Naibu Waziri Mkuu Dkt. Biteko afichua orodha ya matendo ya uhujumu wa miundombinu ya TANESCO

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Hizi hapa Nukuu za Dkt. Biteko akifichua Mtao wa uhujumu miundombinu

1. ’'Tarehe 13 mwezi wa pili mwaka 2024, BAGAMOYO alikamatwa mtu mmoja pale akiwa na Lita 80 za mafuta ya Transfoma, kesi imefunguliwa, maana yake ile Transfoma imekufa mafuta yamesha chukuliwa’’

2. ‘’Mwezi wa tatu tarehe tatu ubungo maziwa Dar es Salaam, amekamatwa mtu jina ninaye hapa akiwa na lita 400 za mafuta ya Transfoma kesi inaendelea na upelelezi unaendelea’’

3. ‘’tarehe moja mwezi tatu Keko Dar es salaam, mwananchi mmoja amekamatwa na kilo 50 za Nyaya ya shaba zenye thamani ya shilingi laki saba na Hamsini, na hawa kuna kiwanda kimoja kila tukio la waya unaona walikuwa wanaenda kushusha kwenye kiwanda hicho, kwa sababu tuko katika upelelezi sitaki kuki disclose. Hawa nao kesi inaendelea’’

4. ‘’baadae Kilo 361 za Nyaya zenyewe zimekamatwa, wapi keko Dar es salaam , keko hiyo hiyo kilo nyingine 1105 zimekamatwa na zilikuwa zinapelekwa kwenye kiwand kile kile zinaenda kuuzwa, zenye thamani ya shilingi milioni 16,575,000/=’’.

5. ‘’Mwezi wa tatu Dar es salaam Keko, kilo 57 za shaba, Bunju Dar es salaam na kwenyewe amekamatwa mtu mmoja lakini ana material zenye thamani ya shilingi milioni 200 mali ya Tanesco kesi inaendelea na upelelezi unaendelea’’.

6. ‘’Tarehe 17 mwezi wa tatu, sisi tupo kwenye maombolezo wenyewe wanaiba, Kigamboni na huyu ni mfanyakazi wetu wa muda maalum anaitwa Hussein Yusuph Rashidi wa kigamboni kaiba copper wire roller nzima na transfoma iliyokuwa kwenye matengenezo ameenda kuuza apate hela. Kesi ipo Mahakamani’’.

7. ‘’Ubungo maziwa tena huyu sio mfanyakazi wa Tanesco , wameiba transfoma tatu kesi inaendelea’’

8. ‘’ Tarehe 21 mwezi wa tatu, Fukayosi kule Bagamoyo wakazi hawa wamekutwa na lita 75 za mafuta ya transfoma, kesi bado iko kwenye upelelezi’’

9. ‘’ 17 mwezi wa tatu, mkuranga huko na kwenyewe mtu mwengine ameenda, transfoma nne zenyewe wameenda kuzichukua kesi iko mahakamani’’

10. ‘’ukienda chalinze wamekutwa na Nyaya za aluminium ambazo zilikuwa ni mali ya ETDCO na kwa kweli hapa na penyewe kuna mtu mmoja mdau wa ETDCO ndio mtengeneza mchongo’’.

11. ‘’Sasa juzi tumeenda kumpekua mtuhumiwa mmoja juzi tu hapa tarehe 25 sitaki kumtaja wamemkuta na vitu vya Tanesco nyumbani kwake, mita anazo nyumbani, ana lakiri (seals) nne na zina namba ya shirika, huyo bwana maeneo ya chanika kule akakutwa na lakiri (seals) 221 zenye nembo ya shirika, amekutwa na rimoti units 37 , hawa watu wote wana connection na watu waliomo ndani ya shirika’’

‘’Sasa katika mazingira kama haya iko michongo mingine ambayo wafanyakazi wetu ndio wanashirikiana na wahalifu hawa’’. Amesema Dkt. Biteko

‘’sasa ninafahamu kuwa wapo wengine wapo mahakamani wapo wengine wako kwenye upelelezi, lakini mimi najiuliza mfanyakazi wa shirika la Tanesco aliyekamatwa redhanded (kidhibiti mononi) na vifaa, ni kweli kuna taratibu za kipolisi na upelelezi unaendelea kwa sababu ni lazima kutafuta haki ya mtu. Wewe MD wa Tanesco, una Imani gani na mtu wa namna hiyo ambaye yeye alikutwa na gari anaiba waya, una Imani gani naye?, halafu unaniambia eti kuna taratibu za kiutumishi mpaka zikamilike’’. Ameongeza

‘’lakini haya majizi yote, awe na connection (maana one of the thing kinachosumbua hapa ni connection zenu za mjini hapa) hatuwezi kuendekeza connections za watu huku watu hawana umeme, haiwezekani. Hawa wote walio kwenye hii taarifa, wako kwenye upelelezi, kwenye utumishi wa umma huku waweke pembeni watasubiri mkondo wao wa kisheria huko utakavyokuwa unaendelea’’. Amesisitiza Dkt Biteko.
1711752126290.png
Screenshot 2024-03-30 014140.png
Chanzo: Jamvi la Habari
 
Si huyo mama yenu anasema yeye awezi kufoka. Ukicheka na nyani, utavuna mabua.

Watanzania sio watu wakuchekea kabisa zinahitajika jitihada za makusudi kuwabadilisha fikra asilimia kubwa ya watanzania ata wasio wezi.

Generally speaking kama nchi kuna asilimia kubwa sana ya watanzania ambao mtazamo wao wa maisha ni unique ukitoka nje ya nchi 90% ya watanzania awawezi urafiki na watu wa nchi nyingine ata hizi za jirani.

Anahitajika mtu wa kubadili fikra, na hawezi kuwa popular akubali tu matusi vinginevyo mafanikio ya haraka kwenye maendeleo sahau.
 
Upuuzi mtupu, sababu alizotoa sio sababu ya Kuwa na mgawo nchi nzima, mafisadi serikalini na incompetents wa TANESCO ndio sababu ya kukosa umeme, aache kusingizia hao vibaka wa nyaya za umeme na mafuta ya Lita 80, Wana uwezo wa kulipa watu minimum wage wakalinda hizo transformer na nyaya za umeme nchi nzima, aongee ukweli tatizo liko wapi sio siasa na visingizio Kila siku
 
Kama kwa muda mfupi tu ameweza kuwabaini wote hao wakati polisi wapo na hawajaweza basi huyu ni nabii
 
Nyie si mnasema kipindi cha magufuli alivyokua mkali alilazimisha mitambo kufanya kazi mpaka sahv imeharibika

Anyway, Ahsante sana Mama kutuvumbulia wezi
 
Mwambieni Biteko TANESCO Magomeni kuna wafanyakazi vishoka kwa malipo kidogo ama wanacheza mita au kukufungia by pass kabisa kuzungukuka nje ya Luku mwezeshaji yupo karibu na ofisi ya Afisa Usalama jina linaanza na F
 
Pathetic, afichua! Ye ye ni polisi, takukuru? Inatusaidia ni ni?
Polisi, takukuru, tiss walikuwa wapi? Ndio maana tunasema mi CCM, imeshindwa kazi, kwanini matukio yafanyike, ndio wanakurupuka? Kuanzia ikulu kuna panyabuku, mpaka kwenye kata.
 
Mfanyakazi badala ya kutafuta njia nyingine ya kipato nje ya ajira anaigeuza ofisi yake kuwa investment yake.
 
We Biteko hao wahusika wamekwamisha uchumi was nchi!!

Tumeunguza vifaa vya gharama tumeshindwa kufanya biashara Sasa unasemaje eti wawekwe pembeni kwanza Sheria ichukue mkondo wake!!?

Hao wangepelekwa mahabusu ya kijeshi kwanza wakafundishwe uzalendo wakati hayo yanaendelea!!

Huo ni uhaini!!
 
Mwambieni Biteko TANESCO Magomeni kuna wafanyakazi vishoka kwa malipo kidogo ama wanacheza mita au kukufungia by pass kabisa kuzungukuka nje ya Luku mwezeshaji yupo karibu na ofisi ya Afisa Usalama jina linaanza na F
Duh..ngoja tufatilie. Asante sana mkuu!
 
Back
Top Bottom