Yaliyojiri Mahakama Kuu kwenye rufaa ya Mbowe na Esther Matiko - Machi 6, 2019

GENTAMYCINE ..... " maarufu na wakubwa kama hao Ulinzi huwa unakuwa ' beefed up ' kama hivyo. Na huwa siyo kwa hao tu Wanasiasa bali kama uko makini hata akina Habinder Seth na James Rugemalira au Malinzi na Mwesigwa wa TFF nao wakipelekwa hapo hali huwa siyo tofauti na hiyo. Tupunguze Majungu na ' Uanaharakati ' wa Kipumbavu unaongozwa na Chuki tu za Siasa zetu na tuache Sheria ichukue mkondo wake na kama ni kutoka watatoka tu hata kama kuna Watu watabana".

Mwisho wa kunukuu
 
Dhamana ya Mbowe na Matiko ilifutwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kile kinachotajwa kuwa walikiuka masharti ya dhamana kwenye kesi ya jinai inayowakabili pamoja na viongozi wengine waandamizi Wa CHADEMA.
Hapo unaongea kama mlei. Dhamana ilifutwa baada ya mahakama kujiridhisha pasi na shaka kuwa mbowe na matiko walikiuka masharti ya dhamana.
 
Ewe Edward Ngoyai Lowassa, nimekuita kwa majina yako ninayo yafahamu, nakuomba kesho uende ukamsalimie FREEMAN MBOWE, kule mahakamani. Hapo, utathibitisha kuwa, kuwa vyama tofauti si ugomvi. Na hasa ukizingatia kuwa, huko nyuma ulikuwa unakwenda mahakamani kuwajulia hali!
Lowasa ni mnafiki tu
 
..nilisoma jinsi Yericko Nyerere alivyokamatwa nilishangaa na kusikitika.

..inajulikana he is not a violent criminal lakini anakamatwa kwa namna ambayo unaona ajali inaweza kutokea na kusababisha madhara makubwa.
Ndugu yangu nchi hii acha tu, ajabu kisutu nilifikishwa ving'ora vya msafara kabisa utadhani gaidi kumbe ni mkulima wa bamia mbutu tu ambapo Siro angenipigia simu kwa vocha ya jero tu ningefika central na kwenda mahakamani hata kwa mguu tu.... Nchi ina siasa kali sana kuliko kitu chochote kile
 
Mahakama Kuu Masijala ya Dar es Salaam kesho Alhamis Machi 7, 2019 inatarajiwa kutoa hukumu kwenye maombi ya rufaa yaliyowasilishwa mahakamani hapo na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa (Mb) na Esther Matiko (Mb) wakipinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwafutia dhamana kwenye kesi na. 112/2018 inayowakabili baadhi ya voingozi wakuu wa Chama na wabunge 7 wa CHADEMA.

Uamuzi huo wa kutoa hukumu kesho Machi 7, umetolewa leo mahakamani hapo na Jaji Rumanyika, baada ya Mahakama Kuu kusikiliza hoja za pande zote mbili katika shauri hilo, upande wa warufani (utetezi) na wajibu rufaa (Jamhuri). Pamoja na masuala mengine, upande wa warufani uliwasilisha hoja kubwa mbili ambapo umeieleza mahakama hiyo kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilikosea kufuta dhamana ya wakata rufaa wakati walikuwepo mahakamani.

Hoja nyingine ni kwamba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilikosea kufuta dhamana prematurely, kabla ya kusema lolote kuhusu amana za wadhamini ambazo hadi sasa ziko pending.

Upande wa wakata rufaa pia umehoji uhalali wa viapo vya upande wa mashtaka walivyowasilisha mahakamani Kisutu kujenga hoja za kuiomba mahakama iwafutie dhamana washtakiwa hao huku upande wa utetezi ukinyimwa nafasi ya kujibu hati kinzani.

Baada ya Mahakama Kuu kusikiliza hoja za pande zote mbili, wakata rufaa na wakatiwa rufaa, Rumanyika J aliamuru kuwa mahakama itatoa uamuzi wake siku ya Alhamis, Machi 7, mwaka huu, saa saba mchana.
 
Mkuu Froida swali langu halihusiani na hayo unayosema! Spika alitoa ruhusa kwa Mh Matiko kufanya kazi ya kamati ya bunge. Issue ni kwanini mahakama imuone Mh Matiko kadharau masharti ya dhamana wakati ana barua ya Spika? Jibu langu likawa ni kutokana na mahakama kutojulishwa na kutoa ruhusha kwa Mh Matiko kusafiri kikazi hivyo kukiuka masharti ya dhamana. Ndiyo hayo mkuu sina linguine.

Spika ni shetani ni lucifel huyo mama mwenye watoto wadogo amwewekwa ndani kwa sababu ipi kwani mtu alitumwa na spika na barua iliandikwa kwa nini anadharauliwa kwa sababu kawa kibaraka wa mihimili mingine spika kaisha kawa dembe dembe hopeless kabisa utafikiri atakuwa spika milele mpuuzi sana
 
Mkuu Froida swali langu halihusiani na hayo unayosema! Spika alitoa ruhusa kwa Mh Matiko kufanya kazi ya kamati ya bunge. Issue ni kwanini mahakama imuone Mh Matiko kadharau masharti ya dhamana wakati ana barua ya Spika? Jibu langu likawa ni kutokana na mahakama kutojulishwa na kutoa ruhusha kwa Mh Matiko kusafiri kikazi hivyo kukiuka masharti ya dhamana. Ndiyo hayo mkuu sina linguine.

Je mitatu mahakama bado haikuendelea kujua kwamba huyo Matukio alipewa ruhusa na spika? Tukisema rais anazitumia mahakama kukomoa wapinzani wake tunakosea?
 
Mkuu swala sio kupewa ruhusa na Bunge bali kufuata utaratibu wa mahakama kuhusu masharti ya dhamana. Sio kazi ya mahakama kuangalia nani kapewa ruhusa bali mshitakiwa mwenyewe kuijulisha mahakama kuwa amepewa ruhusha na kuiomba ruhusa. Ni kweli kulikwa na maswali mengi kuhusu maamuzi ya mahakama kufuta dhamana.

Hamna cha ruhusa wala nini bali mahakimu wasio na weledi kutii maagizo machafu ili wapandishwe vyeo. Sasa na hiyo mahakama kuendelea kuona ni sawa kesi iliyoko mahakamani mtuhumiwa kuendelea kuripoti polisi kila wiki huoni bado ni ushenzi huo huo?
 
Mkuu nimeisha sema incompetence ya Hakimu ni swala kuhimu ila narudia mahakama haihusiki na ruhusa ya Ndugai. Eti Ndugai akitoa ruhusa basi na masharti ya dhamana hayapo.

Mkuu hiyo barua ya ruhusa ya bunge ilitumika kama sehemu ya utetezi na ilikuwa na mashiko lakini hakimu aliipotezea, kwakuwa mkulu alishatoa maagizo nyuma ya pazia wapinzani wakomolewe.
 
Back
Top Bottom