Yaliyojiri katika Uchaguzi Serikali za Mitaa - Dec 14, 2014

Watu ni wengi ajabu nime maliza wajibu wangu...
 

Attachments

  • 1418544260773.jpg
    1418544260773.jpg
    98.8 KB · Views: 260
Wadau hapo mlipo mahudhurio yakoje? Hapa wilayani kwetu mahudhurio ni mazuri sana--target itafika.
 
Wadau naomba niutaarifu umma wa watanzania kinachoendelea kwenye wilaya ya mvomero kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.
Mpaka sasa hakuna kituo hata kimoja ambacho kipo wazi kwa ajili ya watu kupiga kura. Hii imetokana na kukosekana kwa vifaa vya kupigia kura. Hakuna kifaa hata kimoja kilichofika toka kwenye ofisi ya mkurugenzi mtendaji wa wilaya.
Naomba wadau tusaidiane katika hili. Hapa kuna uchakachuaji utakaofanyika. Tujiandae wana ukawa kupinga matokeo haya.
 
Mccm yameanza kucheza rafu tunatarajia refa aokoo jaadhi kabla mechi ajavurujika wanaficha wino ili kutoa furusa ya watu kupiga kura mara mbili,refa asipookoa jahazi baadae tusilaumiane
 
Upinzani ulianza na kikapu kitupu wakati kikapu cha CCM kilijaa matunda.
kadiri siku zilivosonga mbele kikapu cha wapinzani kimeendelea kujaa huku kile cha CCM kikipungua maana matunda yaliyomo upande wa ccm huingia upande wa upinzani.
Huu ni ukweli ambao CCM hawapendi kuusikia.
Kwa kanuni hii ccm haiwezi kukua tena hadi itakapogeuka upinzani. ni suala la muda na spidi ya kukua kwa upinzani vitakavyo "determine" muda wa upinzani kuchukua nafasi.
Ving'ang'anizi wa ccm wakitambua hili wanaweza kuamua wasimameme upande upi kwa maana usafi wa mtu utaonekana popote na yeyote! Jambo muhimu ni kuondoa woga na kuacha unafiki!
 
hadi saa tatu hii asubuhi utaratibu wa kupiga kura hauleweki.. kuna chaos tu hapa..
*HAKUJABANDIKWA MAJINA YA WAPIGA KURA
*MPIGA KURA HAJUI ATAPIGA KURA KATIKA KITUO KIPI (MAJINA SI HAMNA)
*WANASOMA MAJINA KWA MDOMO RAIA MSIKILIZE MAJINA.YENU ..VITUO VITATU WASOMAJI WANATUMIA MDOMO ..NI MKANGANYO TUU.. HUJUI UMSIKILIZE MTANGAZA WA KITUO GANI..
*WAKO SEHEMU YA WAZI TU AMBAYO HATA KUBANDIKA MAELEKEZO NI NGUMU MNO... hili eneo lina mashule mengi tu walishindwa hata kuweka kituo cha uchaguzi katika shule moja wapo
*MISTARI INAPANGWA WASIMAMIZI WANAIVURUGUA NA WATU NI MAMIA..
......NI UGOMVI NA MAKELELE TUPU...kuna dalili zote za kupigwa ngumi hapa
............huu utaratibu sijawahi kuuona sehemu yoyote....mwenye namba ya watu wa tume ya taifa ya uchaguzi tafadhali aweke hapa tupeleke madai yetu kwao

Mkuu,komaeni nao hadi kieleweke! Ukiona hivyo ujue maccm yamejipanga kuchakachua maamuzi yenu
 
Kwenye mamlaka ya mji mdogo Mwanga
kitongoji kimoja cha Mwangondi
hakijafanya uchaguzi kwa upuuzi wa
msimamizi wa uchaguzi... Kwa maana hiyo
uchaguzi huwo utafanyike kipindi kingine
licha ya uhuni unaotaka kifanywa.
 
Katika hali ya kushagaza,uchaguzi wa serikali za mitaa katika kata ya Bulyanhulu katika kijiji cha Kakola umeahirishwa kwa sababu hadi sasa saa 5:13asubuhi hakuna karatasi za kupigia kura. Hari hii ipo pia Bugarama jirani tu na kata ya Bulyanhulu na hadi naandika huu uzi kikao cha kuahirisha upigaji kura kata ya Bugarama unaendelea.
Watu wamegadhabika sana si CHADEMA wala CCM kwani wengi wao wameahirisha safari zao ili kupiga kura halafu wanaambulia maneno toka kwa wasimamizi wa uchaguzi kama vile;msitulaumu sisi,mpigieni simu mkurungezi namba hizi hapa n.k.
NB: TAARIFA NIMEZIPATA MOJA KWA MOJA KUTOKA KWA MGOMBEA/ MTU WANGU WA KARIBU ALIYEKO MAENEO YA UCHAGUZI.
 
Ndugu nimepata taarifa za kusikitisha sana.. niana mdogo wangu pale CBE ansoma actually nilikuwa nataka kumtumasamewhere saivi alicho nambia nilitamani nilie hasa nikiona vijana wanavyosumbuka sababu ya ajira na taabu zote za kijamii.

Kanambia leo anawahi eti Maccm yanakujaga yanagawa nguo kwa wanafunzi bure halafu wanawapandisha kwenye gari wanaanza kutalii nao ili wawashangilie baadae wanawapa chakula na pesa kiasi fulani fulani.
nikaamuliza, Je, wanawaandika majina, akajibu ' hapana, wakija tu wanatugawia hivyo vitu baadae mnaondoka nao, mbona wanatusaidia sana kwakweli, viela ela hivi vidogo vidogo na chakula, aahhhh! si haba. pia tuna refresh kwa kutalii nao.

Jamani mimi machozi yamenitoa.

Toa na mavi kabisa,,nn machoziiiiiiiii
 
Kumefanyika kila jitihada kupotosha wapiga kura wasio wa CCM kama ifuatavyo:

Majina ya wapiga kura hayajabandikwa kokote, yameshikiliwa mikononi mwa watu. Ukifika utapewa baadhi ya karatasi, utatafuta jina asubuhi mpaka jioni hutaona jina lako maana karatasi nyingine zinafichwa.

Kumbuka wana CCM wote waliisha ambiwa mapema namba za majina yao, hivyo akifika tu anataja namba, anapewa karatasi za kupiga kura anondoka.

Karatasi za wapiga kura hazionyesi wazi wazi kutofautisha niipi ya mwenyekiti wa mtaa , ni ipi ya mjumbe na ipi ya mwakilishi viti maalum. inabidi osome kila andishi ndio mwisho unakuta wameandika kwa maadishi madogo kuwa hii ni ya mwenyekiti au mjumbe n.k.

Nani ana muda wa kusoma kila kitu katika karatasi hiyo? Kwa asilimia 80 kura zisizo za ccm zitawekwa kwenye maboxi yasiyosahihi. Wana ccm waliisha pewa hiyo semina hawawezi kuchanganya maboxi.

Maboxi hayakutofautishwa kwa rangi ya mifuniko. na karatasi za kupiga kura za mwenyekiti, mjumbe n.k hazikutofautishwa kwa rangi. Naandishi ya kuonyesha karatai ipi inaingia box lipi ni utata mtupu kwa wapiga kura wengi.

Yule anayetaka kuelekezwa kujua anatumbukiza katika boxi lipi inabidi ufungue karatasi ya kura aliyokwisha piga amuonyeshe polisi msimamizi ili aone hiyo karatasi inaingia box gani. Polisi akiona umechagua upinzani anukuelekeza uweke katika box ambalo sio, yaani kama ni kura ya mwenyekiti wa mtaa atakwambia weka box lileee, kumbe ni la wajumbe au viti maalum. moja kwamoja hiyo inakuwa batili.

Kwa ufupi, tupeleke watoto shule. CCM haikumaanisha uchaguzi halisi bali usanii tu. kwa hicho nilichokishuhudia, wanamageuzi hapa kambarage wategemee mfadhaiko wa nguvu.
 
Back
Top Bottom