Yaliyojiri katika Uchaguzi Serikali za Mitaa - Dec 14, 2014

Wana JF
Habari zenyu bwana . Nipeni habari za mtaani kwenyu huko je ni mbaya kama hapa Kinyerezi ? Kata ya Kinyerezi eti imepokea karatasi na makabrasha ya kura za Kata ya Gerezani .Na Gerezani nadhani watakuwa wamepokea za Kinyerezi au Kata gani ila kwa kifupi kuna tatizo kubwa hadi muda huu niko kituoni hakuna kinacho endelea .

Hebu sema mtaani kwako kama wewe umesha wapa UKAWA kura tafadhali .
 
💥WAZO LA LEO💬:

Ukiona MTOTO unamtuma dukani halafu harudishi CHENJI ujue huyo ukubwani atakuwa MTAFUTAJI mzuri; Ni jambo jema mtie MOYO. Ukiona MTOTO anapiga wenzake ujue chuyo ni BONDIA wa baadae ni jambo jema usimpige. Ukiona MTOTO unampeleka shule za gharama lakini kichwani bado MBULULA! ujue huyo ukubwani atakuwa "MCHEZAJI WA TAIFA STARS" si mbaya sana. Ukiona mtoto anakuwa na tabia za "UONGO, WIZI WA MBOGA, MBISHI SANA" ujue huyo ukubwani atakuwa KADA wa CCM usimtie moyo CHARAZA VIBOKO maana watatuharibia Nchi yetu!!

Haya amka sasa, Kamata bakora yako(kalamu), nenda kituo cha kupigia kura, kamcharaze bakora zako mgombea wa CCM kwa kupeleka kura yako UKAWA!!

Nkutakie Uchaguzi Mwema!!

Ubarikiwe mkuu!
 
dah... mpka sasa hakijaeleweka.. eti wameleta fomu za wajumbe tuh..
wanatuambia tupige tuchague wajumbe kwanza alafu hizo nyingine wanatuletea badae turudi tena kuchagua wenyekiti.

Tabata Liwiti.
 
Hiyo Mbinu haitowasaidia sana hasa huko tuendako kwenye uchaguzi mkuu! Sanasana wanazidi kutupandishia hasira sisi wananchi na kupandisha hasira zetu dhidi ya hicho chama chakavu cha zamani
 
Wapi hukooo!!? Tujuze kamanda

mkuu ni hapa wilaya ya kilosa kijiji cha ruaha hali si shwari hapaa vuguvugu la vurugu linanukia mana wananchi wamekuwa wakali mnoo baada ya ccm kutaka wanyang'anya haki zao za msingi yani wamebadili wagombea wa chademaa na kuweka wanaowatambua wao sio ambao wananchi waliwapitishaa
 
Unaweza kusema CCM inalazimisha mapenzi kwa wananchi. Wananchi wameichoka. Wananchi hawaipendi CCM. Leo nimefika katika kituo changu nilichojiandikishia kupiga kura hapa jijini Mbeya, nikiwa na hamu kabisa ya kutumia haki ya msingi kumchagua kiongozi nimtakaye. Mbali na mimi niliwakuta pia wananchi wengine waliokuwa kituoni kwa lengo hilo hilo. Cha ajabu na cha kusikitisha tunaambiwa hakuna kupiga kura, kisa mgombea wa CCM amepita bila kupingwa. Kwamba mgombea wa UKAWA alienguliwa katika hatua za mwishoni kwa kutokutimiza taratibu za wagombea. Wananchi tukasema basi tumpigie kura huyo huyo wa CCM kuonesha kama tunamtaka yeye au la, wasimamizi wakasema kanuni haziruhusu kufanya hivyo! Tunajua hizo ni hila za CCM kuengua wagombea wa vyama vinavyounda ukawa kiujanja ujanja lakini naomba niwaambie kuwa kufanya hivyo ni sawa na kulazimisha mapenzi kwa wananchi! Kufanya hivyo ni sawa na mwanaume kulazimisha mapenzi kwa mwanamke ilihali hakutaki au kinyume chake! Naomba CCM wajue kuwa wakati wa kuongoza watapata shida kwani watakuwa wanaongoza wananchi wasiowapenda!

Time will tell
 
hadi sasa naona wafanyabiashara waanza funga fremu zao na kuanza rejea makwao maana wameanza ona dalili za vurugu
 
Wanajf; amani iwe kwenu! Muda huu natoka kutimiza wajibu wangu wa kuchagua kiongoz nimtakaye lakini madudu niliyoyakuta huko bado tuna safari ndefu kufkia mabadiliko ya kweli! Kituo nilichopigia kura ni muheza mwisho kariakoo!
Kwanza tumeenda kupga kura tukiwa wanne lakn jambo la kushangaza mmoja wetu kaambiwa jna lake lishapigiwa kura! Nmemshauri xana akomae nao ili wampe haki yake ya kupga kura lakn anaonekana muoga xana kwahyo mpk xx haeleweki!
Pili, kampeni bado znaendelea hasa kwa ccm, maana kuna watu wanawaambia wazee wapgie chama wanachokipenda na wanataja kabsa kwamba pigia ccm na wanaenda mbali zaidi kwa kuonyesha sehemu ya kuweka tiki ambako wanaonyesha sehemu waliko wagombea wa ccm. Kwa kweli hili halijanifurahsha hata kidogo ukizingatia huu c muda wa kampeni!
Tatu, ni utaratbu wa kuwatambua wapga kura ndo umenipa mashaka xana! Ukienda ukataja jna lako na ni namba ngapi unapewa karatasi za kupigia kura! Hakuna uhakiki wa sura wala kuombwa kitambulisho cha kupgia kura! Hili jambo litafanywa mamluki wengi kuoga kura zaidi ya mara moja au watapga kura hata ambao hawakujiandkisha maana mitaa hii watu ni wengi xana km mjuavyo mitaa ya kariakoo!!!!
Ni hayo tu wanajamvi niliyaona ktk kituo cha kupgia kura!!!!
 
Wakuu kumekucha, leo, Disemba 14, 2014 Watanzania wanapiga kura kuchagua viongozi wao wa Serikali za Mitaa. Viongozi wanaochaguliwa leo ni katika nafasi za Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, Wenyeviti wa Vitongoji, Wajumbe 6 wa Serikali ya Mtaa (Halmashauri) na wajumbe wa Viti Maalum wa Mtaa/Kijiji.

Kama ilivyo ada JamiiForums itakuwa ikikujuza yanayojiri, katika uzi huu utapata/utaleta updates zinazohusiana na uchaguzi huu.

Karibuni sana

========
UPDATES MUHIMU:

- Eneo la Shariff Shamba, Ilala jijini Dar uchaguzi umeahirishwa mpaka Jumapili ijayo baada ya vifaa kutopatikana ndani ya muda. Vyama vyote vinavyoshiriki vimeafikiana


- Mgombea wa CHADEMA Kijiji cha Darajani huko Liwale, M. Manakwa amepigwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo, amelazwa hospitali

Kama Shariff Shamba Ilala Jijini Dar es Salaam ambapo ki kitovu cha kila kitu, vifaa havijapatikana kwa wakati hadi uchaguzi kuahirishwa; hali ikoje huko Umugakorongo - Bukoba, Mitomoni - Ruvuma, Kasanga - Rukwa, Robanda - Mara?

 
Nipo kituo cha kawe wilaya ya kinondoni hali ilikuwa si shwari asubuhi baada ya watu kuambia wapige kula bila kuwepo kwa wino wa kupaka kidoli wananchi walichachamaa ila kwa sasa zoezi lipo salama kabisa
 
Uchaguzi mtaa wa mtambani - vingunguti dsm umehairishwa kisa ukosekanaji wa vitendea kazi. Baadhi ya raia waliokuwa wakipinga hatua hiyo, tayari wamewekwa nguvuni.
 
wadau ccm wamebanwa kila kona,wameamua kuwawekea wagombea nembo zisizo za vyama vyao ili kutupotosha wananchi.
Wagombea wa NCCR-MAGEUZI Wawekewa nembo za CHADEMA.
Mf: n kijiji cha SHUNGA
Source: mm mwenyewe npo huku
 
Mgombea wa kitongoji cha Isandula juu kupitia CHADEMA ndugu Kasema amevamiwa usiku wa kuamkia leo tarehe 14/12/2014 na kukatwa katwa mapanga sehemu mbali mbali za mwili wake hali iliyompelekea kupoteza fahamu.

Ndugu Kasema anatarajiwa kushinda kitongoji hicho kutokana na nguvu kubwa aliyonayo, siku kadhaa zilizopita alifuatwa na viongozi wa ccm na kumtishia maisha iwapo ataendelea na msimamo wake wa kujitoa katika kinyang'anyiro hicho.

Hivi sasa amelazwa katika hospital ya Magu akiendelea kupatiwa matibabu. Tunamwombea kwa Mungu apone ili aendelee na harakati za ukombozi wa kitongoji chake

Mkuu,nipo Hapa mtaa wa Isandula magharibi na huo mtaa upo jirani,wote tumeskitishwa sana na vitendo hivyo vya kihuni vinavyofanywa na maccm. Ninachoweza kuwajuza tu hawa vibaraka wa mafisadi ni kuwa cdm tumejipanga kuchukua mitaa yote inayounda mamlaka ya mji mdogo na tuna hasira sana ya kuhujumu na kuengua wagombea wetu katika mitaa miwili.
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom