Yaliyojiri katika Uchaguzi Serikali za Mitaa - Dec 14, 2014

Wana JF
Habari zenyu bwana . Nipeni habari za mtaani kwenyu huko je ni mbaya kama hapa Kinyerezi ? Kata ya Kinyerezi eti imepokea karatasi na makabrasha ya kura za Kata ya Gerezani .Na Gerezani nadhani watakuwa wamepokea za Kinyerezi au Kata gani ila kwa kifupi kuna tatizo kubwa hadi muda huu niko kituoni hakuna kinacho endelea .

Hebu sema mtaani kwako kama wewe umesha wapa UKAWA kura tafadhali .
Haiwezekani kisiendelee kitu, acha uzushi
 
Uchaguzi serikali za mtaa:Baadhi ya wananchi wakiwa katika kituo cha Tabata wakiwa wamepanga foleni wakisubiria kuitwa majina yao ili waweze kupiga,ambapo halo ilitaka kibadilika miongoni mwa wapiga kura na viongozi wa uchaguzi na hivyo kutokea mivutano takribani dakika 5 hali iliyowaladhimu askari kuingilia kati kuzima mivutano hiyo.


Kwa mujibu wa baadhi ya wapiga kura wametuhumu kuwepo kwa hatufi ya hali ya udanganyifu wa kuitwa majina ya wapiga kura ambayo yanaitwa Mara


Mbili mbili huku wakidai kuwa hali hiyo itafanya kwamba watu wapige kura mara mbili mbili jambo ambalo si la kiungwana na litawakosesha wengine haki yao,na hivyo wengne kudai kwamba wapo watu wanao onekana kupiga kampeni Chini Chini wakati zoezi la kampeni lilishakwisha hvyo hali hiyo ilwashinda kuvumilia na kuamua kulikemea lisiendelee ili likaja kuharibu uchaguzi huu.


Imebainika kuwepo kwa baadhi ya wapiga kura ambao wanaonekana kupiga kura na wengine kujichanganya na watu ambao hawajapiga kura kutokana nakinachoonekana kutowekwa utatatibu thabiti wa wapigaji kura wakishamaliza kukaa sehemu maalumu,jambo ambalo hata wapigaji kura katika uchagizi huu wamekiri na kuliona.


Hata hvyo hali kwa sasa imetulia baada ya kuwepo askari kanzu kwaajili ya kuhakilisha zoezi linakwenda salama bila kitokea hali ya udanganyifu na fujo.
attachment.php
 

Attachments

  • p2.jpg
    p2.jpg
    95.9 KB · Views: 221
  • p2.jpg
    p2.jpg
    55.2 KB · Views: 897
Uchaguzi katika kijiji cha Kigadye jimbo la Kasulu vijijini umeahirisha mpaka utakapotangazwa tena, sababu jina la mgombea wa ACT kwa nafasi ya uenyekiti wa kijiji halimo katika karatasi ya kupigia kura
 
Kutoka Kigoma anaripoti kuwa Baadhi ya wapiga kura wa Kigoma Ujiji kata ya Rusimbi mtaa wa Kawawa kituo cha ofisi ya serikali za mtaa kawawa wamemshambulia kwa ngumi bwana Omari kutoka mtaa wa kaburini kwa kosa la kujaribu kupiga kura kituo na mtaa Rusimbi ambao sio mtaa wake.Anaendelea kuripoti kuwa hakuna ulinzi wowote katika eneo la tukio hadi sasa ingawa hali imeanza kutulia

10850136_315170405343600_2739765774035387421_n.jpg


10403634_315170448676929_4371499987844913515_n.jpg


Chanzo: LHRC
 
Hii ni Takwimu inayoonyesha Matukio ya Ukiukwaji wa taratibu kwa kila mkoa. Mpaka sasa kama unavyoona kwenye takwimu hizi mkoa wa Tabora unaongoza kwa ukiukwaji wa taratibu ukifuatiwa na Kagera wakati Shinyanga na Mbeya wakifanya vizuri
10491970_315158675344773_1307595399226685314_n.jpg
 
Dawa yao ni kuanzisha operation ondoa uhai {oou} kwa viongozi watakaopatikana kwa hila.
 
Hiki ni kituo cha kupigia kura kilichopo Majengo A kata ya Majengo Sumbawanga.Kilifunguliwa saa mbili lakini mpaka sasa saa tano vifaa havijafika

10390459_315169178677056_7766613784545228364_n.jpg
 
Kutoka Songea Mjini, anatuambia kuwa kata ya Misufini hadi sasa kura hazijaanza kupigwa kwa sababu fomu za kupiga kura nafasi ya uenyekiti wa mtaa zimechanganywa, kwani kwenye nembo ya CCM jina lililoandikwa ni la mgombea wa CHADEMA kama inavyoonyesha kwenye picha

10801870_315160458677928_8688034558725149839_n.jpg
 
Jipeni moyo hapa jf wakati huku mtaani CCM inachukua mitaaa kilaini sana,,njooni na sababu mpya hizi za kura kuibiwa imechuja,,hii ni salamu kwa 2015 na hivi mmejikusanya pamoja kama panya

Nawe jipe moyo kuwa mmesimama kumbe mnapumulia mashine.
 
Kutoka Songea Mjini, anatuambia kuwa kata ya Misufini hadi sasa kura hazijaanza kupigwa kwa sababu fomu za kupiga kura nafasi ya uenyekiti wa mtaa zimechanganywa, kwani kwenye nembo ya CCM jina lililoandikwa ni la mgombea wa CHADEMA kama inavyoonyesha kwenye picha

10801870_315160458677928_8688034558725149839_n.jpg

duuh,,,,,,hawa wana akili sana, kwa hiyo ukipiga kwa kuangalia chama unakuwa unampigia mgombea wa chama kingine.
 
Kutoka Geita Mjini kuna taarifa kuwa Kituo cha Msalala Road Geita Mjini, upigaji kura ulisimama kwa muda kufuatia vurugu kutokana na kutokuwepo na polisi kulinda usalama, sasa Polisi wamewasili.

LHRC
 
Back
Top Bottom