Kusema kweli mimi najiuliza lkn jibu sijapata... Hivi ktk wizara ya mambo ya ndani hakuna hata mtu mmoja wa kutoa ushauri mzuri ili kuepusha aibu ktk kushughulikia suali hili? Hivi waziri mkuu Mh Pinda (kidogo namwona anatumia kichwa kufikiri) hakuliona tatizo katika uamuzi huo, na kuzuia hatua za kisiasa kuchukuliwa? Hivi ktk chama chetu kinachotawala, hakuna hata mmoja, mwenye busara, wa kutahadharisha kuwa siasa isiingizwe ktk sheria? Hivi na huko bungeni mwenye hekima kuliko wote ni Bi Makinda peke yake? Mbona maamuzi ya aibu yanazidi kujiorodhesha ktk siasa za Tanzania? ... vyombo vya habari vimeripoti kuwa; taarifa, pamoja na uthibitisho vimepelekwa Uingereza, nchi ambayo ni colonial master wetu! Tukumbuke kuwa, budget yetu bado ni tegemezi kutoka huko na nchi zingine, Uingereza ina ushawishi mkubwa duniani, NATO, WB, IMF, nk je wakitugeuzia kisogo tutakimbilia wapi kesho? Leo nimeamini usemi wa wahenga, sikio la kufa.... Pole Tanzania!!!!!!!