Yaliyojiri katika Uchaguzi Serikali za Mitaa - Dec 14, 2014

Wana JF
Habari zenyu bwana . Nipeni habari za mtaani kwenyu huko je ni mbaya kama hapa Kinyerezi ? Kata ya Kinyerezi eti imepokea karatasi na makabrasha ya kura za Kata ya Gerezani .Na Gerezani nadhani watakuwa wamepokea za Kinyerezi au Kata gani ila kwa kifupi kuna tatizo kubwa hadi muda huu niko kituoni hakuna kinacho endelea .

Hebu sema mtaani kwako kama wewe umesha wapa UKAWA kura tafadhali .
 

Ubarikiwe mkuu!
 
dah... mpka sasa hakijaeleweka.. eti wameleta fomu za wajumbe tuh..
wanatuambia tupige tuchague wajumbe kwanza alafu hizo nyingine wanatuletea badae turudi tena kuchagua wenyekiti.

Tabata Liwiti.
 
Hiyo Mbinu haitowasaidia sana hasa huko tuendako kwenye uchaguzi mkuu! Sanasana wanazidi kutupandishia hasira sisi wananchi na kupandisha hasira zetu dhidi ya hicho chama chakavu cha zamani
 
Wapi hukooo!!? Tujuze kamanda

mkuu ni hapa wilaya ya kilosa kijiji cha ruaha hali si shwari hapaa vuguvugu la vurugu linanukia mana wananchi wamekuwa wakali mnoo baada ya ccm kutaka wanyang'anya haki zao za msingi yani wamebadili wagombea wa chademaa na kuweka wanaowatambua wao sio ambao wananchi waliwapitishaa
 

Time will tell
 
hadi sasa naona wafanyabiashara waanza funga fremu zao na kuanza rejea makwao maana wameanza ona dalili za vurugu
 
Wanajf; amani iwe kwenu! Muda huu natoka kutimiza wajibu wangu wa kuchagua kiongoz nimtakaye lakini madudu niliyoyakuta huko bado tuna safari ndefu kufkia mabadiliko ya kweli! Kituo nilichopigia kura ni muheza mwisho kariakoo!
Kwanza tumeenda kupga kura tukiwa wanne lakn jambo la kushangaza mmoja wetu kaambiwa jna lake lishapigiwa kura! Nmemshauri xana akomae nao ili wampe haki yake ya kupga kura lakn anaonekana muoga xana kwahyo mpk xx haeleweki!
Pili, kampeni bado znaendelea hasa kwa ccm, maana kuna watu wanawaambia wazee wapgie chama wanachokipenda na wanataja kabsa kwamba pigia ccm na wanaenda mbali zaidi kwa kuonyesha sehemu ya kuweka tiki ambako wanaonyesha sehemu waliko wagombea wa ccm. Kwa kweli hili halijanifurahsha hata kidogo ukizingatia huu c muda wa kampeni!
Tatu, ni utaratbu wa kuwatambua wapga kura ndo umenipa mashaka xana! Ukienda ukataja jna lako na ni namba ngapi unapewa karatasi za kupigia kura! Hakuna uhakiki wa sura wala kuombwa kitambulisho cha kupgia kura! Hili jambo litafanywa mamluki wengi kuoga kura zaidi ya mara moja au watapga kura hata ambao hawakujiandkisha maana mitaa hii watu ni wengi xana km mjuavyo mitaa ya kariakoo!!!!
Ni hayo tu wanajamvi niliyaona ktk kituo cha kupgia kura!!!!
 

Kama Shariff Shamba Ilala Jijini Dar es Salaam ambapo ki kitovu cha kila kitu, vifaa havijapatikana kwa wakati hadi uchaguzi kuahirishwa; hali ikoje huko Umugakorongo - Bukoba, Mitomoni - Ruvuma, Kasanga - Rukwa, Robanda - Mara?

 
Nipo kituo cha kawe wilaya ya kinondoni hali ilikuwa si shwari asubuhi baada ya watu kuambia wapige kula bila kuwepo kwa wino wa kupaka kidoli wananchi walichachamaa ila kwa sasa zoezi lipo salama kabisa
 
Uchaguzi mtaa wa mtambani - vingunguti dsm umehairishwa kisa ukosekanaji wa vitendea kazi. Baadhi ya raia waliokuwa wakipinga hatua hiyo, tayari wamewekwa nguvuni.
 
wadau ccm wamebanwa kila kona,wameamua kuwawekea wagombea nembo zisizo za vyama vyao ili kutupotosha wananchi.
Wagombea wa NCCR-MAGEUZI Wawekewa nembo za CHADEMA.
Mf: n kijiji cha SHUNGA
Source: mm mwenyewe npo huku
 

Mkuu,nipo Hapa mtaa wa Isandula magharibi na huo mtaa upo jirani,wote tumeskitishwa sana na vitendo hivyo vya kihuni vinavyofanywa na maccm. Ninachoweza kuwajuza tu hawa vibaraka wa mafisadi ni kuwa cdm tumejipanga kuchukua mitaa yote inayounda mamlaka ya mji mdogo na tuna hasira sana ya kuhujumu na kuengua wagombea wetu katika mitaa miwili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…