Yaliyojiri Mahakama Kuu kwenye rufaa ya Mbowe na Esther Matiko - Machi 6, 2019

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Wabunge, Freeman Mbowe wa jimbo la Hai na Esther Matiko wa jimbo la Tarime Mjini wameshafikishwa mahakamani kusubiri kuanzwa kusikilizwa kwa rufaa yao.Timu ya waandishi tutakuwaletea kile kinachojiri kutoka mahakamani

Updates

Mbunge wa Jimbo la Hai ambaye pia Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe Freeman Mbowe akiwa Mbunge mwenzake Esther Matiko wakiwa kizimbani tayari .
Mahakama Kuu kesho tarehe 07.03.2019 majira saa saba itatoa maamuzi ya rufaa ya dhamana ya Mhe Freeman Mbowe pamoja na Mbunge Esther Matiko
IMG-20190306-WA0003.jpg

Capture.PNG

Mahakama Kuu baada ya kusikiliza hoja za rufani kwa pande zote mbili kwenye kesi ya Mbowe na Matiko imesema itatoa uamuzi wake kesho saa 7:00mchana.

======

*Update, uamuzi rufaa ya Mkiti Mbowe na Matiko Machi 7, 2019*

Mahakama Kuu Masijala ya Dar es Salaam kesho Alhamis Machi 7, 2019 inatarajiwa kutoa hukumu kwenye maombi ya rufaa yaliyowasilishwa mahakamani hapo na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa (Mb) na Esther Matiko (Mb) wakipinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwafutia dhamana kwenye kesi na. 112/2018 inayowakabili baadhi ya voingozi wakuu wa Chama na wabunge 7 wa CHADEMA.

Uamuzi huo wa kutoa hukumu kesho Machi 7, umetolewa leo mahakamani hapo na Jaji Rumanyika, baada ya Mahakama Kuu kusikiliza hoja za pande zote mbili katika shauri hilo, upande wa warufani (utetezi) na wajibu rufaa (Jamhuri).

Pamoja na masuala mengine, upande wa warufani uliwasilisha hoja kubwa mbili ambapo umeieleza mahakama hiyo kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilikosea kufuta dhamana ya wakata rufaa wakati walikuwepo mahakamani.

Hoja nyingine ni kwamba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilikosea kufuta dhamana prematurely, kabla ya kusema lolote kuhusu amana za wadhamini ambazo hadi sasa ziko pending.

Upande wa wakata rufaa pia umehoji uhalali wa viapo vya upande wa mashtaka walivyowasilisha mahakamani Kisutu kujenga hoja za kuiomba mahakama iwafutie dhamana washtakiwa hao huku upande wa utetezi ukinyimwa nafasi ya kujibu hati kinzani.

Baada ya Mahakama Kuu kusikiliza hoja za pande zote mbili, wakata rufaa na wakatiwa rufaa, Rumanyika J aliamuru kuwa mahakama itatoa uamuzi wake siku ya Alhamis, Machi 7, mwaka huu, saa saba mchana.

*Tumaini Makene*
*Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano*
*CHADEMA*
 
Hili jambo limenishangaza mno ! hivi ni kwanini lakini ? Bunduki nje nje , wamelenga kumtisha nani ?

Tumechoka sasa na hili neno la Ulinzi Mkali kwani kila mara wakipelekwa tu hapo Kisutu lazima mliseme. Ulinzi ukiwa siyo Mkali na likitokea la kutokea hapo tena mtakimbilia hapa hapa kusema kuwa Tanzania haina Ulinzi. Waswahili tuna taabu na matatizo katika uwezo wa Kufikiri, Kuchanganua na Kutatua mambo Kihoja na Mantiki. Na wala haiitaji ' akili ' kubwa kujua ni kwanini kwa Watu maarufu na wakubwa kama hao Ulinzi huwa unakuwa ' beefed up ' kama hivyo. Na huwa siyo kwa hao tu Wanasiasa bali kama uko makini hata akina Habinder Seth na James Rugemalira au Malinzi na Mwesigwa wa TFF nao wakipelekwa hapo hali huwa siyo tofauti na hiyo. Tupunguze Majungu na ' Uanaharakati ' wa Kipumbavu unaongozwa na Chuki tu za Siasa zetu na tuache Sheria ichukue mkondo wake na kama ni kutoka watatoka tu hata kama kuna Watu watabana.
 
Swadakta!,akirudi kujibu maelezo haya ujue ana kifafa cha ubongo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom