Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,276
Wabunge, Freeman Mbowe wa jimbo la Hai na Esther Matiko wa jimbo la Tarime Mjini wameshafikishwa mahakamani kusubiri kuanzwa kusikilizwa kwa rufaa yao.Timu ya waandishi tutakuwaletea kile kinachojiri kutoka mahakamani
Updates
Mbunge wa Jimbo la Hai ambaye pia Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe Freeman Mbowe akiwa Mbunge mwenzake Esther Matiko wakiwa kizimbani tayari .
Mahakama Kuu kesho tarehe 07.03.2019 majira saa saba itatoa maamuzi ya rufaa ya dhamana ya Mhe Freeman Mbowe pamoja na Mbunge Esther Matiko
Mahakama Kuu baada ya kusikiliza hoja za rufani kwa pande zote mbili kwenye kesi ya Mbowe na Matiko imesema itatoa uamuzi wake kesho saa 7:00mchana.
======
*Update, uamuzi rufaa ya Mkiti Mbowe na Matiko Machi 7, 2019*
Mahakama Kuu Masijala ya Dar es Salaam kesho Alhamis Machi 7, 2019 inatarajiwa kutoa hukumu kwenye maombi ya rufaa yaliyowasilishwa mahakamani hapo na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa (Mb) na Esther Matiko (Mb) wakipinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwafutia dhamana kwenye kesi na. 112/2018 inayowakabili baadhi ya voingozi wakuu wa Chama na wabunge 7 wa CHADEMA.
Uamuzi huo wa kutoa hukumu kesho Machi 7, umetolewa leo mahakamani hapo na Jaji Rumanyika, baada ya Mahakama Kuu kusikiliza hoja za pande zote mbili katika shauri hilo, upande wa warufani (utetezi) na wajibu rufaa (Jamhuri).
Pamoja na masuala mengine, upande wa warufani uliwasilisha hoja kubwa mbili ambapo umeieleza mahakama hiyo kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilikosea kufuta dhamana ya wakata rufaa wakati walikuwepo mahakamani.
Hoja nyingine ni kwamba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilikosea kufuta dhamana prematurely, kabla ya kusema lolote kuhusu amana za wadhamini ambazo hadi sasa ziko pending.
Upande wa wakata rufaa pia umehoji uhalali wa viapo vya upande wa mashtaka walivyowasilisha mahakamani Kisutu kujenga hoja za kuiomba mahakama iwafutie dhamana washtakiwa hao huku upande wa utetezi ukinyimwa nafasi ya kujibu hati kinzani.
Baada ya Mahakama Kuu kusikiliza hoja za pande zote mbili, wakata rufaa na wakatiwa rufaa, Rumanyika J aliamuru kuwa mahakama itatoa uamuzi wake siku ya Alhamis, Machi 7, mwaka huu, saa saba mchana.
*Tumaini Makene*
*Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano*
*CHADEMA*