Yaliyojiri wakati wa hafla jiwe la msingi ujenzi wa meli mpya, chelezo na ukarabati wa meli Ziwa Victoria za Mv Victoria na Mv Butiama

Na wafanyakazi wa serikalini wanatembea kifua mbele maana na wao pia wanajisikia ni matajiri sababu tangu alipoingia madaraka mpk leo wanapandishwa madaraja na annual increment ni uhakika,huku walimu wanao-graduate vyuoni kila mwaka akiwaajiri nao pia wanajisikia ni matajiriiii bila kusahau kada nyingine zinazo graduate kila mwaka amezimwagia ajira kwa maelfu nao pia ni matajiriiiiiiiiiiiii.
 
Kusema kuwa kuvuka hapo yanatumika masaa 2 ni uwongo wa hali ya juu. Nimevuka mara nyingi.

Ukipandisha gari lako MV Misungwi, inachukua kama dakika 15 mpaka 25. Na MV Sengerema huchukua daki 25 mpaka 30. Labda kama hayo masaa mawili wamejumlisha na muda wa kukaa foleni ikitokea kuna magari mengi au kivuko kimojawapo kikawa kimeharibika.
 
Kwasasa kwa ferri mpya ambayo imegharimu pesa kubwa nidakika 15-20tu kuvuka sasa hiyo ferri mpya pamoja na kugharimu pesa nyingi itakaa bila kazi dalaja likiisha hiyo ndo poor economic planning ya nchi hi

Hapana kuna four years za ujenzi ambapo bado watu wanahitaji usafiri, plus Hiyo meli itapelekwa Ziwa jingine lolote kama biashara itakuwa hakuna.
 
Mkuu hapa naongelea kipaumbele katika wilaya husika hizo sengerema na miswingwi hali yao ya uchumi ni mbaya na raia wao masikini sana.....kuliko hilo dalaja wangeziweka hizo pesa kwenye miradi ambayo inagusa maisha ya watu walio wengi

Miladi kama ipi?
 
President John Magufuli has officially inaugurated the construction of modern ship, shed and repairing of two ships.

The ceremony to lay foundation held today in the port of South Mwanza.

The projects costs TSHS 152 billions; the construction of the moder MV Mwanaza Hapa kazi Tu cost TSHS 89 billions, shed valued TSHS 36 billion, repairing of MV Victoria worth TSHS 22 billion and MV Butiama which value is TSHS 5 billion.

The new ship will have a capacity to take 1,200 people and that it's construction has reached 50 percent.

The government has already allocated TSHS 78 billion for the construction of those four projects.

Once completed, the projects will ease transportation in the Lake and that they will simplify movement of cargo between Tanzania, Kenya and Uganda.
 
Mungu Ni Mwema Wakati Wote
Nchi Na Vyote Viujazavyo Ulimwengu Ni Mali Ya Bwana
 
Mkoa wa Bukoba?
Kwahiyo kwasasa hizi nchi ulizotajwa azijaunganishwa na Tz
 
Sawa nijambo nzuri sana kupata maendeleo ila hicho nikipaumbele cha kanda ya ziwa kuna tatizo makubwa la kuvuka hapo kweli kiasi kwamba nchi itumie karibu 700bn......ambozo ingeziweka kwenye kilimo au afya na elimu hizo wilaya zingefaidika kuliko dalaja la kuvuka mgambo wakati kuna vivuuko zaidi ya vitano hapo busisi na Kamanga vipo vivuko.....
Akili zenu, mungu anajua. Kila hela iwekwe katika Afya, elimu! Huwezi kupata maendeleo kwa mawazo ya kijima kama haya
 
*DKT. JOHN POMBE MAGUFULI-RAIS WA TANZANIA*

#Kasi ya utekelezaji wa miradi hii inanipa matumaini kuwa miradi hii yote itakamilika kwa wakati na hivyo kusaidia kutatua tatizo la usafiri katika ziwa Victoria ndani na nchi za Uganda na Kenya

#Utekelezaji wa miradi hii yote, shukrani ziende kwa watanzania, ninyi ndio mmetoa mchango wa fedha zilizotumika kutekeleza miradi hii yote, sisi viongozi ni wasimamizi tu

#Utekelezaji wa miradi hii yote, shukrani ziende kwa watanzania, ninyi ndio mmetoa mchango wa fedha zilizotumika kutekeleza miradi hii yote, sisi viongozi ni wasimamizi tu

#Naipongeza sana Kampuni ya meli kwa kazi kubwa mnayoifanya na naunga mkono wazo lako Afisa Mtendaji Mkuu Bw. Eric Hamissi la kununua meli ya kwenda Comoro

#Wakandarasi mnaosimamia ujenzi wa miradi hii ninayoiwekea mawe ya msingi, hakikisheni mnatekeleza miradi hii kwa kiwango katika muda uliopangwa ikiwezekana hata kabla ya muda huo

#Nawapongeza watu wa kanda ziwa kwa kuendelea kupiga vita uvuvi haramu, sasa samaki wakubwa na wazuri wameanza kupatikana



*MHANDISI ISACK KAMWELWE-WAZIRI WA UJENZI,UCHUKUZI NA MAWASILIANO*

#Tayari tumekamilisha ukarabati wa bandari ya Kemondo, Bukoba, Musoma na bandari mpya ya Nyamirembe

#Tunakushukuru Mhe. Rais Maagufuli kwa kukubali kuwa mgeni rasmi katika uwekaji wa mawe ya msingi katika miradi hii ya ujenzi wa Chelezo, Meli mpya na ukarabati wa meli ya Mv Victoria na Butiama


*JOHN MONGELA- MKUU WA MKOA WA MWANZA*

#Mhe. Rais Magufuli tunashukuru kwa heshima hii kubwa uliyotupa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, sisi tutaendelea kufanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu na kuitumia miradi hii kujiletea maendeleo



*ERIC HAMISSI-FISA MTENDAJI MKUU KAMPUNI YA HUDUMA ZA MELI*

#Gharama za Mradi huu ni USD milioni 39 ambazo ni sawa na Tsh. Bil 89.7 na mpaka sasa tumeshalipa Tsh Bil. 39.2 sawa na 43.7% na ujenzi unatarajiwa kuchukua miezi 24 hadi kukamilika kuanzia Januari 2019 na tutakabidhiwa meli hii Januari 2021

#Meli mpya itakuwa ni kubwa kuliko meli zote nchini na nchi jirani katika ukanda wa Maziwa Makuu, itafanya safari zake kati ya Mwanza na Bukoba kupitia bandari ya Kemondo pia Mwanza na Musoma, na safari kati ya Mwanza na nchi jirani za Kenya na Uganda

#Jiwe lingine la Msingi litahusu uzunduzi wa ukarabati wa meli za Mv Victoria na Mv Butiama, haya yote yametokana na msukumo wa Serikali ya awamu ya tano

#Jiwe lingine la msingi ni ujenzi wa Chelezo itakayotumika kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya na matengenezo yake, yenye uwezo wa kubeba meli ya uzito wa tani 4000, pia itafanya matengenezo ya meli zote katika ziwa Victoria kwa makubaliano ya kibiashara

#Hafla hii ya leo ni ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa meli mpya ya abiria na mizigo katika ziwa victoria, yenye uwezo wa kubeba abiria 1200, tani 400 za mizigo, magari makubwa 3 na madogo 20

#Tunakushukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuwezesha ndoto ya muda mrefu ya kuwa na usafiri wenye ufanisi mkubwa, salama na uhakika katika ziwa victoria
 
Back
Top Bottom