Yaliyojiri kwenye mazishi ya Sumari

Tumemsubiri sana JK Arusha baada ya mazishi, mpaka muda huu hatuamini kabisa kama anaweza akawa ameondoka mjini hapa bila hata ya salamu kwa Wana Arusha!
Mbona Morogoro alitembelea sehemu kadha, ikiwa ni pamoja na kuzindua madaraja akijiandaa kwenda kumzika mar.Regia?


ashafika dar zaid ya lisaa na nusu...yeye hajipendi kwani?
 
mkuu hizo tisheti ni za Taasisi ya Madaktari wahitimu wa vyuo vikuu Tanzania (THPI) ..ndio walioandaa matembezi hayo

Matembezi hayo yalikuwa yanalenga nini hasa kwenye msiba wa huyu aliyekuwa mbunge jina?
 
mazishi ni mazishi2, mpaka avutie kiasi gani? Regia alivutia nafikiri watu walitaka kushuhudia mlemavu aliendeshaje gari mpaka akapata ajari? Zaidi ya hapo hakuna vingine ni vimbwenga vya cdm tuu, maana wao hata kwenye msiba ni siasa tuu
 
http://www.blogger.com/share-post.g...894691&postID=5979635530438087840&target=buzz


Jan 23

[h=1]Rais Jakaya Kikwete,Waziri Mkuu Mizengo Pinda,Spika Wa Bunge Anne Makinda Na Viongozi Mbalimbali Washiriki Mazishi Ya Aliyekua Mbunge Wa Arumeru(CCM)Jeremia Sumari[/h]

Written by haki | // 0 comments

IMG_0012.JPG

Wananchi wa Arumeru kwa kushirikiana na vijana wa UVCCM taifa wakiufukia mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Arumeru mashariki Mhe. Jeremia Sumari wakati wa mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwao Akheri, Mkoani Arusha Leo
 
Waungwana napata sana shida kuamini ghafla kwa yaliyotamkwa na wana siasa na Viongozi wa CCM kwenye Maziko ya aliyekuwa Mbunge wa Arumeru (mashariki) Jerry S Sumari Kuwa ahadi zake zitatekelezwa na Serikali.

Siamini kama wanamaanisha wanachokiongea Hapa kinatoka Rohoni mwao na ndiyo utaratibu za kawaida, bali nashawishika kuona ni kampeni za ki aina kuhusu kupewa ridhaa katika jimbo hilo tena kupitia CCM..

Mbona kuna wabunge Hai wa CCM ahadi zao hawazitimizi au hadi nao wafe?

Jamani hebu tuwe wakweli na wastaarabu kuhusu kuwadanganya Watanzania, Wabunge mliopo humu mtusaidie kujua na kuchambua kauli za Pinda, Lukuvi na Mukama katika msiba Huu....
 
IMG_0117.JPG

Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Jeremia Sumari kabla ya kwenda kuzika kijijini kwao Akheri, Mkoani Arusha. Nyuma ni Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda na Spika mtaafu wa Bunge Mhe. Pius Msekwa
IMG_0123.JPG

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Jeremia Sumari kabla ya kwenda kuzika kijijini kwao Akheri, Mkoani Arusha Leo
 
Rest in peace Jerry Sumari,umetangulia nasi tunakuja.ee mungu utuongoe
 
Mbona msiba wa huyu marehemu hapa JF haujapewa uzito mkubwa kama misiba ya waheshimiwa wengine?

KWA NINI PIA HUKUHOJI KITENDO CHA TV NYINGI KAMA SI ZOTE KWA NINI HAZIKUONESHA MAZISHI YA THE LATE MH MTEMA KAMA ZILIVYOFANYA KWA HUYU MH SUMARI? nIMESHANGAA SANA NA KWAKWELI IMENISIKITISHA KUONA TBC1, STAR TV NA ITV LEO ZIKIONESHA KWENYE TAARIFA ZAO ZA HABARI LEO HII WAKATI YA MH MTEMA UKIONDOA MATUKIO YA WIKI WAMEONESHA.

JE NI KWA SABABU HUYU ALIKUWA KADA WA CHAMA CHA MAGAMB AMBAKO STAR TV, ITV NA HAKIKA TBC1 MMEENDELEA KUDHIRISHA KUWA NYIE WOTE MNAFANYA KAZI YA KADA
 
ole medei akiwakilisha wabunge wa arusha amempiga kijembe lema kwa kusema eti wabunge vijana wajifunze kutoka kwa marehemu sumari.

kwa jambo lipi lamaana ambalo sumari alilifanya katika jimbo lake na akiwa naibu waziri wa fedha,hakuna cha kujifunza kutoka kwa huyo marehemu hzo ni sifa za kijinga ambazo mara nyingi marehemu hupewa hata kama hastaili lakini husífa tu jamani tuwe makini na haya mambo.
 
Nawapa POLE nyote, lakini naomba kunyoshwa kumbukumbu, hivi Marehemu Sumari ALISHA WAPI APISHWA baada ya kuchaguliwa mara ya pili 2010?
 
waungwana napata sana shida kuamini ghafla kwa yaliyotamkwa na wana siasa na viongozi wa ccm kwenye maziko ya aliyekuwa mbunge wa arumeru (mashariki) jerry s sumari kuwa ahadi zake zitatekelezwa na serikali.

Siamini kama wanamaanisha wanachokiongea hapa kinatoka rohoni mwao na ndiyo utaratibu za kawaida, bali nashawishika kuona ni kampeni za ki aina kuhusu kupewa ridhaa katika jimbo hilo tena kupitia ccm..

Mbona kuna wabunge hai wa ccm ahadi zao hawazitimizi au hadi nao wafe?

Jamani hebu tuwe wakweli na wastaarabu kuhusu kuwadanganya watanzania, wabunge mliopo humu mtusaidie kujua na kuchambua kauli za pinda, lukuvi na mukama katika msiba huu....
Ukiona hivyo ujue ndiyo wameanza kampeni za uchaguzi wa mdogo wa ubunge utafanyika hivi karibuni.

Ccm wana waziwazi mkubwa na upinzani wa chadema hivyo wametoa kauli zao za kutoa ahadi.

Sasa wananchi wa hilo jimbo ndiyo watajua ama kusuka au kunyoa wakati wa kupiga kura utakapofika.

 
Tumemsubiri sana JK Arusha baada ya mazishi, mpaka muda huu hatuamini kabisa kama anaweza akawa ameondoka mjini hapa bila hata ya salamu kwa Wana Arusha!
Mbona Morogoro alitembelea sehemu kadha, ikiwa ni pamoja na kuzindua madaraja akijiandaa kwenda kumzika mar.Regia?



Mkuu,
Itamchukua JK miaka mingi sana kukatiza jijini Arusha. Ataishia kwenye viunga na wilaya za nje ya jiji, lakini kamwe hawezi kukatiza jijini! Hata kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu, alifika saa 12 jioni na alimpa Nakaaya kadi, akashuudia Batilda akijipigia debe bila kusema lolote akaondoka! Kumbe walikuja kukusanya watu wa kuwapeleka Karatu maeneo ya Monduli na Leguruki ili ionekane anakubalika huko kuliko Dr Slaa. Na magazeti kama kawaida yakaandika " kikwete aiteka Karatu!".

Anajua hakubaliki Arusha na hapa jijini wanamchukia na hakuna hata ahadi yoyote aliyowaahidi. Ndio maana hata yeye hathubutu kutia mguu jijini Arusha. Naamini hii itachukua muda wake wote uliobaki. Mtaniambia!
 
Naona habari zake hazijavutia jukwaa kama la Rejia!RIP SUMARI

Uwajibikaji wake kwa taifa,aina ya chama alichokuwa akikitumikia na amelifanyia nini taifa nje ya jimbo yake ndivyo huleta mvuto kwa watu.
R.I.P MP SUMARI
 
Back
Top Bottom