Yaliyojiri kwenye mazishi ya Sumari

Mungu amrehemu lakini hakuna cha kumkumbuka alichofanya akiwa mbunge na waziri . Ole Medeye amalizie tu muda wake maana na yeye hatarudi bungeni kama mbunge wa kuchaguliwa 2015
 
Mungu amrehemu lakini hakuna cha kumkumbuka alichofanya akiwa mbunge na waziri . Ole Medeye amalizie tu muda wake maana na yeye hatarudi bungeni kama mbunge wa kuchaguliwa 2015

Ole Medeye kinachompa kiburi ni kuwa kambi ya Lowasa

hata unaibu waziri, alimwombea kwa J.K
 
Marry Nagu hakuwepo mkuu.... Mary nagu alikuwa kwenye matembezi yale wanyoita ya hisani ili kusaidia mama mjamzito ajifungue salama...hakuwepo kwenye mazishi...

JE DR SLAA NA KIKWETE WALISALIMIANA AU ALIMPIGA CHENGA KM IFAKARA
 
Mbona msiba wa huyu marehemu hapa JF haujapewa uzito mkubwa kama misiba ya waheshimiwa wengine?



Tumeandika sana hapa JF! Huyu Mheshimiwa alianza kuugua muda mfupi baada ya kampeni kuanza! Chama na Serikali vikamtelekeza kitandani kwa muda wote hadi mwanzoni mwa mwaka huu, mtoa roho alipoizungukia roho yake, na kelele za kuhoji kutelekezwa kwakeke ndio wakampeleka India. Wakati wenzake waliopelekwa huko walipatiwa huduma hadi wakapata nafuu ndio wakarudishwa nyumbani, yeye alirudishwa akiwa bado mgonjwa vilevile na kupelekwa Muhimbili kwenda kumalizia uhai wake!

Baada ya kifo chake, barabara zimepigwa greda, bendera za chama zimepamba maeneo yote na mkuu wa kaya ameongoza viongozi wenzake wa chama na serikali waliomtelekeza wakati anaumwa kwenda kumzika. Ni unafiki mtupu!?

Ndio maana waungwana wamekaa kimya washirikishwe kwenye unafiki. Na wewe umeona msiba haupewi uzito. Ukweli ni kwamba hawataki kujiingiza kwenye unafiki huu!

Ni hayo tu!
 
ukweli ni kwamba kapeni zimeshaanza maana leo mida ya asubuh wakati ninakwenda kwenye mihangaiko ya kutafuta chochote niliona magari ya ccm yakiwachukua wanachama wake maeneo ya makao mapya na ngarenaro hapa arusha,,, nilishuhudia wengine wakipewa tshirt na hela ili waendeke kwenye msiba.... so ulikuwa ni uwanja wa siasa na si mazishi....
 
Tangulia Sumari, ukikutana na mwl mwambie Zenj pana serikali ya umoja wa kitaifa, na serikali ilikata rufaa juu ya mgombea binafsi. Haki ya mtz kuchagua na kuchaguliwa imebakwa kwa sehumu.
Msalimie Prof Haroub, mwambie msamiati wa tume huru ya uchaguzi haujaeleweka kwa watawala wetu.
Kampumzike kwa amani.
 
hii nayo ilipatikana nyumbani kwa marehemu sumari.....muone wasira anavyowaangalia


Jicho la Wasira ni la kutoamini amini kinachotokea mbali ya upeo wake...heheh kidogo acheke! kumbe mshikaji naye handsome! teh theh
 
Back
Top Bottom