Sheria itamke Marufuku Mtendaji wa Serikali kujihusisha na masuala ya uchaguzi

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,555
41,066
Wakati wote, sheria hubadilishwa ili kujibu matatizo ya wakati fulani.

Sahizi mjadala mkubwa umekuwa marekebisho ya sheria ya Uchaguzi kutokana na uhuni wa kupindukia ambao umekuwa ukifanyika kwenye uchaguzi.

Tunapoiangalia sheria, pia tuwaangalie wahusika wakuu waliokuwa wakiharibu maana ya uchaguzi.

Maadui wakubwa wa demokrasia ya uchaguzi na waporaji wa haki ya wananchi kuchagua viongozi wanaowataka, kwa miaka yote ambapo kumekuwa na uchaguzi wa kihuni, waliokuwa wakisimamia na kuhakikisha uhuni huo unafanikiwa ni wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Wilaya, Polisi na Watendaji wa Kata.

Kwa hiyo ni vema tukahakikisha sheria mpya ya uchaguzi inawaondoa kabisa maadui hawa wa demokrasia kwenye mchakato mzima wa uchaguzi. Hivyo ni vema sheria mpya ya uchaguzi ikatamka wazi kuwa ni marufuku Mkurugenzi wa Halmashauri, Mkuu wa Wilaya na OCD kujihusisha na masuala ya uchaguzi. Hawa wasionekane mahali popote panapohusika na uchaguzi. Siku ya kupiga kura, wakishapiga kura wasionekane kwenye kituo chochote cha kupigia kura wala ofisi yoyote inayohusika na masuala ya uchaguzi. Polisi watakaohusika na uchaguzi kwaajili ya kusimamia usalama, wapewe mafunzo ya muda mfupi juu ya namna shughuli zao za kusimamia usalama zinavyotakiwa kuzingatia sheria na kanuni za uchaguzi.

Sheria pia itamke kuwa kiongozi yeyote wa Serikali au Tume ya Uchaguzi atakayethibitika kuvuruga uchaguzi au kuzuia demokrasia kufanya kazi, atafungwa jela bila ya kuwepo adhabu mbadala. Siku ya kuingia jela achapwe fimbo 12 na siku ya kutoka achapwe fimbo 12 ili akamwoneshe mke wake au mumewe.

Tafadhali Mod: Isomeke "Sheria"
 
Ni ngumu sana kwa wapumbavu kusimamia kilicho bora,bali upumbavu wao huwa dhahiri na usio tia shaka.Dhamira zao zimejaa tamaa ya madaraka hivyo msingi wa taasisi ni tishio kwa maslahi yao.

"Huwezi muelimisha mpumbavu akaacha upumbavu wake"Mwl.Nyerere
JamiiForums-1059566392.jpg
 
Ni ngumu sana kwa wapumbavu kusimamia kilicho bora,bali upumbavu wao huwa dhahiri na usio tia shaka.Dhamira zao zimejaa tamaa ya madaraka hivyo msingi wa taasisi ni tishio kwa maslahi yao.

"Huwezi muelimisha mpumbavu akaacha upumbavu wake"Mwl.NyerereView attachment 2866672

Umenena vyema.

Kwa sasa ukiangalia, ni kama wanatafutwa wapumbavu kushika madaraka, na kusimamia mambo ya kitaifa ambayo, tena ni ya msingi kabisa kwa Taifa lolote.. Watu ambao uwezo wao wa akili unaishia kwenye kusema NDIYO, KUKARIRI, NA KUIMBA SIFA ZA KINAFIKI.
 
Back
Top Bottom