeza kwenye miundombinu ya usafirishaji ni kuokoa muda, uhai, kuchangamsha biashara n.k
 
Unguja Wana serikali yao, ya kwao hayatuhusu. Nadhani ujenzi sio wizara ya muungano
Mbona tulimpa Mzanzibar awe Waziri wa Ujenzi kama Ujenzi siyo suala la Muungano? Au ndiyo maana alimtoa haraka haraka?
 
Tangu dunia iumbwe hii kitu imetokea Tanzania pekee. Leo Rais John Magufuli akiwa huko mkoani Mwanza ameweka jiwe la msingi na kuzindua utengenezaji wa meli hapa nchini.

Sijawahi kuona utengenezwaji wa meli kokote kule duniani ukiwekewa jiwe la msingi

Maswali ya kujiuliza, ilo jiwe la msingi litakuwa linazunguka na meli kokote iendako?

Je meli za wenzetu huko walioendelea meli zao zina mawe ya msingi?

Rais wa kuweka mawe ya msingi kila kitu ni mawe ya msingi tu hakika ni rekodi ya karne.
 
Tatizo ni akili zako..

Appreciation. Jiwe la msingi maana yake ni kumbukumbu ya kuasisi uzinduzi wa tukio fulani.

Je, alichofanya ni kibaya..? Kina manufaa kwa waTanzania wa hali zote?

Mi nafkiri tuzingatie manufaa ya Taifa zaidi badala ya ushabiki usiokuwa na mpango.

NB: mimi sio mwanasiasa na sio mwanachama wa chama chochote cha siasa
 
Back
Top Bottom