Yaliyojiri Mahakamani kesi ya Mbowe na wenzake: Upande wa Utetezi waanza kutoa ushahidi. Kesi yaahirishwa mpaka 26 Novemba, 2021

Nimesha gundua we ni shabiki tu huna hoja, kabisa hapo kabatali alicho ongelea kina mashiko.
 
ha ha ha, yamewakuta nao kuhusu Content.
 
Kesi imeisha
1. wamekiri kukusanywa na kumfahamu Mbowe
2. wamekiri kwenda Moshi
3. wamekiri kufanya mikutano na Mbowe kwenye maeneo yanayomilikiwa na Mbowe
Hizo ni ingridient za kesi ya Jamhuri
Kwaio hizo ingridients ndo zinaleta nia ya kufanya ugaidi? Intent to commit terrorism mdogo wangu umesoma chuo gani?
 
shahidi kafundishwa kuja kusema maneno ya kutia huzuni mahakamani akifikiria yatamuokoa yaani hata aseme alilishwa mavi jela iko palepale hao ni magaidi
Hiyo ni lugha ambayo imekuwa ikitumiwa sana na watesi/madhalimu na HASA mawakala wao, ILI kutisha wapigania haki.
Ninaamini kuwa hilo ni SWALA la muda tu, kwani ukweli na haki ndio vitakujashinda na hatimae kutawala taifa hili. AMEN
 
Mawakili wa Mbowe na wenzake wamepelekewa moto wanakula matapishi yao

Jaji: endelea tu, Nimesha andika hicho Ulichosema

WS Abdallah Chavula: Asante Mheshimiwa Jaji

WS: Mheshimiwa Jaji Shahidi amesema Kwamba alimuelekeza Wakili Wa Mshtakiwa Wa Tatu, Wakili wa Mshtakiwa wa Nne akaalikwa na Wakili wake

WS: Akayatoa Yale ambayo alitaka Yafanywe na Wakili wake, Katika Hali ya Kustaajabisha, Katika Uandishi wa Barua ambayo yeye alielekeza Haikuandikwa na yeye wala Wakili wake Bwana Fredrick Kihwelo, Ikaenda Kuandikwa na Bw. Kibatala, Wakili wa Mshtakiwa Wa Nne

WS: Mheshimiwa Jaji Sote tunafahamu, Awali Kaka zetu na Dada zetu Wasomi MAWAKILI Walikuwa wanawatetea washtakiwa Wote wanne Kwa umoja wao, Waliacha Kuwatetea Washtakiwa wote kwa Umoja wao Baada ya Kuonekana Kuna Mgongano wa Kimaslahi..

Kwamba Hivyo hawawezi Kuwatetea Washtakiwa Wote Kwa Pamoja bila Kuacha Athari..

Wakili Fredrick Kihwelo: Mheshimiwa Jaji Tunamuomba Kama ana meneno Mengine ya Kutumia atumie, Hicho anachokisema Siyo Jambo Letu....

Wakili Peter Kibatala: Kama ana submit Pingamizi Jipya hapo Lisajiliwe kuwa ni Pingamizi Jipya, kwa sababu Sisi tunaguswa Kama Upande wa Mshitakiwa Wa Nne....

WS: Mheshimiwa Jaji Hakuna Pingamizi Jipya Hapo, Na Amri ya Mahakama ipo wazi Kwamba palikuwa na Mgongano Wa Maslahi ya Haki za wateja
 
Inasikitisha Judge anavyoonyesha waziwazi kuwagandamiza kina Mbowe! Inasikitisha kwamba kumbe askari wa JWTZ, tena makomandoo wanaweza kusingiziwa, kunyanyaswa, kuonewa na hata kudhulumiwa na polisi wenye rekodi chafu ya utumishi kama Mahita baba na sasa kwa bahati mbaya sana, Mahita mtoto, kina Jumanne na wengine bila consequence? Hivi polisi wanaoweza kutenda uovu huu kwa wanajeshi kwa raia wa kawaida itakuwaje? Kuna lutakalofuata stay tuned.
 

Mkuu kila anayependa haki na kulitakia taifa mema anajiuliza Hilo swala ulilojiuliza hapo. Ni Mambo ya Aibu na kusikitisha sana. Alafu wanajiona wanaweza kufanya chochote wanachotaka. Na kwamba wanaweza kujitawala pasipo MUNGU. Ndiyo maana wanapanga Maovu. Kutesa .kuteka na kuuwa watu.
 
Kesi imeisha
1. wamekiri kukusanywa na kumfahamu Mbowe
2. wamekiri kwenda Moshi
3. wamekiri kufanya mikutano na Mbowe kwenye maeneo yanayomilikiwa na Mbowe
Hizo ni ingridient za kesi ya Jamhuri
Haswaaaa,kesi imeisha kabisa,ni mvua za kutosha tu!
 
Duh..huyo jaji sio poa.
Ni kama tayari ameshaandika hukumu hivyo saivi anatimiza formality tu.
 
Kesi imeisha
1. wamekiri kukusanywa na kumfahamu Mbowe
2. wamekiri kwenda Moshi
3. wamekiri kufanya mikutano na Mbowe kwenye maeneo yanayomilikiwa na Mbowe
Hizo ni ingridient za kesi ya Jamhuri

Wamekiri kufanya ugaidi...!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…